Je wafanyakazi wenzako wanakutembelea nyumbani?

mimi sitaki wajue kwangu,bado nafaidi ujana,Mungu akipenda labda nikioa ndo waje.
 
Ha ha ha, basi mie wananing'ang'aniza waje kwangu
Nawapigaje chenga
ongeza chenga tu,wakija wengine ni umbea tupu...ooh,mshahara wote ananunulia simu,kumbe kapanga,,,,ngoja nikuchekeshe,kuna jamaa alienda nyumbani kwa boss wake,na huyo boss ni mnene vibaya mno,kufika msalani wakakuta kamba....guess ilikuwa ni ya nini.........mzee akikata gogo hawezi kunyanyuka,mpaka aji-support na kamba...hiyo stori imesambaa ofisini kwao mpaka ikanikuta mimi...full vituko,usiwaalike.
 
Nimegundua wafanyakazi wengi wa Dsm na miji mingine mikubwa hawana utamaduni wa kupelekana majumbani.
Vikao mara nyingi huishia kwenye nyamachoma.
Je kwanini hali hii?
Mimi hapa ofisini kwangu nimejaribu sana kuwakaribisha wenzangu nyumbani kwangu, lakini wamegoma katakata kunitembea.
Hili lipo sana! Tunaogopana sijui!...lakini mtu atauliza tunaogopa nini?

Anyway, mimi binafsi napenda marafiki wa kazini na masuala ya kazini yaishie huko huko na ya nyumbani kwangu yabakie nyumbani kwangu (private). Labda marafiki wa karibu sana (normally, one or two!) ndio tunaweza kushare masuala private ikiwemo la kualikana majumbani!
 
Bujibuji nafikiria tatizo lingine ni kuwa hapa Dar watu hawana muda wa kutosha. Pia foleni huchangia kwa kiasi kikubwa kuwatia watu uvivu wa kutembeleana. Imagine wewe unaishi Kawe na rafiki yako yuko Gongo la mboto, ukiamua kumtembelea utaiweza hiyo foleni? Si utakuwa umemaliza siku nzima njiani?

Binafsi naona fuleni za magari zimechangia sana kuharibu utamaduni wetu mzuri wa kutembeleana kwa nia njema ....
 
Last edited by a moderator:
Ni vizuri kualikana nyumbani; inaleta umoja na sense ya trust pia. Chakula cha jioni mara moja kwa mwezi sio mbaya hata kama kila mtu aje na drink yake!

Namiss sana good old days tulipokuwa porini no TV no Simu; you only have yourselves to entertain each other. Lkn siku hizi ni marafiki wa mtandaoni ndio wamereplace real companies!
 
Bujibuji nafikiria tatizo lingine ni kuwa hapa Dar watu hawana muda wa kutosha. Pia foleni huchangia kwa kiasi kikubwa kuwatia watu uvivu wa kutembeleana. Imagine wewe unaishi Kawe na rafiki yako yuko Gongo la mboto, ukiamua kumtembelea utaiweza hiyo foleni? Si utakuwa umemaliza siku nzima njiani?

Binafsi naona fuleni za magari zimechangia sana kuharibu utamaduni wetu mzuri wa kutembeleana kwa nia njema ....

hapo umeua SOO 2je J2 sikuku ????
 
Last edited by a moderator:
tatizo lako unajitahidi kukaribisha wakike zaidi!!na kumbuka wanajua huna mke nani atatia mguu kwako asiyejipenda!!!
 
Mi nadhani mkipanga ratiba vizuri inawezekana kutembeleana.
Bujibuji nafikiria tatizo lingine ni kuwa hapa Dar watu hawana muda wa kutosha. Pia foleni huchangia kwa kiasi kikubwa kuwatia watu uvivu wa kutembeleana. Imagine wewe unaishi Kawe na rafiki yako yuko Gongo la mboto, ukiamua kumtembelea utaiweza hiyo foleni? Si utakuwa umemaliza siku nzima njiani?

Binafsi naona fuleni za magari zimechangia sana kuharibu utamaduni wetu mzuri wa kutembeleana kwa nia njema ....
 
bujibuji yawezekana unawakaribisha kwa pembeni unawapiga vijembe ndo maana wanakataaa
 
hahaha, umenikumbusha munene mmoja wa msd alikuwa anatuambia kuna jamaa ofisini kwao kafiwa na mtoto. siku wanaenda msibani wakadhani wamepotea. accounts clerk ana jumba la maana kuliko la mkurugenzi:majani7:
 
Nimegundua wafanyakazi wengi wa Dsm na miji mingine mikubwa hawana utamaduni wa kupelekana majumbani.
Vikao mara nyingi huishia kwenye nyamachoma.
Je kwanini hali hii?
Mimi hapa ofisini kwangu nimejaribu sana kuwakaribisha wenzangu nyumbani kwangu, lakini wamegoma katakata kunitembea.

Ukitaka watu wakutembelee kwako anza kwanza wewe kwenda majumbani kwao then some watapata moyo kuja kwako kama unawish wakutembelee!!!!!!!!!!!!!!
 
Bujibuji nafikiria tatizo lingine ni kuwa hapa Dar watu hawana muda wa kutosha. Pia foleni huchangia kwa kiasi kikubwa kuwatia watu uvivu wa kutembeleana. Imagine wewe unaishi Kawe na rafiki yako yuko Gongo la mboto, ukiamua kumtembelea utaiweza hiyo foleni? Si utakuwa umemaliza siku nzima njiani?

Binafsi naona fuleni za magari zimechangia sana kuharibu utamaduni wetu mzuri wa kutembeleana kwa nia njema ....

hapo umeua SOO 2je J2 sikuku ????

Karibuni sana, ila msimsahau charminglady naye pia namwalika na ningependa kumuona, Kaizer naomba usilalamikie mwaliko huu, lol!
 
Last edited by a moderator:
Mi nadhani mkipanga ratiba vizuri inawezekana kutembeleana.

Itawezekana sana, ila ni mara chache sana kutokana na nature ya mji wenyewe ulivyo. Ila ni jambo jema kukaa na marafiki kama familia na kubadilishana mawazo.
 
ila kuna watu naturally hawataki wageni, hata ndugu zao wanawafukuza wakitoka kijijini unaulizwa umekuja kufanya nini? utaondoka lini? kama majibu hayaridhishi kesho asubuhi na mapema unajikuta umeamkia ubungo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom