Je, Wabunge wa CCM ni mashujaa au wanafiki na "opportunists" ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, Wabunge wa CCM ni mashujaa au wanafiki na "opportunists" ?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mag3, Mar 21, 2009.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Mar 21, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Je, tangu mwaka 2005 hadi leo kuna rekodi yoyote ya mbunge kutoka CCM kutofautiana na wenzake wakati wa upigaji kura bungeni. Kama sijakosea nafikiri kwenye kambi ya upinzani tumeshuhudia wakitofautiana kwenye mitizamo hadi kufikia upigaji kura.

  Licha ya majadiliano makali ya awali kabla ya upigaji wa kura, wabunge wote wa CCM kwa pamoja ama wameishia kuunga mkono hoja kama imetoka serikalini au kupinga hoja kama imetolewa na Upinzani. Je hali hii inaashiria nini kama si uwoga na unafiki ?

  Je kuwaita baadhi ya hawa Wabunge mashujaa ndani ya CCM ni sawa ?
   
 2. mwakatojofu

  mwakatojofu JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2009
  Joined: Dec 17, 2008
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hapa ushujaa utakuwa umepimwa kwa kigezo kimoja. hivyo ndivyo ushujaa unavyopimwa?

  utamaduni wa kutounga mkono hoja jamaa wa ccm ni kama hawana. utakuta maneno mengi na pointi tupu kuonyesha mambo kutokwenda sawa halafu mwishoni mheshimiwa mbunge anasema anaunga mkono hoja kwa asilimia 100. eh! hapo kuna unafiki na uoga

  kama hawawez kutoa shiling ni bora wasiwe wanaanika hizo weaknesses. wawe wanasema mazur matupu na mwishon wakiunga mkono hoja kwa 100% tutawaelewa
   
 3. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #3
  Mar 21, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Wabunge wa ccm wote ni wanafiki na wazandiki kwa kuwa wote waliingia bungeni kwa rushwa na hakuna hata mmoja ambaye hakuhonga wapiga kura; hapo hapo ndio maana sishangai wanaposema kuwa Zitto amelembishwa faranga na Rostam kwa vile wao wamezoea kuhongwa hawaamini kuwa mtu anaweza kuwa na msimamo tofauti na matarajio akiongozwa na conscience yake na si fedha!! Hao hao wanawatuhumu wabunge wenzao kuwa wamehongwa ndio hao hao mimi binafsi nilishuhudia wakipokea hongo toka kwa mbunge mwenzao aliyekuwa anacampaign ili mumewe achaguliwe kuwa mbunge wa bunge la Afrika Mashariki; leo hii wao wamesahau kuwa huwa wanapokea mshiko, ama kweli NYANI HAONI KUNDULE!!
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  Mar 21, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,533
  Trophy Points: 280
  Siasa za Tanzania ni siasa za vyama na sio siasa za watu. Wabunge wote wanaingia bungeni kwa tiketi za vyama, hivyo kwanza unakuwa mtiifu kwa chama ndipo kwa nafsi yako na waliokuchagua.
  Mjadala ukipamba sana moto, wabunge wa CCM hukaaa kama kamati ya chama. Hapo hutoka na kauli moja ya collective resiponsibilities hata kama kwa nafsi yako hukubaliani na msimamo wa chama.
  Wapo wabunge mashujaa ambao nia zao kuutaka ubunge ni kuwatumikia wananchi. Pia wako wange waganga njaa waliutafuta ubunge ili wapate ulaji ama waule kwenye uwaziri, hawa ndio wale wanaousaka ubunge kwa gharama yoyote.
   
 5. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #5
  Mar 21, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  wabunge wa ccm ni wanafiki that is the only adjective befitting their stutus
   
 6. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #6
  Mar 21, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Mwakatojofu, tatizo langu ni pale wengine kati yao wanapodai kuwa wasafi na wenzao kuwa wachafu lakini mwisho wa siku wanakaa na Paulo. Sasa, utawezaje kumwona mwenzako fisadi asubuhi halafu jioni mnatumbua pamoja. Huko nje mitaani na kwenye ma "press conference" unatoa tuhuma nzito dhidi ya wenzako lakini kwenye vikao rasmi unanywea kama umenyeshewa mvua, sasa tukueleweje ?

  Wapo na wengine leo atanguruma kama radi na atajizolea sifa kama shujaa na mpiganaji, halafu asisikike tena mpaka hapo maslahi ya chama yatakapo tishiwa. Wabunge wa CCM wengi unaweza kuwafananisha na "toothless bulldogs" ambao kishindo cha kubweka kwao ni dalili ya kukosa meno ya kung'ata. Nasononeka kila ninapoliona neno shujaa likitumika kwa hawa waoga na wanafiki.

