Je wahadhiri hawa wa ustawi kudai haki zao ni kosa mpaka wafukuzwe kazi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je wahadhiri hawa wa ustawi kudai haki zao ni kosa mpaka wafukuzwe kazi?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by kionambal, Aug 21, 2011.

 1. k

  kionambal Member

  #1
  Aug 21, 2011
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  NDUGU ZANGU, NIMEPOKEA TAARIFA HIZI ZA HUZUNI KUTOKA KWENYE VYOMBO MBALIMBALI VYA HABARI KUHUSU KUWASITISHA KAZI WAHADHIRI HAO. LAKINI NINACHOJIULIZA WAHADHIRI SASA NI WENDAWAZIMU WA KUDAI MAMBO YASIYO NA TIJA KWA TAIFA? MIMI NADHANI PALE CHUONI KUNA MAMBO NYETI YANAFICHIKA, NILIWAHI KUSIKIA KWAMBA KUNA MAMA MMOJA

  <STRONG>MKURUGENZI WA FEDHA NA UTAWALA (DFA) </STRONG>YEYE NDIYE CHANZO CHA MIGOGORO YA CHUO HICHO MUHIMU AFRIKA MASHARIKI NA KATI, KAMA NI YEYE KWELI KWA NINI SERIKALI HAICHUKUI HATUA AU HUYO MAMA ANA HISA NA CHO AU AMETUMWA? WASOMI WENZANGU, TULIFUATILIE JAMBO HILI. NADHANI WAHADHIRI WALIKUWA NA MABO MUHIMU YA KUIAMBIA SERIKALI NA JAMII YA WATANZANIA KUHUSU CHUO CHAO NA SI KUONGEZA MISHAHARA AU KUTHIBITISHWA KAZI YAPO MENGINE YANAYOHUSU ITHIBATI AMBAYO NI UTI WA MGOGNGO WA CHUO CHOCHOTE. SAA BASI NI WAKATI HUU AMBAO RAISI KIKWETE AUNDE TUME HURU KUCHUNGUZA UKWELI WA CHUO HICHO NA KURUDISHWA KWA WAHADHIRI HAO KAZINI. HVI NDUGU ZANGU KAMA WASOMI WANADAI MAMBO YA MSINGI WANADAI HAKI ZAO NA ZA NCHI KWA UJUMLA WANAFUKUZWA KAZI JE SISI NGUMBALU SI TUTAISHIA JELA? NIMESKITIKA SANA KWA SABABU NIMESIKIA MAMBO MABAYA SANA YA UONGOZI WA CHUO HICHO, VIONGOZI HAO NI WASHIRIKINA, WAMEJAWA NA CHUKI.

  MFANO, <STRONG>ANDREW MCHOMVU</STRONG> AMBAYE TUMEKUWA TUKIMUONA KWENYE TELEVISION AKIDADAVUA MADA ZA KIJAMII KUMBE NA YEYE ANAHITAJI COUNSELING. WAZIRI MKUU NA RAISI KIKWETE NAWAPA TAARIFA KUNA MTANDAO MKUBWA KUANZIA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII, BODI YA MAGAVANA YA CHUO CHA USTAWI WA JAMII PAMOJA NA MENEJIMENT NDIYO CHANZO CHA MIGOGORO PALE CHUONI. JAMANI FUNGUENI MAONI YENU TUELIMISHE UMMA WA WATANZANIA, NA KUANZIA SASA TUSIPELEKE WADOGO ZETU KILE CHUO SASA NI VETA YA MIGOGORO.

  POLENI SANA WAHADHIRI ENDELEENI KUPIGANIA HAKI ZA JAMIII YA WATANZANIA.
   
 2. b

  brianjames11 Member

  #2
  Aug 29, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hilo swala nimeliona kwenye vyombo vya habari pia. Ila kama bodi ya chuo inaweza kufukuza wahadhiri wote hao kwa mara moja inawezekana kuna tatizo mahali. kama ni uongozi wa chuo bado hayo matatizo yataendelea, kwa kuwa bado uongozi ulikuwepo unaendelea na kazi. Lakini kwa wahadhiri wenye sifa za kutosha kufukuzwa kazi sio issue kabisa, kwa kuwa kuna uhaba mkubwa wa wahadhiri sehemu nyingi Africa na hata nchi zilizoendelea. Kama walikuwa active na kufanya utafiti itarahisisha wao kupata ajira haraka sana. Lakini pia nina mashaka na sifa zao kitaalama, maana kwa mhadhiri mwenye sifa sitahili chuo kikimfukuza kinapata hasara kwa kupoteza asset. Siku zote chuo kinakuwa kizuri kama kina wahadhiri wenye sifa (i.e. PhD holders) na ambao wanafanya research. Ni vema bodi ikalifikiria vizuri swala hilo kama wamefukuza wahadhiri wanaojitosheleza kufanya kazi hiyo. Itakuwa ni hasara kubwa sana kwa chuo hicho, na faida kwa vyuo vingine ambavyo vitawachukua hao kiurahisi.
   
 3. MWAKIGOBE

  MWAKIGOBE Member

  #3
  Aug 30, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 65
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kama tatizo ni uongozi basi kilasiku wataendelea kuwafukuza wahadhiri, kwani hata hao wapya hawajashuka kutoka nbinguni.
   
Loading...