Je Wa TZ Tutafika Safari Yetu????? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je Wa TZ Tutafika Safari Yetu?????

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nsololi, Aug 23, 2010.

 1. N

  Nsololi JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2010
  Joined: Mar 8, 2007
  Messages: 290
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45

  Bado safari ni ndefu na itaendelea kuwa ndefu hasa tukiendelea na chama kile kile kilicho na sera zile zile na desturi, tamaduni, mazoea na taratibu zilezile zilizotufikisha hapa tulipo kwa karibu miaka 50 ya uhuru tukiendelea kupigana pasipo mafanikio ya ushindi dhidi ya maadui wale wale wa ujinga, umaskini na maradhi n.k.

  Inasikitisha sana, Inauma sana.

  [​IMG]
  [​IMG]
   
 2. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mkuu nimefurahishwa na thread yako angalau ina mantik, kwani imeongelea chama zaidi kuliko mtu, kwani wengi humu huwa na lengu la kumponda JK tu as if wa TZ walikuwa wakiishi maisha ya zaidi ya dola moja kipindi cha Mkapa na watangulizi wake.
  Binafsi sioni tofauti ya kipindi cha Jk na wengine kwani maisha yangu na hata ndugu zangu huko vijijini ni yaleyale ya siku zote miaka nenda miaka rudi.
  Lakini pia inanisikitisha sana kwamba wengi wanajifanya ndo wanaona uozo wa CCM sasa wakati miaka yote ipo hivyo, na wengi humu humu JF wamekuwa wakiisapoti CCM sana tu miaka ya huko nyuma.
  Ukijumuisha yote haya ndo hapo ninapokuwa na wasiwasi juu ya huo upinzani sasa hivi unaoongelewa na baadhi ya watu na hasa kuhusishwa na Chadema. Naiona hatari ileeee mbele inakuja kwa ushabiki wa aina hii kwa sababu wengine hawatakubali kuwa maamuma miaka yote.
   
 3. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hatuwezi kufika mana VIONGOZ WETU WANAUMWA VIFAFA muda wao wate wanafikilia afya zao
   
 4. N

  Nsololi JF-Expert Member

  #4
  Aug 23, 2010
  Joined: Mar 8, 2007
  Messages: 290
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Ndugu kigwendu, uko sahihi lakini pia tusiwalaumu wanaosema watu kama akina J. M. Kikwete kwani chama kinaendeshwa na watu. Sera, tamaduni, mazoea n.k. vinatengenezwa na watu - chama ni umoja wa watu wenye idiology moja ya namna watakavyoongoza (siyo kutawala) jamii fulani ya watu (nchi) pindi wakipewa ridhaa ya kufanya hivyo - Kama haitoshi ubora wa chama inategema leadership capability za kiongozi wao. Kwa hiyo influence ya kiongozi aliyekabidhiwa chama au nchi haiwezi kuwa sawa na mwanachama mwingine yeyote.

  Ndiyo maana naamini mara nyingi kama si wakati wote ni vigumu kutenganisha chama na watu, hasa waliopewa dhama ya kukiongoza chama, hatimaye na nchi, hasa kwa nchi yetu ambayo chama tawala kila anayechaguliwa kugombea urais automatically anajua kuwa akishinda ataukwaa pia umwenyekiti wa chama.

  Vision ya kiongozi, utayari wake, uthubutu wake, kujitambua kwake, utumishi wake unaweza uka-make difference kiongozi na kiongozi.

  Ubaya unakuja pale watu wanapokuwa walimtegemea sana mtu fulani lakini wanakuja kuwa disappointed pale anapopewa nafasi na akashindwa ku-deliver kama watu wake walivyomtarajia.
   
 5. MANI

  MANI Platinum Member

  #5
  Aug 23, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Nsololi ni kweli chama ndicho kimeshindwa lakini kwa uelewa wa watanzania unadhani wako tayari kujaribu kubadili serekali. Angalia hii mikutano ya kampeni ya hicho chama hao watu wanaokwenda na kushangilia as if hawana shida zozote kwao zilizoletwa na hicho chama. Tunayo safari ndefu lakini tutafika.
   
 6. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #6
  Dec 12, 2010
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Chama hakina tatizo kwani ni chombo tu lakini tatizo ni watu waliopo ndani ya chama. CCM inaundwa na viongozi na wanachama.Asilimia 99 ya viongozi wake ni wapumbavu na asilimia 1 ni wajinga. Na asilimia 99 ya wanachama ni wapumbavu na asilimia 1 wajinga. Kwahiyo chombo hiki kina wapumbavu wengi na jumla ya asilimia 2 ya wajinga na asilimia 0 ya watu wenye akili ndio maana tumeona ufisadi na uzushi mwingi ndani ya ccm na unavumilika kwa hao wote isipokuwa kwa asilimia 2 ya wajinga ambao pia wanashindwa kuchukua maamuzi sahihi je tutafika tuendako? Hapa jibu hatufiki kamwe hivyo yatupasa sisi tulio nje ya chama kuchukua hatua za msingi kushawishi kundi la wanachama wajinga na wapumbavu kukiacha chama na hapa kazi ipo hasa hapa kwa wajinga. Viongozi ni wachache sana watakuja wenyewe watakapoona hawana support
   
Loading...