Je, wajua kuhusu sera na sheria ya afya ya akili

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,007
9,873
JE WAJUA KUHUSU SERA NA SHERIA YA AFYA YA AKILI?


Sera ya afya inasema Afya ya akili ni sehemu muhimu ya huduma za afya ya jamii. Magonjwa na ulemavu wa akili vimekuwa vikiongezeka katika jamii kutokana na mabadiliko ya hali ya maisha. Huduma za afya ya akili nchini ni duni, kutokana na kutopewa umuhimu wake na upungufu wa wataalam wa magonjwa ya akili.

Sheria ya magonjwa ya akili ya mwaka 2008 imetafsiri kuwa magonjwa yatakayoainishwa na shirika la afya duniani(WHO) kuwa ni magonjwa ya akili na nchi itayaona magonjwa husika kama ni magonjwa ya akili.

WHO limetaja Sonona ‘depression’, Bipolar disorder, Schizophrenia (Uchizi), Dementia na Usonji ‘autism’ kuwa ni baadhi ya magonjwa ya akili. Magonjwa haya hasa sonona humfanya mtu kujitoa uhai kwa kuwa mtu huyachukia maisha.

Na sheria ya afya ya akili imetaka watu wenye magonjwa hayo kupelekwa kwa wataalamu wa afya ili kupatiwa matibabu. Sheria ilitaka kuanzishwa kwa National Health for mental health, na sera ilitaka uwepo wa bodi itakayoshughulikia afya ya akili.

Katika hali ya kustaajabisha Januari 2020, Kamanda wa Polisi mkoani Tabora, Barnabas Mwakalukwa alisema wangeanza msako kuwabaini wanaotaka kujinyonga na kisha kuwapeleka Mahakamani.

Kitu ambacho si sahihi kisheria kwa kuwa kwenye sheria ya afya ya akili imemtaka mtu yoyote polisi akiwemo kusaidia kuwabaini wagonjwa wa akili na kuripoti kwa Mental health facility na sio mahakamani
 
Mada umeianza vizuri mwishoni ukaweka lawama. Cha muhimu hapa ni kuelimishana je nchi yetu ina mpango gani wa matibabu kwa watu hawa maana kiukweli gharama kuzimudu ni kubwa mno.Watu wenye matatizo haya ni wengi na wengine huwezi wagundua ni watu wa maana (influencials) matajiri,wenye vyeo vikubwa na masikini wakiwepo.Watu wengi wanafikiri mtu mwenye ugonjwa wa akili ni yule mchafu mchafu watu wengine ni ma professors.

Google neno John Nash utaona professor huyu alipata nobel price mara mbili.Naandika hili nikiwa na ushahidi mimi mwenyewe mtoto wangu ana schizophrenia na anasoma chuo kikuu. Usimlaumu huyu afande ni kutokujua au huwezi jua naye ana tatizo gani.

Cha kujiuliza hapa je kuna chama cha magonjwa ya afya ya akili?Ningefurahi mhe waziri wa afya dada yetu mchapakazi asome uzi huu.

Ahsante kwa uliyeuanzisha


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu zangu huu uzi nmefurahia sana na na natamani hili liweze fika mbali sana sbb watu wengi wanna mental issues sema hawatambui ,sbb mm mwnyw hapa npo nafanya mpango niweze onana na psychiatrist kwan ninahofu pengine nikawa Nina OCD ,ivyo jaman huu uzi uweze kufika mbali jaman hadi kwa uyo waziri wa afya ataye teuliwa cjui ndio Ummy Mwalimu
 
Back
Top Bottom