Je, wajua kuna uwezekano Barrick wanatuingiza mkenge?!. Hili la kugawana 50/50 ya faida ni kweli au ni changa la macho tu?.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,468
113,583
Wanabodi,

Leo tena nimepata fursa ya kuendelea na zile makala zangu za kwa maslahi ya Taifa, nikiendelea kujikita katika ulinzi wa rasilimali zetu dhidi ya hadaa na ulaghai tunaotaka kufanyiwa na Barrick Gold na binti yake Acacia kupitia kitu kinachoitwa majadiliano yanayoendelea na yasiyokwisha, baada ya kufikiwa kwa makubaliano ambayo mezani walikubaliana tutagawana faida 50/50. Jee ni kweli tutagawana faida ya Acacia 50/50 au hii taarifa kuwa tutagawa faida ni changa tuu la macho?, yaani tunadanganywa kama watoto wadogo kudanganyiwa pipi?!

Declaration of Interest
Baadhi ya Watanzania tuna matatizo ya uelewa na haswa kushindwa kuzibaini alama za kuuliza maswali. Mada hii ni swali nikiuliza, "Jee wa Wajua Kuna Uwezekano Barrick Wanatuingiza Mkenge?!. Hili la Kugawana 50/50 ya Faida ni Kweli au ni Changa la Macho Tuu?". Nawaombeni sana msome alama ya kuuliza kwenye mada zangu, mwenzetu sitaki tena kuitwa mahali popote na kuhojiwa tena kuwa nimesema jambo fulani!, hapa sijasema jambo lolote, bali nimeuliza swali la kuhusu jambo fulani, mwenye majibu atoe!.

Jee ni Nini Haswa Kilichokubaliwa Kwenye Makubaliano na Barrick Kuwa Tutagawana 50/50?.
Sisi Watanzania tulielezwa na rais wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, akalitangazia taifa tena akiwa mubashara kabisa kwenye redio na TV ili mwenye macho aone, na mwenye masikio asikie kuhusu habari njema hii, ya kugawana faida kwa 50/50!. Mwenyekiti wa Barrick naye akaitangaza kwa kinywa chake pale pale ikulu, taarifa rasmi ya ikulu ikaeleza tutagawana faida 50/50 na waziri wa Sheria aliyeongoza timu ya Tanzania, kwenye majadiliano hayo, Prof. Palamagamba Kabudi akatoa ufafanuzi mzuri kabisa.Lakini katika taarifa yao rasmi kuhusu ni nini kilichokubaliwa, wote wawili Barrick na binti yake Acacia wakageuza kibao, badala ya kusema tutagawana faida kwa 50/50, wao wamesema na kuandika tutakacho gawana ni 50/50 ya economic benefits na sio 50/50 faida!. Hii maana yake unaondoa gharama zote za uendeshaji, halafu kinacho patikana ndicho mnagawa 50/50!. Ndani ya hiyo 50/50 kutakuwepo kodi zote, na ile asilimia 16% ya free carried shares za serikali.

Kitakacho fanyika, kwanza gharama za uendeshaji zitakuwa juu, management watalipana super salaries, consumables zote zitaangizwa kutoka Canada au London na kuambiwa za kwetu ni low quality, hivyo kitakachobaki kugawana 50/50 kitakuwa kama sio nothing, the ni almost peanut!.
Waandishi Wa Wazuri wa Habari, Sio Tuu wana Nose for News, Bali Wengine Wana Jicho la Tatu Kuona Visivyoonekanika Kwa Jicho La Kawaida!.
Serikali yetu lazima ijifunze kusikiliza na kufuatilia taarifa za media ikiwemo mitandao ya kijamii. Sisi waandishi wa habari kwanza ni watu tuu wa kawaida, kama watu wengine wowote, ila ili uwe mwandishi mzuri wa habari, unakubidi uwe na kitu cha ziada kuliko watu wa kawaida tuu, kitu hicho kinaitwa "a nose for news", uwe na pua ya kunusa kuwa hapa kuna habari.

Waandishi wa Habari ni Jicho la Tatu na Daraja la Kiunganishi Kati ya Serikali na Jamii.
Naiomba sana serikali yetu iheshimu sana vyombo vya habari na kuwaheshimu waandishi wa habari kwa sababu ndio kiungo kati yake na jamii, media inaripoti kinachofanywa na serikali hivyo jamii kufahamu, na wakati huo huo ndilo jicho la serikali ndani ya jamii kwa kuripoti vitu ambavyo jicho la serikali haliwezi kuviona, kama hili la kugawana 50/50 ya faida na Acacia, tunataka kupigwa changa la macho la kugawana 50/50 ya economic benefits na sio tena ya faida!.

Miongoni mwetu sisi waandishi, wengine wana jicho la tatu la kuona vile sivyoonekanika kwa jicho la kawaida. Hawa ndio huwa investigative journalists ambao kama wasingekuwa waandishi wangekuwa police investigators.

Kupitia jicho la tatu, nimeona kabisa serikali yetu ikidanganywa mchana kweupe na sasa inataka kuingizwa mkenge!. Kwa vile makubaliano ya mwisho bado hayajafikiwa na mazungumzo yanaendelea yakielezwa yamefikia katika hatua nzuri, kwanza naomba tuelezwe na serikali yetu, mazungumzo haya yamefikia wapi, yako hatua gani?, pili sintofahamu ya mgawo wa 50/50 ni ya faida au economic benefits?. ufafanuliwe, na tatu naomba kutoa angalizo muhimu kwa serikali yetu kuwa tunadanganywa na Barrick mchana kweupe, na tusipokuwa makini, tutaingizwa mkenge na kupigwa wazima mazima mchana kweupe!

Its High Time Tanzania Pia Tujikite Kwenye Inteligensia ya Kiuchumi.
Wenzetu wazungu wanatumia hadi mashine za kubaini kauli za uongo zinazoitwa lie detectors, lakini kuna watu wenye jicho la tatu, wanauwezo wa kugundua kuwa mtu fulani anasema uongo, au anadanganya au anatania, hivyo kupitia jicho langu la tatu, naomba kujibainisha wazi, kuieleza serikali yetu na viongozi wetu na wajumbe wa kamati ya majadiliano kuwa kama sio viongozi wetu wametudanganya kuwa tutagawana 50/50 ya faida, then Barrick ndio wanawadanganya, na kama Barrick ndiye anayedanganya, hatupaswi kupiga kelele kwa nini tumedanganywa, tujikite zaidi katika kubaini the motive behind Barrick moves!, zamani concentration ya intelligence yetu ilijikita kwenye security intelligence, kulinda usalama wa taifa!, Tanzania inaelezwa ni moja ya nchi nzuri yenye inteligensia nzuri ya usalama wa taifa ndio maana tuko very stable security wise, lakini katika intelligence ya kiuchumi, kiukweli kabisa, we are very poor, ndio maana tukapigwa kwenye rada, ndege ya rais, vifaa vya kijeshi, EPA, Escrow, Deep Green, Tan Gold, DCP, na mascandle mengine kibao. Tungekuwa hata na minimum inteligence ya kiuchumi, by now tungekuwa tunajua bei ya container moja la makinikia sokoni ni kiasi gani?, gharama za kuchenjua ni kiasi gani, na mchanga huo ukiisha chenjuliwa, ni nini kinapatikana, na kujua Acacia wanapata nini?.

Its high time sasa na sisi Tanzania, tujikite kwenye economic intelligence, kama mimi tuu a layman mwandishi wa kujitegemea nimebaini kuna ka mchezo tunachezewa, hawa watu wetu wa intelligence wanafanya nini?!, by the time tunakuja kugundua kuwa tunachezewa mchezo, it might be too little too late!.