  Utakaaje meza moja ukala na Paulo mwenye mikono michafu ?​
   
 7. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #7
  Mar 22, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  Kwa nature ya siasa za Bongo zilivyo, wabunge wote wa CCM ni maopportunists!! Haiwezekani siku zote wawe wanafikiri sawa. Tatizo lililopo ni maslahi, watu wazima hawana hata independent thinking, nikiwa na maana hakuna mbunge anayeenda kuwasilisha kero za wananchi kama zilivyo isipokuwa kutetea maslahi ya chama, huku akitetea kuchaguliwa tena. Nadhani ule utaratibu wa majina ya wagombea ubunge kupitiwa na kamati kuu ya CCM ndio unaowatia woga wa kukosa siku nyingine wakiwa wa kweli. Utaona kuwa wale wote waliodiriki kutoa madukuduku yao wameishia kujengewa visa kula kukicha. Nimeshangaa kuona hata madaktari na maprofesa wakiingia katika siasa zetu wanabaki na vichwa vya kuazima. Hakuna ukweli kwamba mtu anagombea ubunge kupitia CCM kwa ajili ya maendeleo ya wananchi, bali yake binafsi.!!
   
 8. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #8
  Mar 22, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Hakuna mbunge hata mmoja kwenye bunge la Jamhuri anayestahili kuitwa shujaa wote ni wagaganga njaa; wangekuwa mashujaa saa hizi wangekuwa wanapigania kuwa na katiba mpya kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa!! They are not even agitating for the participation of independent candidates [ inspite of the favourable ruling of the apellate court] kitu ambacho kingewapa uhuru wabunge wa ccm ambao watapigwa kalamu na chama chao kwenye preferential votes!!!! There is no way the opposition can beat CCM if they will go to the polls with this constitution as it is!!
   
  Last edited: Mar 22, 2009
 9. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #9
  Mar 22, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Swali zuri sana linaloibushwa na swali hili ni kwamba, je, wananchi wa Tanzania wanaowachagua hawa wabunge wana access ya voting records za wabunge hawa? Na kama ipo inapatikana vipi?

  Zaidi ya hapo tutakuwa hatujibu swali kwa facts, ila tunatumia instincts tu.
   
 10. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #10
  Mar 22, 2009
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - "Huwezi kupanda mahindi ukavuna mihogo", na "you cannot be wrong and get it right".

  William.
   
 11. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #11
  Mar 24, 2009
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Good abservation.

  William.
   
 12. M

  Mkandara Verified User

  #12
  Mar 24, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mag3,
  Mkuu kabla hujawatazama wabunge wa CCM nadhani ipo haja ya kuwatazama wananchi wenyewe wanaowachagua hawa Wabunge.. Ikiwa wewe unafahamu mtu fulani ni mnafiki kwa miaka 40 iliyopita bado leo chaguo lako la kwanza ni CCM... hapa mnafiki nani?..
  Mimi nadhani wabunge wachache walioko CCM kwa mtindo waliokuja nao leo ni mwanzo mzuri kwetu wananchi na Upinzani...
  Kwa mara ya kwanza tunaona wabunge wa CCM wakipinga hadharani miswada ambayo haina tija kwetu hata kama wanashindwa ktk kura au kujenga hoja..hata kama ni wachafu at least wanatafuta maji kuoga au kusafisha hilo shimo..
  Binafsi sikubaliani na msemo uliotoka sasa hivi kuwa hawa watu wanaishi dampo..Kwa sababu tunaotazama haya sisi wenyewe tumekalia maji machafu vilevile pamoja na kwamba sii ya taka..Wao kwa Ufisadi wao na sisi kwa Ulimbukeni wetu...Ni sawa na Mkenya anayetucheka Tanzania wakati yeye mwenyewe hana usafi huo..
  Ni Wabunge wachache sana toka Upinzani walioleta mageuzi ya kweli pia na hakika Dr. Slaa ni mmoja kati ya wachache hao, lakini siwezi kumhukumu kwa sababu tu naye yupo bungeni.. Bunge ambalo mimi binafsi naliona kama shimo linaloonekana safi lakini limejaa virusi vya maradhi makubwa ya Ufisadi..
  Hivyo, sioni tofauti ya Mwakyembe, Mama Kilango, Zitto na Dr. Slaa ikiwa swala hapa ni WABUNGE... huwezi kutenganisha CCM -A + CCM -B bungeni bila kuweka Upinzani A + Upinzani B kwani wote hawa ndio wanaolifanya Bunge kuwa lilivyo leo hii -USANIII...
   
 13. v

  vincent New Member

  #13
  Mar 25, 2009
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu,
  Nijibu swali letu juu ya hawa wabunge wetu wala si chochote. Wameshaanza ubabaishaji wa kuanza kuhonga watu ilwa wachaguliwe tene. Ni miezi 18 iliyobakia utasikia wameanza ubabaishaji wao. Oh! nitewafanyia hiki na kuwaletera kile. Wemeanza kutuzungukia wakinadi kula yao. Wengi wao ni wababaishaji tu na wanafiki tu. Huwasikii hata neno lolote wanaliongelea wakiwa bungeni. Wenginie wanadiriki hata kukimbia vikao kama wayoyo wa shule kwenda kurandaranda mjini. Dodoma imekuwa shpping centre yao.
  Tinao wachache wawe wa upinzani au wa chama tawala ni mashujaa. Hatuwezi kuwasahau. Lakini hawana wa kuwaunga mkono kwani namba ya wanafiki ni kubwa kuliko mashujaa. Ebu fikiria kuna mbunge gani ameweza hata kuongelea uuaji wa albino na vikongwe. Si ajabu hata baadhi yao utasikia wanatembea na mifupa ya albino kusudi wachaguliwe mwaka 2010
   
Loading...