Mzalendo_Mkweli
JF-Expert Member
- Jan 30, 2012
- 1,988
- 1,175
Leo nilijaribu kujipa kazi ya kufuatilia maendeleo ya timu za Afrika ambazo wachezaji wetu wa kulipwa wanazichezea huko. Wachezaji ambao nimefuatia timu zao ni Himid mao Mkami (Petrojet-Misiri), Thomas Ulimwengu (JS Saoura-Algeria), Simon Msuva (Difaa el jadida- Morocco) na Abdi Banda (Baroka fc- Afrika Kusini). Katika Tathmini yangu nimegundua kwamba mchezaji pekee ambaye timu yake itashiriki mashindano ya vikombe vya Afrika mwakani ni Thomas Ulimwengu wa JS Saoura ya Algeria ambayo katika Ligi ya huko inashika/Itashika nafasi ya nne.
Nilipojaribu kufuatilia mchango wa wachezaji (wanavyopangwa) wa Tanzania katika timu zao, nimekutana na changamoto kidogo ya kupata taarifa sahihi sana hasa kwa timu za mataita ya kiarabu (Morocco, Algeria na Misri) ambao mifumo ya kutoa hali za michezo katika mitandao (Status) hawatoi Line-up (wachezaji waliopangwa) ila nimeona Substitutions tu (wachezaji wa akiba) hivyo kushindwa kupata hitimisho kama wachezaji Thomas Ulimwengu, Himid mao Mkami, Simon Msuva wanapangwa mara kwa mara katika vilabu vyao au la. Nilipojeukia kwa Abdi Banda ambaye anachezea huko afrika ya kusini huko nimepata taarifa zote za wachezaji yaani vikosi vya kwanza na wachezaji wa akiba kwa kila mechi. Nilipofuatilia takwini za kiuchezaji za Abdi Banda nimegundua kwamba ni zaidi ya miezi mitatu/minne Abdi Banda hajawepo katika Kikosi cha kwanza au cha akiba cha Baroka fc. Natambua kwamba Baroka fc katika miezi kama sita iliyopita wamekuwa katika vita kubwa ya kuepuka kushuka daraja katika ligi yao, lakini Je mchezaji ambaye hakuweza kumvutia kocha hata mara moja kuwa katika kikosi cha akiba kwa zaidi ya miezi minne atakuwa na "Fitness" ya kutosha kuichezea timu yetu ya taifa Taifa? Je mchezaji akishasajiliwa tu timu ya nje ya Tanzania kunampa ticket ya moja kwa moja ya kuitwa timu ya Taifa.
Nimetoa mawazo yangu kama mfuatiliaji tu wa mambo ya mpira wa miguu na sio mtaalamu wa mpira wa miguu.
Wataalamu na wafuatiliaji wenzangu wa mpira wa miguu mnakaribishwa kutoa maoni yenu.
Nawakilisha