Je, wajua chama cha mapinduzi ( ccm ) kilipata usajili wa muda na kudumu siku moja? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, wajua chama cha mapinduzi ( ccm ) kilipata usajili wa muda na kudumu siku moja?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kitomai, Mar 17, 2010.

 1. Kitomai

  Kitomai JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,036
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA NDANI YA ULIMWENGU WA ULIMWENGU TBC 1.


  Jana tarehe 16/march/2010, Msajili wa vyama vya siasa alikuwa mgeni mwalikwa katika kipindi cha ulimwengu wa ulimwengu kinachotayarishwa na Jenerali Ulimwengu na kurushwa na kituo cha runinga cha TBC 1. Kawaida kipindi hicho urushwa hewani kila Jumanne saa 1 jioni.

  Moja ya swali aliloulizwa Mheshimiwa John Tendwa linahusiana na muda ambao Msajili anapaswa kutoa cheti cha kudumu baada ya kutoa cheti cha muda. Kwa maelezo ya mheshiwa John Tendwa cheti cha kudumu hakitoweza kutolewa chini ya miezi sita hata kama chama kitakuwa kimekamilisha taratibu zote ndani ya mwezi mmoja. Hiyo ndiyo tafsiri ya sheria aliyoitoa msajili wa vyama vya siasa.

  Kwa tafsiri hiyo chama kama CCJ ni dhahiri kuwa hakitoweza kupata usajili wa kudumu ndani ya miezi sita ijayo. Hivyo hakitoweza kushiriki uchaguzi mkuu ujao kama mpango huo ulikuwepo. Huo ndio ukweli halisi kwa mujibu wa tafsiri iliyotolewa na msajili wa vyama vya siasa.

  Binafsi mimi nadhani suala la namna msajili anavyopatikana na mamlaka aliyonayo ni jambo ambalo linatakiwa kufikishwa Mahakamani kwa kufanyiwa uamuzi.

  Kwa nini nasema hivyo? Binafsi kwa uelewa wangu sheria inayomsimika msajili wa vyama vya siasa inakiuka sheria za asili; pili, haina uwezo wakuzuia madaraka yasitumiwe vibaya kuwakandamiza wananchi, na tatu, ni pana mno kiasi cha kuweza kuwabana hata wale ambao hawajakusudiwa kubanwa na hiyo sheria hiyo.

  Msajili wa vyama vya siasa anapatikana vipi? Kutokana na anavyopatikana ni dhahiri kabisa huyu ni mtu awezaye kutiliewa shaka katika maamuzi yake

  Msajili wa vyama vya siasa anateuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano chini ya kifungu cha 4(1) cha sheria ya vyama vya siasa 5/1992.
  Rais wa sasa ni Mwenyekiti wa chama cha C.C.M Upo hapo? Kwa nini wenyeviti wa vyama vingine hawashirikishwi katika uteuzi wa huyo Msajili?

  Chama Cha Mapinduzi kilipata usajili wa muda na wa kudumu siku moja tu. Mheshimiwa Tendwa unalijua hilo? Mimi binafsi sijapata muda wa kuchangia hapo TBC 1. Kama haya maneno ninayoyasema ni ya uongo kanusha katika kipindi kijacho, ambacho kitarushwa Jumanne ijayo ya tarehe 23/march/2010. Cha ajabu nini CCJ kupata usajili wa kudumu ndani ya mwezi mmoja, ikiwa CCM ilipata usajili wa muda na kudumu siku moja?

  Msajili wa siasa anafanya kazi kwa kushirikiana kwa kushirikiana na Waziri wa Sheria ambaye vilevile anachaguliwa na Rais. Kwa mazingira hayo Msajili wa Vyama wa Bwana John Tendwa na mtangulizi wake Bwana Liundi ni watu ambao wanaotiliwa shka sana katika utendaji wao wa kazi.

  Msajili ana madaraka makubwa-na ana uwezo wa kukataa kukiandikisha chama, ana uwezo wakukifuta chama cha siasa, anaingilia mambo ya fedha ya vyama, walijua hilo?

