Je wajua kuhusu Madhara ya ahadi za wagombea kwenye uchaguzi 2010?

Shadow

JF-Expert Member
May 19, 2008
2,897
671
Tunapoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu-2010; haya maneno ya Justice Scalia yanamaana kubwa sana kwa wapiga kura wote:
"[C]ampaign promises are—by long democratic tradition—the least binding form of human commitment...." Justice Scalia on Republican Party v. White, 536 U.S. 765 (2002) (majority opinion
 
Kwa hiyo tusiwabane viongozi wetu kwa yale waliyotuahidi??

Mkuu Babuyao, ni kujaribu kuonyesha kwamba hizo ahadi zimekaa kimkao wa makubaliano ya kiungwana zaidi 'Gengtleman Agmt' na hazina nguvu yoyote ya kisheria kama zisipotekelezwa. Tuamke na kujifunza katika hili.
 
Mkuu Babuyao, ni kujaribu kuonyesha kwamba hizo ahadi zimekaa kimkao wa makubaliano ya kiungwana zaidi 'Gengtleman Agmt' na hazina nguvu yoyote ya kisheria kama zisipotekelezwa. Tuamke na kujifunza katika hili.
Hapana mkuu, sikubaliani naye. Ahadi ni aina ya mkataba; ndo maana waswahili wakaiweka kiulaini kuwa "ahadi ni deni". Kisheria kuna kanuni inasema: contacts must be respected. Huwezi ukaweka mkataba (ahadi) halafu ukasema mkataba huo siyo binding. Unajidanganya. Mkataba lazima ukuwajibishe, ukusukume utende, na usipotenda unakuwa na makosa kwani unakuwa umeuvunja. Na hapo ndipo lilipo kosa la wanasiasa wetu. Wanapoahidi jambo wanajiweka pingu, na wanaposhindwa kutekeleza lazima tuwaajibishe. Hivo ahadi zina nguvu ya kisheria, na lazima ziheshimiwe na kutimizwa.
 
Back
Top Bottom