Kati ya Serikali Yetu na Barrick, Kuna Mtu ni Muongo, Kuna Mtu Kadanganya, Kuna Mtu Kadanganywa na Kadanganyika!.
Nimemsikiliza kwa makini sana Rais Magufuli akizungumzia hili la kugawana faida 50/50

Prof. Kabudi akitoa ufafanuzi wa kilichokubaliwa mezani!, kupitia jicho la tatu, ukimsikiliza Kabudi kwa makini akizungumzia walichukubaliana, utakubaliana na mimi kuwa Prof. Kabudi ni mkweli 100%, anachokisema hapa ndicho kitu cha kweli walichokubaliana kwenye meza ya majadiliano. Hivyo alichokisema rais wetu Magufuli kuhusu kugawana faida 50/50 ndicho alichoeleza na Prof. Kabudi, na kilicho andikwa kwenye taarifa rasmi ya Ikulu, ni kile rais wetu alichokisema, hivyo as of now bado msimamo wa Watanzania ni tutagawa faida 50/50.


Bosi wa Barrick Yuko Very Conscious, Makini!, Prof. Wetu na Rais Wetu, Wamehamanika!.
Pia nimemsikiliza bosi wa Barrick Prof. Richard Thontom, ukimwangalia body language yake wakati akizungumza, yuko very Consciously, anazungumza kwa kituo na kuchagua maneno kwa makini!, sisi viongozi wetu wamehamanika, sii waziri sii rais!. Boss wa Barrick amesema tutagawa 50/50 bila kusema ni 50/50 ya nini, ni ya faida au ni ya economic benefits. Huyu Prof wao, amesisitiza sana msingi wa majadiliano na makubaliano hayo ni uaminifu na uwazi, trust and transparency. Nimemuangalia kwa makini huyo Prof akizungumza na kumnote kuwa japo anaongea kwa lugha ya Kiingereza na mkalimani anatafsiri kwa let lugha ya Kiswahili, lakini hili li jamaa pia linasikia Kiswahili!, hivyo humdanganyi kitu!. Lilikuwa likisema neno fulani, halafu mkalimani asilitafsiri, hurudia alichosema hadi mkalimani atafasiri. Alipotoa ahadi ya zawadi ya dola milioni 300, mkalimani akakosea kuitafsiri kiwango!, jamaa likamtizama mkalimani na kumsisitizia ni dola milioni 300!.


Everything in Black and White, Maximum Transparency,
Ili kuweka rekodi vizuri na uwazi, (to put records clear), wenzetu wazungu kila walichokubaliana hukiweka in black and white, yaani kwenye maandishi. Hivyo baada ya kauli zile pale ikulu na makubaliano yale, wenzetu wazungu, wote wawili, baba na binti yake, walichapisha kilichokubaliwa na kukiweka kwenye website zao, katika maandishi yao, kipengele cha kugawana 50/50 kimeeleza wazi ni economic benefits na sio faida!. Kwa vile makubaliano ya mwisho yanafuata maandishi ya kilichokubaliwa awali, na sio kauli za Prof Kabudi na rais wetu, hivyo sasa kitakachoelezwa kuwa tumekubaliana ni 50/50 ya economic benefts na sio 50/50 ya faida!, hii itamfanya Prof. wetu Kabudi kuonekana ni muongo!, na rais wetu alichotungazia pale ikulu pia kuonekana ni uongo!. Watanzania tusikubali waziri wetu kuonekana ni muongo, au rais wetu kuonekana alitueleza kitu cha uongo kuhusu kugawana faida 50/50!. Tangu kutokea kwa kadhia hii, Acacia wametoa taarifa mara 54 kwenye website yao, sisi tumesema nothing zaidi taarifa ya Ikulu.
Barrick Gold Corporation - Barrick Comments on Proposed Framework for Acacia Mining plc Operations in Tanzania
Usiri wa Nini Katika Rasilimali za Taifa?. Kwanini Sisi Tumenyamaza na Tunaficha Wenzetu Wanaonyesha?.
Ufike Wakati Sasa Mikataba Yote ya Rasilimali za Taifa Iwe Wazi na Ipitishiwe Bungeni Kuridhiwa!.

Anapotokea mtu na kukutwanga ngumi, kisha wewe ukatulia tuu na kusamehe, aliyekutwangwa ngumi akatangulia polisi na kuripoti kuwa ameshambuliwa na wewe, kwa vile wewe hukuripoti, unafuatwa, utalazwa ndani na kama hakuna shahidi aliyeona, itakula kwako!.