  Uamuzi wa msajili ni uamuzi unaoweza kukosolewa kuwa ni uamuzi batili kwani ni uamuzi wa mtu anayetiliwa mashaka. Msingi wa kuwa muammuzi yeyote asiwe mtu anayetiliwa shaka kama mtu anayeweza kutoa uamuzi wa upendeleo ni moja ya haki za asili ambazo tumezipokea kutoka Uingereza chini ya kifungu cha 2 cha sheria Judicature and Application of Laws Act No. 51/1961(Sura ya 453).

  Mahakama zetu zimefafanua lini uamuzi utakuwa batili kwa ajili ya uamuzi kutiliwa shaka. Mahakama zimesema suala siyo kuwa uwezekano wa uamuzi kupendelea upande fulani ni mkubwa sana bali ni kuwa mtu kawaida anaweza kumtilia shaka huyo muamuzi angalau shaka kidogo.

  Kwa hiyo suala sio kuwa Msajili ni mtu kwa kiasi kikubwa anaonekana atapendelea upande fulani, bali suala ni kuwa je mtu wa kawaida anaweza kumtilia shaka juu ya uamuzi wake?

  Hivyo ndivyo ilivyoamuliwa na Mahakama ya Rufaa ya Tanzania katika kesi ya Zabroni Pangamaleza Vrs Joakim Kiwaraka: Civil Appeal No.33/1987. katika kesi hiyo hakimu aling’ang’ania kusikiliza kesi wakati mmoja wa wadaawa alimkataa asisikilize kesi hiyo. Jaji Mfalila alisema hukumu hiyo ilikuwa batili, kwani kitu muhimu sio kuwa tu haki inatendeka bali haki ionekane kutendeka wazi kwa mtu wa kawaida. Na akasema kuwa suala sio kulikuwa na uwezekano wa mkubwa wa hakimu huyo kupendelea upande fulani, bali suala ni kuwa je mtu wa kawaida (kama yule mdai aliyemkataa hakimu) angeweza kumtilia shaka hakimu angalau shaka kidogo tu juu ya uamuzi wake? Kesi zingine za Tanzania zinazosisitiza suala hilo ni Mbuji Vrs R.:(1971) H.C.D. n. 200; R.Vrs Abdallah Msumi: (1973) L.R.T. n.45; Michael Marogwa Leonard Vrs R.:133. Kuna kesi zingine za nchi za nje zinazosisitiza sual hilo kuwa muamuzi asiwe mtu wa kutiliwa shaka nazi ni:
  Metropolitani Properties Co.Ltd. Vrs. –Lennon:(196 3 All E.R. 304 (Uingereza); Livesey Vrs. New Southern Wales Bar Association:(1985) L.R.C (Const.)580 (Trinidad and Tobago); Law Society of Lesotho Vrs. The Prime Minister: (1986) L.R.C. (Const)508(Dominica).

  Utaratibu huo wa kumkataza muamuzi anayetiliwa shaka asishiriki kutoa uamuzi, hauhusu mahakimu pekee bali unahusu hata waamuzi wowote wa vyombo vingine vya dola vingine-tazama hukumu ya Uingereza ya Allinson Vrs. General Council of Medical Education and Registration:(1891-4)All E.R. Rep. 768.

  Hoja hiyo ya kuwa uamuzi wowote wa Msajili wa vyama vya siasa hauwezi kubatilika kisheria inaungwa mkono na Mhariri wa Sheria Professa Issa G. Shivji katika mada yake ambayo aliitoa kwenye Semina ya Chama cha Tanganyika Law Society hapo tarehe 22-23 April 1992 Dar es Salaam juu ya ‘’Fiasco at Law:Comments on Bills for the 8th Constitutional Amendment Act 1992 and the Political Parties Act 1992’’ na mada hiyo imo katika Ripot ya chama hicho cha wanasheria iitwayo’’ Democracy and the Rule of Law during and After Mageuzi’’ ukrasa wa 10.


  Swali la Msingi ambalo Bwana John Tendwa anatakiwa kilijibu kwa ufasaha. kwa nini CCM iliweza kupata usajili wa muda na wa kudumu siku moja ili hali vyama vingine vinapitishwa katika mchakato mgumu wa kisheria?
   
Loading...