Mwanamayu
JF-Expert Member
- May 7, 2010
- 11,347
- 6,471
Mara nyingi wabunge wanawahidi wananchi kuwa watawapelekea maendeleo, je hiyo ndio kazi ya mbunge? Kwenye katiba ya URT ibara ya 63 na 64, kazi ya mbunge ni kushiriki kwenye kutunga sheria na kusimamia na kushauri serikali. Sasa haya mambo ya nitajenga barabara, nitawachimbia kisima ni ya kweli? Na wanaofanya hivyo kwa pesa zao sio rushwa hiyo? Wananchi tusome katiba!
Au watuambie watatunga sheria nzuri kwa kiwango kipi ili kuboresha maisha yetu? Watasimamia serikali na kuishauri ili kuleta ubora wa maisha? Tusipowasikia bungeni, hakuna ajira! Wakishabikia sheria mbovu, wakiwashabikia mafisadi, hakuna ajira!!!
Swali No.2 Kutoka kwa Kijakazi
Nina swali ambalo limekuwa likinitatiza siku nyingi sana hapa nchini nalo ni kuhusu kazi ya Mbunge, hivi kazi ya Mbunge hasa nini (kikatiba) jimboni kwake?
Nauliza hivyo kwa maana mara nyingi nimekuwa nasikia wananchi wengi wanamlalamikia Mbunge wao kwamba hajafanya kitu jimboni kwao kwamba hajajenga Barabara, au hajaleta Maji au sijui hajajenga Daraja, sasa kitu ambacho sielewi Mbunge yeye ana mamlaka gani ya kufanya hayo mambo niliyoyataja?
Kama swala la Miundo mbinu mtoaji na muamuaji Barabara au Maji yawekwe wapi si Serikali, sasa yeye Mbunge ana uwezo gani au mamlaka gani ya kujenga Barabara au daraja jimboni kwake mpaka kustahili kupata lawama zote hizo? naomba mwenye uelewa na haya mambo aweze kunielezea kazi hasa ya Mbunge (Kikatiba ) ni ipi?
MAJIBU KUTOKA KWA WANAJF
======
Au watuambie watatunga sheria nzuri kwa kiwango kipi ili kuboresha maisha yetu? Watasimamia serikali na kuishauri ili kuleta ubora wa maisha? Tusipowasikia bungeni, hakuna ajira! Wakishabikia sheria mbovu, wakiwashabikia mafisadi, hakuna ajira!!!
Swali No.2 Kutoka kwa Kijakazi
Nina swali ambalo limekuwa likinitatiza siku nyingi sana hapa nchini nalo ni kuhusu kazi ya Mbunge, hivi kazi ya Mbunge hasa nini (kikatiba) jimboni kwake?
Nauliza hivyo kwa maana mara nyingi nimekuwa nasikia wananchi wengi wanamlalamikia Mbunge wao kwamba hajafanya kitu jimboni kwao kwamba hajajenga Barabara, au hajaleta Maji au sijui hajajenga Daraja, sasa kitu ambacho sielewi Mbunge yeye ana mamlaka gani ya kufanya hayo mambo niliyoyataja?
Kama swala la Miundo mbinu mtoaji na muamuaji Barabara au Maji yawekwe wapi si Serikali, sasa yeye Mbunge ana uwezo gani au mamlaka gani ya kujenga Barabara au daraja jimboni kwake mpaka kustahili kupata lawama zote hizo? naomba mwenye uelewa na haya mambo aweze kunielezea kazi hasa ya Mbunge (Kikatiba ) ni ipi?
MAJIBU KUTOKA KWA WANAJF
Ndugu wanaJF,
Baada ya kusoma Katiba ya Jamahuri ya Muungano wa Tanzania kifungu cha 63 (hapo chini) chenye kuianisha madaraka ya wabunge nimekuwa nikijiuliza hii dhana ya watanzania kuwatarajia wabunge kuleta maendeleo katika jimbo moja moja k.m huduma za kijamii kama vile shule, zahanati, barabara, maji n.k chimbuko lake nini.
Ikiwa wananchi wataendelea kuwapima wabunge wao kwa viwango vya manedeleo katika majimbo binafsi badala ya uwezo wa kuisimamia na kuishauri serikali; kwa kuwa Rais na Mawaziri ni sehemu ya Serikali ambayo wabunge wanatakiwa kuisimamia kwa mujibu wa katiba; na ili kupata maendeleo binafsi jimboni wabunge hulazimika kuwapigia magoti mawaziri ambao kwa mujibu wa katiba hii wanapaswa kuwasimamia.
Hatuoni kwamba katika kila chaguzi watanzania hupoteza fursa ya kuingiza bungeni idadi kubwa ya wabunge wenye uwezo wa kuisimamia serikali na badala yake kuwaingiza bungeni makuadi wa ufisadi ambao hawana ujasiri wa kuwasimamia mawaziri, makatibu wakuu n.k;
Na kibaya zaidi kuwatoa bungeni wale walionyesha uwezo wa kuisimamia serikali lakini wakashindwa kuwapigia magoti mawaziri (wanaopaswa kusimamiwa) ili kupatiwa migao binafsi ya maendeleo jimboni?
Ikiwa watanzania wataendelea na dhana ya kuwatarajia wabunge kuleta maendeleo katika majimbo binafsi kama vile chenge alivyofanya bariadi, lowassa alivyofanya monduli n.k kwa kutumia fungu dogo kati ya mabilioni ya fedha zinazoibiwa serikalini kila mwaka kutokana na usimamizi hafifu wa bunge.