Vivyo hivyo kile tulichokubaliana mezani na Barrick kuwa tutagawana, lakini sisi hatukukiweka kwenye maandishi in black and white, na haturipoti progress report yoyote tumekalia usiri!, usiri gani katika rasilimali za taifa?. Yule anayetangulia kuweka mambo hadharani, very transparently in black and white na kuweka kila kitu very open and very transparent, ndiye mkweli na wewe na usiri wako kuonekana muongo. Katika nia njema ya kulinda rasilimali zetu, ufike wakati sasa mikataba yote inayohusu resilimali za taifa, ijadiliwe kwa ukweli na uwazi, na ikibidi ipitishwe bungeni na kuridhiwa na wawakilishi wa wananchi ambao ndio wenye mali. Usiri wa nini katika rasilimali za taifa?.

A Way Forward Katika Hoja ya 50/50 ni Faida au Economic Benefits?.
Nashaushi hapa tufuate kanuni ya wazungu ya truthful, trust na transparency, kunapotokea kutoelewana kwenye matokeo ya majadiliano yoyote, kinachofanyika ni kurejea kwenye meza ya mazungumzo, back to the drawing board, jee walipokaa walikubaliana kugawana 50/50 ya nini?. Jee ni kugawana faida au economic benefits?, kama walikubaliana ni kugawana faida, serikali yetu haikupaswa kuzinyamazia taarifa za Barrick na Acacia kuwa watagawana 50/50 ya economic benefits na kuwalazimisha Barrick na binti yake Acacia wafute kauli zao kuwa tunachogawana ni 50/50 ni net profits baada ya kutoa costs zote na kodi zote. Na kama walichokubaliana ni 50/50 ya economic benefits, then Prof. Kabudi itambidi tuu ajitokeze tena na kufafanua upya ikiwemo kuwaomba radhi Watanzania na kumpotosha rais wetu kwa 50/50 ya economic benefits kuuita ni 50/50 ya faida!, hapa ata sight tuu matatizo ya uelewa ligha za wenzetu na haswa kwa kuzingatia IQ za baadhi ya makabila, unakuta mtu ni professor mzima, lakini hajui, tofauti ya economic benefts, na net profit, yeye kaambiwa economic benefts, kaja kusema ni net profits, na Watanzania tutamuelewa kabisa!.

Issue ya Kile Kishika Uchumba cha Dola Milioni 300/
Kwa vile Watanzania tulimsikia wenyewe kwa masikio yetu, wala hatukuomba, naomba kabla ya kufikiwa kwa makubaliano yoyote, hatua ya kwanza ni huu mzigo wa dola milioni 300, uwekwe kwanza mezani, kuwapooza wajomba machungu ya binti yao kuzalishwa kwanza, ndipo kuposwa. Hii habari ya Acacia kuwa italipa baada ya kutoa madeni yake, iishie huko huko Acacia, maadam Prof wa Barrick aliahidi, then he must honour his promise!.

Kutokuwepo Kwa Acacia Kama Sehemu ya Mazungumzo.
Hapa ndipo dili nzima ya changa la macho itakapochezewa!. Kila statement kuna line inayosisitiza Acacia is not involved na kusisitiza chochote kitakachokubaliwa, ni lazima kiwe approved na independent commitee ya bodi ya Acacia!. Kwa maoni yangu, Baba Barrick na Binti yake Acacia wanajuana, binti kaharibu, Baba anakuja kumkingia kifua, na baba kuja kwenye meza ya mazungumzo bila binti yake, huyu baba anaweza kutuahidi hata dunia, kisha akamwambia binti yake, wewe kataa, usitekeleze!. Kwenye hili, naomba serikali yetu isikubali kufikia makubaliano yoyote na Barrick kama Acacia haiko mezani!, isisitize, makubaliano yoyote yatakayofikiwa, utekelezaji wa kwanza ni kodi yetu ya ilipwe ndipo mengine yafuate!.

