JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 625
- 938
Back up ni hatua muhimu ya #UlinziWaData kwani humsaidia mhusika kutunza taarifa zake muhimu ili hata akipoteza kifaa chake au kikiharibika aweze kuzipata tena
Kuna majukwaa mengi yanayotoa huduma ya Backup kwa uchache ni Google Drive, One Drive, Team Drive, iCloud, SugarSync, MyPCBackup n.k
Aidha ya data ambazo zinaweza kuwekwa au kufanyiwa Backup: Nyaraka laini, picha, video, na sauti. Unaweza kufanya backup kwa kutumia simu yako au kompyuta yako
Hata hivyo umakini unahitajika sana wakati wa kuchagua sehemu ya kuhifadhi taarifa zako, hakikisha mtoa huduma hiyo anazingatia ufaragha wa taarifa zako
#UlinziWaData
JINSI YA KUFANYA BACK UP KWENYE GOOGLE DRIVE KWA WATUMIAJI WA SIMU ZA ANDROID
JINSI YA KUFANYA BACK UP KWENYE GOOGLE DRIVE KWA WATUMIAJI WA SIMU ZA ANDROID
Kwa watumiaji wa simu za mfumo wa Android wengi wao wanatumia Email na huduma za Google hivyo wao wanaweza kuhifadhi data zao katika Google Drive
Unaweza kufanya back up ya taarifa zako kwa kufuata hatua zifuatazo: Kama simu yako haina Application ya Google Drive basi unapaswa kuipakua (Download) kwanza
Kama tayari una application hiyo ifungue kisha nenda sehemu yenye alama ya kujumlisha au tafuta sehemu imendikwa Pakia Faili au Upload File bofya sehemu hiyo
Simu yako itakutaka uchague faili, data au nyaraka unayotaka kuifanyia back up, chagua taarifa husika kama ni picha, video, namba za simu au nyaraka
Baada ya kufuata hatua hizo simu yako itaanza kuhifadhi taarifa hizo kwenye Google Drive kwa ajili ya kutunzwa
KUMBUKA: Kazi hii huitaji simu yako iwe ina kifurushi cha Internet au iwe imeunganishwa na huduma ya Internet kwa njia nyingine kama vile Wi-Fi
Aidha, unaweza kuchagua na kuiruhusu simu yake iwe inafanya backup kila inapounganishwa na huduma ya Wi-Fi