Uchaguzi 2020 Je, Vyombo vya Habari vitaanza kumpa "Coverage" kubwa Tundu Lissu, mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA?

Sijui kwanini had Leo hawana radio yao jamani..mie Kuna mambo yananikera Sana .Kama baadhi ya majimbo kupitia bila kupingwa .hivi chadema walishindwa toka muda kuwatafuta vijana smart wakawekwa kila Jimbo kupinzana na Hawa NYAU wa Kijani? Yaani najiskia Moto moyoni!Mnyika na Mbowe mnaboa kinyama.
Haa haaa amna hela mwenyekiti anajilipa kwanza 50m .alizozikopesha chama na mwaka huu ruzuku inaenda kwaanguka kwa asilimia 96
 
Habari ya Mjini ni Lissu kwa sasa, wanafikiri kwa kuvikataza vyombo vya habari basi Lissu hatasikika kumbe ndo kwanza habari zake zinatembea kwa speed ya mwanga, jiwe na jopo lake la roho mbaya anataman kupasuka
 
ITV Jana walibalance habari, walilipoti habari za kuenguliwa mkurugenzi wa UCHAGUZI Jimbo la Vunjo, walilipoti kuhusu kuuwawa kwa mvamizi dhidi ya Mgombea CHADEMA Ukara Mwanza, na walilipoti habari ya Lisu baada ya kutangazwa na NEC kuwa mgombea uraisi kwa Tiketi ya CHADEMA. Mambo mazuri yanakuja
Tunashukuru kama vyombo vya habari vimerejea katika kutekeleza majukumu yao kwa weledi
 
Ingawaje kwenye sekta ya habari, kuna kanuni moja Kuu kuwa ni lazima waandishi hao wazisake kwa nguvu zote habari zinazouzika, lakini kwa hapa nchini hali imekuwa tofauti sana, kwa vyombo vyote vya habari nchini, ambapo "vimelazimishwa" kutangaza habari za upande mmoja pekee, za Rais Magufuli pekee, katika kile kinachoitwa, kutangaza juhudi zake za kuliletea maendeleo Taifa letu

Kwa msingi huo huo ni kama habari nyingine zozote zilikuwa zimewekewa "blackout" hususani habari zinazohusu, chama kikuu cha upinzani nchini cha CHADEMA na zinazomuhusu Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, ambaye pia ndiyo mgombea wa nafasi ya Urais kwa chama hicho, Tundu Lissu.

Nikitoa mfano halisi ni namna serikali hii ya awamu ya tano, ilivyotoa "kibano" cha kutoa onyo kali kwa baadhi ya vyombo vya habari vya hapa vya hapa nchini na vingine kupigwa faini kubwa kwa "dhambi" ya kutangaza habari za washirika wao, mashirika ya habari ya nje ya BBC, DW na VoA, walipomhoji mgombea huyo wa kiti cha Urais Tundu Lissu!

Hakika sheria ya vyombo vya habari vya hapa nchini zimekuwa kandamizi mno, kiasi ambacho kunakuwa na "censorship" kubwa mno kiasi ambacho waandishi wa habari wa hapa nchini wanafanya kazi katika mazingira magumu mno, kwa kuwa hawajui ni habari gani ambayo wahariri hao wa vyombo vya habari wataiafiki itolewe kwenye vyombo vyao vya habari!

Kwa hiyo siyo ajabu kuviona baadhi ya vyombo vya habari vya hapa nchini, yakiwemo magazeti ya Tanzania Daima na Mwanahalisi, yakipewa vifungo vya maisha kwa kosa tu la "kubalance story" na siyo kujiegemeza upande mmoja kwa kutangaza mazuri pekee ya serikali hii, bila kukosoa yale ambayo hayafanyiki vyema, ambapo ni kanuni muhimu sana kwenye sekta ya habari.

Kinachoshangaza ni kwa chombo cha habari cha Umma, cha televisheni ya Taifa nchini ya TBC, ambayo inagharimiwa na wananchi wote wa nchi hii, bika kujali itikadi zetu za chama, kwa maana tupo walipa kodi wana-CCM na wana-CHADEMA, kujiunga katika "praise and worship" kwa kumtangaza Rais Magufuli kwa "almost" masaa 24 ya matangazo yao

Kinachotakiwa na watawala wetu wa Serikali hii ya Awamu ya 5 ni kutaka kuona habari zinazowapa wao pekee sifa na mapambio katika kile kinachoitwa maendeleo makubwa sana, yanayofanywa na serikali hii.

Swali ninalojiuliza hivi sasa, je vyombo vya habari vitabadilisha mwelekeo wao na kuanza kuwatangaza wagombea Urais wa vyama vingine, hususani wa kutoka chama kikuu cha upinzani nchini cha CHADEMA?

Kwa kuwa siyo siri tena kuwa habari yenye mvuto mkubwa hivi sasa hapa nchini ni za Tundu Lissu pamoja na chama chake cha CHADEMA, kwa hiyo kama wamiliki wa vyombo hivyo vya habari nchini, vitataka ku-survive, hawana budi kuzitangaza habari hizo za Vyama vya Upinzani.
Hiyo ndio hali alisi kabisa kila ninapo angalia TVs na Ninapo soma Magazeti. Kwa kweli hii hali inasikitisha kwa Tasnia ya Habari nchini karne hii ya 21. NI AIBU!
 
Back
Top Bottom