Hitimisho.
Huko nyuma tulipigwa na tukapigika!. Na sasa kwenye mazungumzo haya, kupitia jicho la tatu, naona kabisa kuwa tunataka kupigwa!, naziona kila dalili za Barrick kuuza shares zake zote za Acacia kwa Wachina, atakayenunua atadai hajui lolote kuhusu mazungumzo ya Barrick na GoT, hivyo tutarudi back to squire one. Ila tukija kwenye economics principles, mtu unamiliki shares asilimia 16% mwingine anamiliki shares asilimia 84% halafu mgawane faida 50/50!, this will be only in Tanzania kwa sababu it doesn't make any sense and its not logical, hivyo kwenye hili la kugawana 50/50 sorry to say Ph.D ya sheria na Ph.D ya kemia lugha ya watu piga chenga, hawajui tofauti ya economic benefits, wao wameita ni profits, hili kosa la lugha za watu ni kosa dogo linasameheka, ukweli ni tutagawana 50/50 ya economic benefits na sio 50/50 ya faida.

This is just a wake up call!, its not too late kuchukua tahadhari!.

Nawatakia Furahi Day Njema.
Paskali
 
Nilichoelewa mimi kwa kadiri ya andiko la Barrick na Acacia, kitakachogawanywa 50/50 ni economic benefits na siyo financial benefits. Na wala sidhani kama tutagawana 50/50 ya net profit.

Economic benefits zinazoongelewa ni kama vile ajira. Kampuni ile itakayoanzishwa itakuwa na uwakilishi wa 50/50, hizo ndizo miongoni mwa hizo economic benefits zinazotajwa lakini siyo mgawanyo wa pesa ya faida.

Jambo jingine la msingi ni kuwa yale hayakuwa makubaliano ya utekelezaji bali ni MAKUBALIANO YA MAPENDEKEZO. Mapendekezo yale ilibidi kwanza yapitishwe na Board ya Barrick kama mapendekezo yaliyokubaliwa na Barrick kupelekwa ACACIA. Kule ACACIA mapendekezo yale yaliyokubaliwa kuwa Mapendekezo ya Kupeleka ACACIA, yatapokelewa kama mapendekezo na siyo kama maamuzi. MAPENDEKEZO YANAWEZA KUKUBALIWA, KUKATALIWA AU KUTAKA YAFANYIWE MAREKEBISHO. Kama INDEPENDENT COMMITTEE YA ACACIA ikapendekeza yafanyiwe marekebisho ili yaweze kukubaliwa, katika hali ya kawaida yatapitia njia ile ile mpaka kuifikia serikali ya Tanzania. Na kisha yapiye kwenye mnyororo ule ule kuweza ku8fikia ACACIA.

Ni vema WATANZANIA tukaendelea na shughuli zetu za kuutafuta mkate wetu wa kila siku kuliko kufikiria kuwa kuna mabilioni yatadondoka toka ACACIA. Tuliwaita, tukasaini nao mikataba, wakatenda kwa kadiri ya mikataba, sasa tunapiga kelele. Upenyo wetu wa kupata zaidi upo katika kushawishi na kubembeleza lakini siyo katika nguvu za kisheria.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Barrick na Acacia watoto wa mjini weka mbali na hao wakamua mafuta ya maganda ya korosho...

Jiwe ni mbishi angemwelewa yule toto tundu sasa hivi angekuwa ameshakula matunda sgr ingekuwa manyoni sasa hivi, angekuwa ameajiri walimu na madaktari wote plus million 50 kila kijiji hafu baada ya hapo angewaambia upinzani wachague tume yao ya uchaguzi ambayo wanaamini itakuwa huru, nakwambia angeshinda mapema tu lakini sasa hivi kusurvive kwake ni kutumia jeshi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kala Maganda na Vibudu alishasema nyumba yenye pesa ndo inaingiliwaga na wezi. Nadhani kishika uchumba kishatolea kabisa japokuwa zile balimi zetu ndo hivyo tena bila kusahau ile noah yangu ya khaki naendelea kuisubiri

NB: Pascal hapo kwenye interest naomba uombe radhi kwa kusema watanzania tuna matatizo ya kuelewa
 
Mimi nashukuru Mungu kuniweka hai na kushuhudia moja wa manabii katika ardhi hii, niliwasoma akina nabii Isaya, Yeremia nk nikadhani hawakuwa watu wa kawaida, nikawa napiga picha akilini kwamba nabii lazima awe na ndevu nyingi, awe na fimbo mkononi, awe na mshipi kiunoni, awe na nguo kama kanzu na avalie katambuga si unajua movie za kina Musa na Yohane ziliniharibu mtazamo. Lakini nimeona moja wa manabii makini kabisa akivalia kisasa kabisa bila kusahau koti na miwani machoni.
 
