Je, wahafidhina ndani ya CCM, wameafiki Kwa shingo upande, maamuzi ya Rais Samia kuruhusu mikutano ya kisiasa, Kwa vyama vyote?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,480
30,152
Nimeisikiliza Kwa makini Sana hotuba ya Rais Samia Suluhu Hassan, aliyoitoa Leo, huko Ikulu, wakati anaongea na viongozi wa vyama vya siasa nchini.

Kwa kweli Sina budi kumpongeza Rais wetu Samia Suluhu Hassan, Kwa msimamo wake Kwa kueleza kuwa kama Taifa, inabidi tujenge mshikamano, umoja na utulivu na vyama vyote vya kisiasa, kwani ndiyo nguzo kuu ya kutuletea maendeleo endelevu ya kudumu.

Alieleza zaidi kuwa hatuwezi kuujenga umoja huo kama tutaendelea kutowafanyia haki Kwa kutowatendea haki vyama vya upinzani, Kwa kuendelea kuwanyima haki yao ya kikatiba ya kuitisha mikutano ya hadhara ya kisiasa.

Jambo moja ninalojiuliza, ni Kwa vipi mtangulizi wake Hayati Magufuli, aliamua kuzivunja Sheria za nchi, ambazo zinaruhusu mikutano hiyo ya hadhara kwenye nchi hii ya mfumo wa vyama vingi vya kisiasa?😎

Alieleza kuwa wajibu wa Jeshi la Polisi ni kuilinda mikutano hiyo Ili ifanyike Kwa amani na wala siyo kuipiga marufuku isifanyike.

Rais aliendelea kueleza kuwa wao kama watawala, wangependa Sana kukosolewa, kwani ni Kwa njia hito inayoweza kuwafanya wajirekebishe na kuwatendea mambo mazuri watanzania, Kwa lengo la kuwapatia maendeleo.

Lakini ingawa uamuzi huo ameutoa kama Rais na wakati huo huo kama Mwenyekiti wa chama chake Cha CCM, ninaamini kabisa kuwa ndani ya chama chake Kuna wahafidhina wachache ambao Bado wanaunga mkono maamuzi ya Hayati Magufuli ya kuipiga marufuku mikutano hiyo hawatapenda maamuzi hayo na wangependa kuendeleza malumbano na kutotenda haki dhidi ya vyama vya upinzani

Kwani wahafidhina hao wanaamini kuwa Kwa kuruhusu mikutano hiyo ya hadhara Kwa vyama vya siasa, maovu yao yatawekwa hadharani na hivyo kuzifanya nafasi zao za kiutendaji Serikalini ziwe katika hati hati😃
 
Na Kuna wabunge waliyatelekeza majimbo yao wakakimbilia Dar kwa kujua hakuna mpinzani atakayekuja jimboni
Hongera Mama,na Rais wetu kwa kuruhusu mikutano ya vyama vingi.
Kingine cha muhimu tuletee na katiba mpya.!
IMG_20221114_112805.jpg


Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Kwani hao ndio waliozuia?
Crimea
Kwani hujamsikia mhafidhina Makamba, akitamba ndani ya Mkutano Mkuu wa CCM uliopita, akiwaponda Sana wapinzani na kuwaambia kuwa Katiba mpya, siyo hitaji la watanzania?😎

Kwa maelezo ya Mzee Makamba, eti mtanzania yeye anahitaji kupata mlo wake tuu!
 
Hii kitu maridhiano ni upumbavu mtupu, kwanza wanaridhiana kuhusu nini??? Hapa ilichotakiwa kupewa kipa umbele ni katiba mpya basi, maana haya yanayoitwa maridhiano mpaka 2025 watakua bado wanajadiliana tu na matokeo yake ni haya;

Winner = CCM aka Chama Cha Mambuzi
Loser = Upinzani ie CDM.
wapinzani wangeingia 2025 bila huu utumbo wa maridhiano matokeo yangekua haya:
Winner = CDM
Loser = CCM ila ndio hivyo wapinzani wamedanganyika wamauvaa mkenge...kwisha habari yao maana hio kuruhusu mikutano wamepangiwa na cha kuongea la sivyo mkong'oto utawapata toka kwa chawa wa Hangaya, na hao chawa ni Polisi na ma TISS..

Mangi sijui kapotea wapi hadi kapigwa changa la macho namna hii.
 
Hii kitu maridhiano ni upumbavu mtupu, kwanza wanaridhiana kuhusu nini??? Hapa ilichotakiwa kupewa kipa umbele ni katiba mpya basi...
hebu punguza jazba dadangu... inamana unawaona upinzani hawana akili wewe ndo unaakili etiee,,,
 
Back
Top Bottom