Je waijua nguvu kubwa na hatari toka CCM iliyokabiliwa na Wabunge wa CDM Mwanza? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je waijua nguvu kubwa na hatari toka CCM iliyokabiliwa na Wabunge wa CDM Mwanza?

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Idimulwa, Apr 2, 2012.

 1. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2012
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  1.Mgombea wa udiwani Kirumba kupitia CCM Bwana Jackson Robert ni mfanyabiashara maarufu sana na sifa za umafia pia swahiba mkubwa wa Ridhiwani Kikwete,Lawrance Masha na DCI Kanumba.

  2.Bwana Kitana ni mfanyabiashara maarufu,tajiri na mafia pia.

  3.Lameck Airo ni mfanyabiashara maarufu Mwanza na ni Mbunge wa Rorya kupitia CCM.

  4.Mwita Gachuma ni mfanyabiashara maarufu na mjumbe wa NEC.

  Hii ndiyo ilikuwa timu ya ushindi ya CCM kwa kushirikiana na uongozi wa CCM mkoa na ndiyo maana pesa ilitumika sana inasadikika kiasi cha zaidi ya MILION 80 zilitumika kuhonga,kununua shahada za kupigia kura na kila aina ya rafu ili ushindi upatikane.

  Lakini wabunge wa CDM Wenje,Kiwia na Machemuli,Madiwani,BAVICHA na viongozi wengine waliweza kuwaunganisha wana Kirumba huku wakiwasisitiza kuchukua pesa za CCM na kuwaomba wazitumie kumchangia mgombea wa CDM na hilo lilifanikiwa kwani si chini ya shilingi laki 3 zilikuwa zikichangwa papo kwa papo katika kila mkutano wa kampeni.

  CDM walifanikiwa kuwaingiza kasa CCM katika zoezi lao chafu la ununuzi wa kadi za kupigia hali ambayo ilikuja kuwavuruga sana siku kama 1 kabla ya uchaguzi baada ya kugundua kuwa asilimia kubwa sana ya shahada walizonunua ni za wafuasi wao wenyewe(CCM) na ikawa kazi kuwatafuta wawarudishie.

  Hii ndiyo hali ilivyokuwa Kirumba pamoja na CDM kuibuka kidedea.Shughuli ilikuwa pevu na ndiyo maana habari ya wabunge kukatwa mapanga inaweza isimshangaze mtu.
   
Loading...