Wanabodi,

Leo tena nimepata fursa ya kuendelea na zile makala zangu za kwa maslahi ya Taifa, nikiendelea kujikita katika ulinzi wa rasilimali zetu dhidi ya hadaa na ulaghai tunaotaka kufanyiwa na Barrick Gold na binti yake Acacia kupitia kitu kinachoitwa majadiliano yanayoendelea na yasiyokwisha, baada ya kufikiwa kwa makubaliano ambayo mezani walikubaliana tutagawana faida 50/50. Jee ni kweli tutagawana faida ya Acacia 50/50 au hii taarifa kuwa tutagawa faida ni changa tuu la macho?, yaani tunadanganywa kama watoto wadogo kudanganyiwa pipi?.

Declaration of Interest
Baadhi ya Watanzania tuna matatizo ya uelewa na haswa kushindwa kuzibaini alama za kuuliza maswali. Mada hii ni swali nikiuliza, "Jee wa Wajua Kuna Uwezekano Barrick Wanatuingiza Mkenge?!. Hili la Kugawana 50/50 ya Faida ni Kweli au ni Changa la Macho Tuu?". Nawaombeni sana msome alama ya kuuliza kwenye mada zangu, mwenzetu sitaki tena kuitwa mahali popote na kuhojiwa tena kuwa nimesema jambo fulani!, hapa sijasema jambo lolote, bali nimeuliza swali la jambo fulani, mwenye majibu atoe!.

Jee ni Nini Haswa Kilichokubaliwa Kwenye Makubaliano na Barrick Kuwa Tutagawana 50/50?.
Sisi Watanzania tulielezwa na rais wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, akalitangazia taifa tena akiwa mubashara kabisa kwenye redia na TV ili mwenye macho aone, mwenye masikio asikie kuhusu habari njema hii, ya kugawana faida kwa 50/50!. Mwenyekiti wa Barrick naye akaitangaza kwa kinywa chakepale pale ikulu, taarifa rasmi ya ikulu ikaeleza tutagawana faida 50/50 na waziri wa Sheria aliyeongoza timu ya Tanzania, kwenye majadiliano hayo, Prof. Palamagamba Kabudi akatoa ufafanuzi mzuri kabisa.Lakini katika taarifa yao rasmi kuhusu ni nini kilichokubaliwa, wote wawili Barrick na binti yake Acacia wakageuza kibao, badala ya kusema tutagawana faida kwa 50/50, wamesema na kuandika tutakacho gawana ni 50/50 ya economic benefits na sio 50/50 faida!. Hii maana yake unaondoa gharama zote za uendeshaji, halafu kinacho patikana ndicho mnagawa 50/50!. Ndani ya hiyo 50/50 kutakuwepo kodi zote, na ile asilimia 16% ya free carried shares za serikali.

Kitakacho fanyika, kwanza gharama za uendeshaji zitakuwa juu, management watalipana super salaries, consumables zote zitaangizwa kutoka Canada au London na kuambiwa za kwetu ni low quality, hivyo kitakachobaki kugawana 50/50 kitakuwa ni almost peanut!.