Hatuoni kwamba hali ndio husababisha usimamizi wa serikali kupwaya na kupelekea rais na mawaziri kutumia fedha za rasirimali za Tanzania watakavyo. Matokeo yake Tanzania imeendelea kubaki katika lindi la umaskini licha ya kupata uhuru mika 49 iliyopita ikilinganishwa na kiwango cha rasirimali kilichopo?.
Ni kwanini Watanzania wasiwaachie wabunge kazi ya kuisimamia serikali na wakasubiri maendeleo kwa mujibu wa mipango ya serikali kwa wananchi wote kwa uwiano sawa kwa majimbo yote badala ya utaratibu wa sasa ambapo baadhi ya mawaziri na watendaji wa serikali wanaruhusu kiasi kikubwa cha fedha na rasalimali za taifa kupotea ili waweze kupata kidogo cha kupeleka majimboni mwao kuwapoza wananchi wanaowachagu na kujilimbikizia ziada?
Je, katika hali hii vita dhidi ya ufisadi itafanikiwa kweli?
63.-(1) Rais kama sehemu moja ya Bunge atatekelezamadaraka yote aliyokabidhiwa na Katiba hii kwa ajili hiyo.
(2) Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu chaJamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwaniaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii.
(3) Kwa madhumuni ya utekelezaji wa madaraka yake Bunge laweza-
(a) kumuuliza Waziri yeyoyote swali lo lote kuhusu mambo ya umma katika Jamhuri ya Muungano ambayo yako katika wajibu wake;
(b) kujadili utekelezaji wa kila Wizara wakati wa Mkutano wa Bunge wa kila mwaka wa bajeti;
(c) kujadili na kuidhinisha mpango wowote wa muda mrefu au wa muda mfupi unaokusudiwa kutekelezwa katika Jamhuri ya Muungano, na kutunga sheria ya kusimamia utekelezaji wa mpango huo;
(d) kutunga sheria pale ambapo utekelezaji unahitaji kuwapo sheria;
(e) kujadili na kuridhia mikataba yote inayohusu Jamhuri ya Muungano na ambayo kwa masharti yake inahitaji kuridhiwa.
======
Wana jamvi naomba tuwekane sawa Nitapokuwa nimekosea nisahisheni juu ya h baadhi ya duku duku, maswali na maoni yangu.
Baadhi ya majibu ni kuwakilisha/ kutatua matazizo ya wananchi. Jibu hili lina zaa swali lingine
- Kwanza napenda nieleweshwe kazi hasa ya mbunge ni nini.?Je kazi za Mbunge wa magu zinatofautiana na zile za mbunge wa Sengerema.?Wajibu wa diwani unaanzia wapi na wajibu wa mbunge unaishia wapi.Je hakuna duplication ya vyeo. Ni katika level gani inakuwa ni kero ya kufanyiw akazi na diwani na katika level gani inakuwa ni kero ya kufanyiwa kazi na mbunge?
2. Je matatizo ya msingi ya wanachi wa jimbo la bunda yanatofautiana na matatizo ya msingi ya wanachi wa jimbo la Tarime?Binafsi naamini Tanzania tofauti na nchi zilizoendelea matatizo yetu ya msingi kwa sasa ni common. hatuhitaji wabunge wengi sababu matatiz ni yetu ni yale yale ELIMU, AFYA, MAJI, NISHATI, etc.Nadhani USA UK wanahitaji wabunge wengi sababu naamini matatizi ya msingi walishayatatua wamebaki kutatu area specific problem ndio maana kilo cha mbunge wa jimbo fulani la labda london inaweza isiwe tatio kwa mbunge wa jimbo fulani la Birmingham .
Nadhani kila wilaya ingekuwa na mbunge 1ja ingetosha na hizo na hizo hela ambazo wanalipwa wabunge zingeenda kwenye kutatua true poblem in local areas.
Naamini hii kasumba ya kuongeza majimbo ni ya kupumbaza wanachi wajione serikali imesogea karibu yao wakati huduma na mahitaji yya msingi ya wanachi bado inakuwa kero.
3. Je Ni halali kwa mbunge kusema akichaguliwa ataleta barabara ya rami au atajenga shule au ataleta umeme au visima vya maji? je ni kazi ya wabunge kufanya hivi? Najiuliza mbunge anakuwa ana maanisha nini kusema yeye ataleta barabara ina maana washindani wake hawawezi kuleta barabara?Ina maana atatumia Hela zake mfukoni?Hapa napata wasi wasi kuwa kuna aina ya watu wakiwa wabunge( eg profesors, Dk, friends to president family, etc) labda serikali inakuwa wepesi kutekeleza maombi yao na kuna aina ya watu wakiwa wabunge hata wakiongea kitu gani cha maana serikali inaziba masikio.
KAZI ZA WABUNGE HASA NI NINI?
4.Je wastani wa gharama za uchaguzi kwa kila jimbo ni shilingi ngapi? Kwani mbunge
akifariki. akitimuliwa chama kabla ya mhuhula kuisha nafasi isichukuliwe na yule aliekuwa
wa pili ?
Hoja yangu ni kuwa badala serikali kofocus na kutumia a mapensa mengi kwenye dhana ya demokrasia ya uteuzi na si ku focus zaidi kwenye dhana utekelezaji wa sera zake.
Last edited by a moderator: