Je, Vyombo vya Habari vioneshe wazi vyama wanavyosapoti kama Nchi zilizoendelea?

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
Vyombo vya Habari vya nchi zilizoendelea kama Marekani, vimekuwa na kawaida ya kusema wazi Vyama au Itikadi ambazo wanazisapoti katika vipindi vya uchaguzi, na hali hiyo huendlea hata baada ya uchaguzi.

Katika nchi zetu za Afrika vyombo vya habari haviweki wazi labda baadhi ya magazeti ambayo kiuhalisia humilikiwa na vyma husika ambavyo kimsingi mrengo wao huwa wazi kutokana na chama kinacho wamiliki.

Je, unaona haja kwa vyombo vingine kuwa wazi kuonyesha kuwa wanawasapoti watu wa chama fulani katika kipindi cha uchaguzi kama wanavyofanya nchi zilizoendelea?
 
Kwa nchi yetu hilo bado mkuu kwa sababu ni wachanga sana kwenye demokrasia ,yaani nchi hii kumkosoa Waziri ni uhujumu uchumi ,kucheka kinyago unasweka rumande hebu fikiria leo magazeti yote yanaandika kwa kumsifia Rais ,sasa tutapata wapi maendeleo ya kweli katika safari hii lazima mawazo yatofautiane ndipo maendeleo tuyaone lakini ukisema mimi naandika upande wa upinzani maana yake umekubali kupigwa risasi,kuvunjwa pumbu ,kuwekewe tindikali na kubambikiwa kesi za uhujumu uchumi njia nzuri ni wananchi kutaka katiba mpya ambayo itaainisha namna kazi za kiuandishi na waandishi wawe kwa mitindo Gani kwa Sasa nchi yetu ipo kwenye udikteta .
 
Bila katiba ni ngumu wataishia kupigwa risasi, uhujumu uchumi,Kodi,tcra,nk.
Africa kujiongoza bado sana
 
Back
Top Bottom