A Way Forward Katika Hoja ya 50/50 ni Faida au Economic Benefits?.
Nashaushi hapa tufuate kanuni ya wazungu ya truthful, trust na transparency, kunapotokea kutoelewana kwenye matokeo ya majadiliano yoyote, kinachofanyika ni kurejea kwenye the drawing board, jee walipokaa walikubaliana kugawana nini 50/50?. Jee ni kugawana faida au economic benefits, kama walikubaliana ni kugawana faida, serikali yetu haikupaswa kuzinyamazia taarifa za Barrick na Acacia kuwa watagawana 50/50 ya economic benefits na kuwalazimisha Barrick na binti yake kuwa tunachogawana 50/50 ni net profits baada ya kutoa costs zote na kodi zote. Na kama walichokubaliana ni 50/50 ya economic benefits, then Prof. Kabudi itambidi tuu ajitokeze tena na kufafanua upya ikiwemo kuwaomba radhi Watanzania na kumpotosha rais wetu kwa 50/50 ya economic benefits kuuita ni 50/50 ya faida!, hapa ata sight tuu matatizo ya uelewa ligha za wenzetu na Watanzania tutamuelewa!.

Issue ya Kile Kishika Uchumba cha Dola Milioni 300/
Kwa vile Watanzania tulimsikia wenyewe kwa masikio yetu, wala hatukuomba, naomba kabla ya kufikiwa kwa makubaliano yoyote, hatua ya kwanza ni huu mzigo wa dola milioni 300, uwekwe kwanza mezani, kuwapooza wajomba machungu ya binti yao kuzalishwa kwanza, ndipo kuposwa. Hii habari ya Acacia kuwa italipa baada ya kutoa madeni, iishie huko huko Acacia, maada aliahidi, he must honour his promise!.

Kutokuwepo Kwa Acacia Kama Sehemu ya Mazungumzo.
Hapa ndipo dili nzima ya changa la macho itakapochezewa!. Kila statement kuna line inayosisitiza Acacia is not involved na kusisitiza chochote kitakachokubali, lazima kiwe approved na independent commitee ya bodi ya Acacia!. Kwa maoni yangu, Baba Barrick na Binti yake Acacia wanajuana, kwa upande huu baba anaweza kutuahidi hata dunia, kisha akamwambia binti yake, usitekeleze!. Kwenye hili, naomba serikali yetu isisitize, makubaliano yoyote yatakayofikiwa, utekelezaji wa kwanza ni kodi yetu ya ilipwe ndipo mengine yafuate!.

Hitimisho.
Huko nyuma tulipigwa na tukapigika!. Na sasa kwenye mazungumzo haya, kupitia jicho la tatu, naona kabisa kuwa tunataka kupigwa!, naziona kila dalili za Barrick kuuza shares zake zote za Acacia kwa Wachina, atakayenunua atadai hajui lolote kuhusu mazungumzo ya Barrick na GoT, hivyo tutarudi back to squire one.

This is just a wake up call!, its not too late kuchukua tahadhari!.

Nawatakia Furahi Day Njema.
Paskali
Mkuu hiyo 50:50 inapatikana baada ya mwwkezaji kuondoa gharama zake za uzalishaji ,mfano kama imeptikana shilingi za kitanzani kama tzs 100, mwekezajia anatoa gharama zake amaboza si chini ya asilimia 60 ya hela iliyoptaikana (cost share) iliyobaki ambayo itakiwa ni Tzs 40 ndio wanagawana nusu kwa nusu(profit share),kwa hiyo serikali inapata Tzs 20 na mwekezaji anapata Tzs 20 ,kiuhalisia mwekezaji anabaki na Tzs 80 kati ya mia na serikali inapata Tzs 20 kati ya mia.
 
Theory na uhalisia ni vitu viwili tofauti.
Biashara ya madini na uendeshaji wake inahitaji uhalisia hasa na watu wenye kuujua huo uhalisia.
Kwa bahati mbaya wasomi wetu wengi mpaka level ya uprofesa wengi wamekariri sana pasipo kujua uhalisia wa mambo mengi kwenye dunia ya kisasa ya kibiashara.

Dunia ya sasa inaamini kwenye kujifunza, kutenda na matokeo na sisi tunaamini kwenye kukariri,kuhisi na kuongea.

Dunia ya sasa haihitaji siasa kwenye uendeshaji wa mambo hasa yale yenye maslahi mapana na chanya kwa taifa, tunashindwa na tutashindwa maana akili zetu bado zinawaza siasa na kutawala na si Tanzania na maendeleo yake.
 
Back
Top Bottom