Je wafanyakazi wenzako wanakutembelea nyumbani?

Mmmh jamani hata mimi mazoea ya kuja nyumbani siyataki. Labda mara moja kwa mwaka sio mbaya au ninakafunction nitawaalika lakini sio zaidi ya hapo, kama itatokea mmojawapo ndio mwenzangu kazini na my best pal I might think.
 
Hahahaa wengi hawapendi kujuana kuana hasa kwa wanawake. Hupenda kwenda kuangalia flan anaishije, ana nini na vitu kama hivyo. Mimi binafsi sipendi kwenda kwa mtu pasi na shughuli muhimu. Mf. Sherehe au tatizo. Mwisho wa siku utajaambiwa umemtangaza analalia mkeka. Marafiki unafiki tu hasa urafiki wa wanawake
 
Afu hapo hapo

Watu wanaanza investigation, ni noumer watu kuja kwako aisee
wengine wanaenda kugoogle bei za magaei waliyokuta yamepark hapo nje. Mara auditors, ukikaa sawa unahamishiwa tandahimba ukaanzishe kitengo. Kila mtu akae kwake, ajiju. Na vikao vya msiba siku hizi vinafanyikia break point, kuaga maiti kanisani ama hospitali. Bhaaaassss!
 
mimi niliwakaribisha kufika waliyoona mansion wakapagawa,wakaanza kuja kunitega,mara nimekuja kukufanyia usafi,mara mimi niko single ni balah tupu
 
Kuna jamaa yangu bosi wa nssf alikuwa ana tabia ya kupeleka vimwana kwake kumbe wale vimwana wanakusanya data tu wakamwanika juzi imetoka barua kwenda tarime nusu apate kiharusi wakati alishazoea ac ya benjamin mkapa house
 
BUJIBUJI umenikuna haswaaa! Asante sana kwa uzi huu, yaani hamuwezi amini kuna mfanyakaz mwenzetu mmoja yaani yeye hataki watu wajue kwake, akipata matatizo mf: msiba wa karibu, au anaumwa, yaani kama ni msiba wa kusafirisha, akirud tu kesho yake yupo kazini, ukimwambia tunakuja kukupa pole utasikia Nipeni hapahapa tu. Hakuna hata mfanyakaz m1 anajua kwake, 2naishia kujua anaish Mbez Makonde. Akiumwa sasa, "tunakuja kukuona" utasikia nipo hsp ntatoka sa10 kesho yake huyo kazini. Unaendeleaje? Ah! Mi nshapona. Wakat unaona bado kalegea. Last week J2 kapata msiba wa kaka yake hukooo upareni, kaenda kuzika, karudi Alhamis last wk, Ijumaa huyu kazini!! Mmh! Juzi j5 2kamwambia 2nakuja ijumaa kukupa pole ya msiba kaitikia sawa karibuni, jana kaja kazini kawaida, leo sasa! He he! He! Anapigiwa simu atuelekeze kwake watu ndo 2shapewa ruhusa na Boss tukampe pole mwenzetu, kwani anapokea? Badae anatuma msg Nipo hsp Muimbili nimemleta mtoto ntarud sa 10! Yametushukaje?? Na Vizigo vyetu! Si mnajua tena mambo ya Vikanga na Visukari? Yaani watu wazima na akili zetu 2kaachwa Solemba!
huyo ameshawapa msg kuwa hataki mtu nyumbani kwake,ila bado mnamng'ang'ania.kuna wengine wakienda kwa watu huchunguza mengi hasa wanawake,wanachokiona wanaenda kuhadithia.au kuna wengine huwa uongo mwingi.ukienda kwao ni tofauti kwa wanayoyaelezea.kuna dada mmoja alikuwa na tabia ya kujisifia kuwa kanunua hiki na kile.na alikuwa na tabia ya kusema nyumba za watu.siku akafiwa,duu,watu walioenda kwao,walishangaa,yote aliyokuwa anasema kanunua ni uongo mtupu.
 
mimi kwanhu sitaki mtu aje,na mimi siendi kwa mtu labda kuwe na jambo maalum.wanaokuja kwangu ni ndugu zangu tu.wengine tutaishia huko huko nje.huyo ndugu yangu mmoja namuheshimu,maana akija,mmh,hebu badilisha hiki,au mpaka leo hichi unacho.ni full maneno tuu.ila manuheshimu tu
 
Ni vizuri kualikana nyumbani; inaleta umoja na sense ya trust pia. Chakula cha jioni mara moja kwa mwezi sio mbaya hata kama kila mtu aje na drink yake!

Namiss sana good old days tulipokuwa porini no TV no Simu; you only have yourselves to entertain each other. Lkn siku hizi ni marafiki wa mtandaoni ndio wamereplace real companies!

unayosema dada ni mazuri lakini binadamu wa leo mawivu na roho mbaya ole wako aje kwako akute unamaendeleo kuliko unachopata kazini utajuta unaweza kurushiwa hata mawe (Kufanyiwa mambo ya ajabu kama yapo). kuna rafiki yangu alikuwa anakaribisha wafanyakazi wenzake wanachinja mbuzi kwa furaha na drinks kidogo alifanya hivyo kwa muda wa mwaka moja mwaka uliofuata alifukuzwa kazi kiaina aina vile.. haya mambo yana uzuri wake na ubaya wake inategemea ninani anaupendo wa dhati na kufurahia mafanikio yako kama yapo
 
huyo ameshawapa msg kuwa hataki mtu nyumbani kwake,ila bado mnamng'ang'ania.kuna wengine wakienda kwa watu huchunguza mengi hasa wanawake,wanachokiona wanaenda kuhadithia.au kuna wengine huwa uongo mwingi.ukienda kwao ni tofauti kwa wanayoyaelezea.kuna dada mmoja alikuwa na tabia ya kujisifia kuwa kanunua hiki na kile.na alikuwa na tabia ya kusema nyumba za watu.siku akafiwa,duu,watu walioenda kwao,walishangaa,yote aliyokuwa anasema kanunua ni uongo mtupu.

asilimia kubwa ya wasiopenda kutembelewa majumbani kwao ni watu wa kujisifia mambo ya uongo na hivyo huogopa kuumbuka
 
du unanikumbusha mwalimu wangu moja pale UDSM aliwahi tualika darasa zima tulikuwa19 nyumbani kwake kwa dinner mara 2 alikuwa na mke mzungu and real we enjoyed the dinner.
 
kwako pazuri bana ndio maana wakaribisha!!wengine wanajifanyaga matawi ya juu huko job kumbe anapoishi ni kama pangoni
 
sihitaji.... marafiki oooh no no no- Fid Q
FID Q ALIKUWA ANAMUIMBA ADILI CHAPA KAZI BAADA YA KUFULIA.
ADILI-4.jpg
 
Wengi tunaishi maisha ya kuigiza. Nyumbani kwangu hapalingani na status yangu kitaan, bar ofcn nk! So wengi tunaogopa kualikana!
 
Nimegundua wafanyakazi wengi wa Dsm na miji mingine mikubwa hawana utamaduni wa kupelekana majumbani.
Vikao mara nyingi huishia kwenye nyamachoma.
Je kwanini hali hii?
Mimi hapa ofisini kwangu nimejaribu sana kuwakaribisha wenzangu nyumbani kwangu, lakini wamegoma katakata kunitembea.


Bujibuji leo ni Jumatatu na huu ni muda wa kazi. Je, umelewa wakati una post huu uchizi au ulitaka tu kuchekesha watu? Kingine, yule demu Natalia anaye confuse watu kwa kuandika yasiyoeleweka unayeje?
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom