Je, wajua haramu isipoharimishwa inageuka halali? Na batili isipobatilishwa inageuka halali. Je, tuhalalishe ubatili huu kwa mhimili wetu wa Bunge?

3. Japo Spika Mhe. JYN tayari ameisha jiuzulu uspika, kujiuzulu huko, japo ni kujiuzulu batilifu, lakini kujiuzulu ni kujiuzulu na Spika amejiuzulu, lakini kwa kuheshimu katiba, lazima ubatili katika barua hizo uondolewe kwa kuandikwa barua rasmi kwa mujibu wa katiba.
4. Bunge lipokee kimya kimya barua mpya ya kujiuzulu kwa Spika iliyoandikwa kwa mujibu wa katiba, kisha Bunge ndio litoe copy kwa CCM.
Hitimisho.
Namalizia kwa lile swali la msingi la uzi huu
Je wajua, haramu Isipoharimishwa Inageuka halali?, na batili Isipobatilishwa inageuka halali!. Je, Tanzania, tuhalalishe ubatili huu wa kujiuzulu kinyume cha katiba kwa mkuu wa mhimili wetu wa Bunge? Kama katiba imeelekeza jinsi ya kufanyika kwa jambo fulani, kuna sababu gani ya msingi ya kutofuata katiba na badala yake tukumbatie ubatili?

Jumatatu Njema.
Pascal
Habari njema kwa watu wote, pendekezo No. 3 na No. 4 Katika bandiko hili, limetekelezwa kwa asilimia 100% kama lililopendekezwa.
Hivyo sasa ule ubatilifu katika barua ya Kujiuzulu kwa JYN umeondolewa kama nilivyo shauri, na kuwasilishwa barua halali,
Hivyo ile taarifa ya JYN kwa waandishi wa habari, kuwa ameandika barua kwa Katibu Mkuu CCM, sasa imebatilishwa na imefutwa kwenye website ya Bunge, barua rasmi ni kwa Katibu wa Bunge, na CCM kupewa nakala.
Hongera sana Bunge letu tukufu kuubatilisha ubatili huu. Sasa kwenye hili la Spika umebaki ubatili mmoja wa Naibu Spika, Dr. Tulia Akson kujiuzulu u Naibu Spika, kabla ya kugombea Uspika.
P
 
Back
Top Bottom