Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,000
- 9,862
Kazi hii inapatikana nchini Japan kutokana umati unaokwenda kazini nyakati za asubuhi kwa kutumia usafiri wa treni. Japan ni taifa linalochapa kazi, na huhakikisha kila mtu anafika kazini kwa wakati unaotakiwa.
Kutokana na wingi wa watu, Japan imewaajiri watu wenye taaluma ya kuwasukuma watu ndani ya treni wakati kuna msongamano ili pasiwe na mtu hata mmoja wa kuchelewa kazini.
Wasukumaji hawa wakati mwingine hulazimika kuwasukuma ndani ya treni wasafiri ambao huchelewa kupanda treni au wakati wanapositasita kupanda kwa madai kwamba treni imejaa.
Wanaotaka kazi hii wanatakiwa kuvaa sare nyeupe na glovu nyeupe na watatakiwa kufanya kazi hiyo kati ya saa moja na saa tatu asubuhi, kisha saa moja jioni hadi saa tatu usiku.
Kazi hiyo huchukuliwa kama kama kazi ya ziada na mara nyingi hufanywa na wanafunzi na mshahara haufahamiki.
Bongo tunaweza kuajiri watu kusukuma watu daladala za Mbagala, Gongolamboto na Kimara