Je, wajua kumsikiliza mtoto wako ni silaha muhimu ya kumkinga dhidi ya ukatili na udhalilishaji?

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Kumsikiliza mtoto kunaaminika kuwa ndio ngao muhimu zaidi ya kumlinda mtoto. Wataalamu wa malezi wanatuambia kuwa mtoto anayesikilizwa huwa jasiri na muwazi kwa mzazi au mlezi kwa yote anayoyapitia yawe mema au mabaya kwani wanaamini kuwa watachukua hatua kwa ajili yao.

Mara nyingi mtoto asiyesikilizwa, pindi anapopitia changamoto ya kufanyiwa udhalilishaji au ukatili wa aina yoyote, hukosa mahali pa kueleza ili apatiwe msaada kwani huhisi kutokuaminika kabisa hali inayompa maumivu ya kudumu na kuendelea kuwa mtumwa wa udhalilishaji huo.

Ndugu mzazi/mlezi hakikisha unamsikiliza mwanao kila mara, weka mazingira ya yeye kukuamini na wewe kumuamini ili awe salama wakati wote.

Sema Tanzania
 
Aisee kuna wazazi ni changamoto.

Wanaamini kuwasikiliza,watoto ni kuwalea kimayai.

Asante kwa uzi wako. Natumai wazazi tutajirekebisha katika hili.
Labda kumsikiliza Wanamaanisha kumpa kila kitu anacho kitaka ,Akita simu basi umpe hata kama unaingea nayo ,akitaka kungalia katuni mumpe remote anytime anayotaka
 
Akina mama muda mwingi tunakaa na kuangalia watoto...wababa sasa?????
Kina Mama pamoja na kushinda na watoto muda mrefu ila huwa mnakuwa na uangalizi mdogo wakati mwingine.

kuna makosa yapo ambayo ukiyasikilize ni wazi mtoto anafanya na wewe unamtazama.

muda huu naandika hapa mwanangu kameza hela ya sarafu na mama yake alikuwa akimuona anachezea halafu baadae anaanza kukuambia kameza shilingi ngapi. sasa huu kama si uzembe ni nini pamoja na kuwa mko na watoto lakini mazingira hatarishi wala hamyaoni kwa urahisi.

Sent from my M2006C3LI using JamiiForums mobile app
 
Sasa hiyo hela imepita kwenye koo? Au mmeshamtoa hiyo sarafu
 
Back
Top Bottom