Je, wafungwa watapewa nafasi ya kutoa maoni yao? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, wafungwa watapewa nafasi ya kutoa maoni yao?

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Kaa la Moto, Jun 18, 2012.

 1. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Monday, 18 June 2012 13:42
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  Phinias Bashaya
  MWANANCHI aliyefungwa jela, kifungo hakimuondolei haki ya kuwa Mtanzania. Wananchi ni msingi wa mamlaka na wafungwa wana haki ya kutoa maoni ya uundwaji wa katiba mpya.

  Tume ya Jaji Warioba itafanya kosa la kihistoria ikipuuza maoni ya wafungwa. Sauti za kundi hili ni muhimu katika mijadara ya usawa mbele ya sheria na misingi ya utoaji haki.
  Wafungwa ni ndugu jamaa na rafiki zetu ambao baada ya kutumikia adhabu hujumuika na jamii kuendelea na maisha nje ya kuta za gereza.
  Katika kipindi hiki mbele ya tume ya Jaji Warioba kundi hili linahitaji uhuru wa wafungwa ili watoe maoni yatakayoweka msingi wa taifa lao kwa miongo ijayo.
  Ripoti ya tume ya Jaji Warioba kuhusu tatizo la rushwa nchini iliyoteuliwa Januari 17, 1996 inajenga hoja ya umuhimu wa kuangalia hali inayowakabili wafungwa.
  Hoja ya tume hiyo kuwa dola na mahakama ni sehemu ya tatizo baada ya baadhi ya maofisa kubainika kushiriki vitendo vya rushwa inaongeza ukweli kuwa wapo wafungwa walioko magerezani kwa sababu iliyotajwa na tume.
  Kwa msingi huo wapo wananchi wanaotumikia vifungo vya wengine kwa sababu tu ya umaskini wao. Sehemu ya ripoti hiyo inasema polisi hupokea rushwa, kuwakamata watu na kuwatungia makosa ya uongo.
  Polisi mwenye ujasiri wa kutunga makosa ya uongo kama mtego wa kupewa rushwa hashindwi kukusanya ushahidi wa kutunga.Kwa kuwa msingi wa hukumu ni ushahidi watuhumiwa wengi wa aina hii huishia jela.
  Tume ya kukusanya maoni ya uundwaji wa Katiba haitakuwa na haki ya kujisifu kuwa imekusanya maoni ya Watanzania bila kufika gereza la Segerea, Bukoba na penginepo.
  Ukusanyaji wa maoni usiwabague walioko kifungoni,baadhi wangekuwa huru kama wangepata mawakili wa kuwatetea na kukata rufaa kama wafanyavyo wenye fedha.
  Wengi wameshinda rufaa baada ya kutiwa hatiani kwa kilichotajwa ni makosa katika hukumu za awali. Ismail Rage ni miongoni mwao. Leo ni Mbunge wa Tabora Mjini na kiongozi mahili wa timu ya Simba.
  Kutoa maoni juu ya uundwaji wa katiba mpya ndio wajibu na haki muhimu anayostahili kupewa kila mwananchi bila kujali kama yuko gerezani au uraiani.
  Tume ya Warioba kukwepa kufika magerezani ni kuwanyima pia fursa maelfu ya mahabusu wasiojua hatima ya kesi zao kutokana na mfumo unaochelewesha utoaji haki.
  Walioko ndani ya magereza ndio wenye ushuhuda halisi kama kweli utoaji haki katika Jamhuri ya Muungano unatenda haki kwa wote bila ya kujali hali ya mtu kijamii au kiuchumi.
  Katiba ya sasa inasema kila mtu anao uhuru wa kuwa na maoni na kueleza fikra zake.Haiyabagua makundi mengine kwa sababu zozote zile.Wote tuko huru kwa mawazo na imani ya kuabudu.
  Tume ya Jaji Warioba isikwepe kufika magerezani kwani kazi yake ni kukusanya maoni ya wananchi na hailazimiki kujibu maswali ya wafungwa na mahabusu.
  Ni ndani ya kuta za gereza pekee ambapo tume inaweza kusoma hisia za wafungwa wanaotaka uundaji wa katiba uwape haki ya kuwa wapiga kura.

  Maoni ya wadau
  Kifungo ni njia ya kumrekebisha mtu aliyetiwa hatiani na wala hakifungi uwezo wake wa kufikiri na kutoa mchango wa mawazo.

  Rais wa Shirika la (Peoples Organisation Transparency Agency) POTA Idrisa Massalu anasema katiba inatungwa kwa ajili ya wananchi na haoni sababu ya wafungwa kutengwa katika utoaji wa maoni.
  Anataka tume itumie busara ya kusikiliza maoni ya makundi yote na wafungwa wapewe fursa hiyo bila kuzungumzia kesi zao.

  Anapendekeza ipitie baadhi ya magereza na kupata maoni kwa kuzingatia huko pia kuna wataalamu wenye maoni tofauti kuelekea uundwaji wa katiba mpya.
  Kabla ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010,Msajili wa vyama vya siasa nchini John Tendwa 30, Septemba alinukuliwa na gazeti la Mwananchi akizungumzia umuhimu wa wafungwa kupewa haki ya kupiga kura.
  Alisema kuwa wana haki ya kuchagua viongozi kama walivyo wananchi wengine na kutoa mifano ya nchi za Afrika Kusini, Botswana na Lesotho ambazo wafungwa hupiga kura.
  Alisema katika nchi hizo wasioruhusiwa kupiga kura ni wale waliohukumiwa vifo na vifungo vya maisha utaratibu unaweza kutumika pia hapa nchini.
  Kwamba tume ‘ikigoma’ kwenda magerezani itakuwa imepuuzia maoni ya msajili wa vyama vya siasa na wote walioko nyuma yake wakililia haki za wafungwa.
  Katiba inatamka 5(1)kila raia aliyetimiza umri wa miaka 18 ana haki ya kupiga kura katika uchaguzi unaofanywa na wananchi.
  Ibara ndogo ya(2) inasema Bunge linaweza kutunga sheria kuzuia raia asipige kura kwa kutiwa hatiani kwa makosa fulani ya jinai.
  Bunge halijawahi kutunga sheria ya kuzuia haki ya wafungwa kupiga kura na sio wote walioko magerezani wametiwa hatiani kwa makosa ya jinai.
  Wapo wasiojiweza wanaotaka kusikika kupitia tume ya Jaji Warioba.Ripoti ya Kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC)ya mwaka 2010 inaonyesha kuwa magereza yote nchini yana uwezo wa kuhifadhi wafungwa 27,653 na kuna ziada ya wafungwa 10,490.

  Mkasa wa Victoria
  Victoria Jasson(49)ni mwanamke aliyetupwa jela mara mbili katika gereza lile lile kabla ya kuokolewa na msamaha wa rais Kikwete Desemba,2008.

  Alitumikia kifungo cha miezi nane na baadaye mwaka mmoja na nusu katika gereza la Kayanga wilayani Karagwe.Mpaka leo anaamini alifungwa kwa sababu ya jeuri ya fedha.
  Jeuri ya fedha ya mume wake ambaye anadai baada ya kuoa mwanamke mwingine ulitokea mgogoro mkubwa wa kifamilia.Hatimaye alijikuta anakabiliwa na mashitaka ya kula njama na unyang’anyi wa kutumia silaha.
  Aliunganishwa na vijana wengine sita ambao baadaye walimkana mahakamani kuwa hawamfahamu,huku akiwa tayari amekaa gerezani miezi nane.
  Anakumbuka kukatishwa masomo akiwa na umri wa miaka 14.Walivyoishi na mme wake na kupata mabinti watatu wa kike na wavulana sita ambao wote wamesambaratika baada ya mgogoro wa wazazi.
  Mara ya pili alijikuta anatumikia kifungo cha mwaka mmoja na nusu jela baada ya kulazimisha kurudi kijijini kuhudhuria sherehe ya arusi ya mwanawe aliyekuwa anafunga ndoa.
  Ana mengi ya kusimulia kuhusu mateso aliyopata akiwa ndani na nje ya gereza. Sasa anatafuta msaada wa kutunga kitabu, kwani simulizi yake inajaza kurasa zote za gazeti hili.
  Anataka aeleze maisha yake baada ya kujitambua,safari ya kuelekea gerezani, hapa alipo na matarajio yake anapoelekea uzeeni.
  Kwamba baada ya kupelekwa jela mabinti wake walikimbilia Bukoba Mjini na kulazimika kuishi maisha ya kujilea.Baada ya kifugo aliwakuta wakiwa na wajukuu.
  Watoto walitumbukia katika mfumo wa maisha uliotokana na makosa ya wazazi na kwa hakika baada ya kifungo cha mama yao
  Tume itupe katiba itakayoweka msingi imara na mwongozo makini wa haki za binadamu. Haki ya wafungwa kutoa maoni na kupiga kura.


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  Source Mwananchi:18 June 2012
   
Loading...