Je wajua kuna epa ya majumba na viwanja huko masaki na osterybay?

mwana2009

New Member
Aug 10, 2008
4
4
Katika kile kinachoitwa epa watu wengi sana haswa watanzania wanajisahau na kuendelea kushinikiza tu hela za epa zirudi zirudi wakati kuna vitu vingi sana hawa vigogo wa serikali wamevifanya ambavyo bado ni mali ya wananchi na wananchi wenyewe ndio serikali .Kumbuka hapo miaka ya nyuma kama themanini hadi tisini hapo hakukua na nyumba binafsi kati ya maeneo ya masaki hadi osterybay zile nyumba nyingi zilitumiwa na wazungu ambao walikuwa wanalipa kodi pamoja na watanzania wenye vyeo vya juu selikarini yaani wakubwa.Cha ajabu na kushangaza sasa hivi zile nyumba wameuziana wenyewe vigogo na sio nyumba za serikali tena na cha ajabu zile nyumba zina viwanja vikubwa karibu heka au nusu heka kila kiwanja ila sasa hivi wakubwa wamegawana vile viwanja kwa bei nafuu sana na wengine kupeana bule kabisa na mimi nna mfano mmoja hapa kuna nyumba moja kule osterbay karibu na ronise pub kwenye round about kuna mzee mmoja pale alikukwa serikalini ameuziwa nyumba hivyo sh milioni 15 tu na sasa hivi amestaafu na ile nyumba amemkodisha fisadi mwenzie mhindi kwajina anaitwa JITU PATEL naye anahusika kwenye hii issue ya epa,hapo kwenye hiyo nyumha imevunjwa na patajengwa apatments za kutosha mule nda baada ya muda huyo fisadi JITU PATEL akimaliza kuvuna chake atairudisha nyumba kwa mwenyewe au atambidi alipe kodi upya sasa hapo ni makubaliano yao wenyewe.
Ila kikubwa zaidi ni kwamba sisi watanzania tunaomba nyumba za serikali zirudishwe ni nguvu ya wananchi .tunaomba zile nyumba na viwanja vya kule masaki na osterbay vikakaguliwe na virudishwe kwenye mikono ya serikali kwanini wauziane wenyewe tu kimya kimya yaani wamepeana kama serikali iliamua viuzwe kwanini wasitangaze kwenye redio.
tunaomba mlifanyie kazi hilo swala.
WADAU NASKIA UCHUNGU SANA TAFADHALI TUONGANE WOTE KWENYE MADA HIII.

NAOMBA MAONI YENU.
 
Nchi hii wanaimaliza wajanja. Mara utasikia majumba, migodi, viwanda, viwanja vimetupwa kwa bei ya kutupwa na serikali bado inatoa ruzuku kwa makampuni hayo binafsi kwa gharama za kuviendesha kama ilivyo kwa Kampuni ya Reli na Mgodi wa Minjingu. Wana JF tusichoke!
________________________
Ten people who speak make more noise than ten thousand who are silent. Napoleon -
 
Back
Top Bottom