Je viwanja vipya vya London Kaskazini vina nuksi na laana?

Johnny Sins

JF-Expert Member
Nov 4, 2019
2,538
3,826
ARSENAL ilianza kuharibika lini? Ilipojenga uwanja wake wa Emirates. Ilikuwa inatesa sana ikiwa katika uwanja wa Highbury lakini tangu walipohamia Emirates habari ikageuka. Natania tu, lakini kuna ukweli ndani yake.
Mei 2006 walifika katika fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya. Julai mwaka huohuo wakahamia Emirates. Hawajawahi kufika tena fainali za Ulaya wala kuchukua ubingwa wa England ambao walichukua mara ya mwisho miaka miwili kabla ya kutua Emirates.

Waliyumba sana mpaka miaka ya karibuni walipochukua mataji mawili ya FA. Sikiliza. Kuna sababu nyingi zinatajwa. Ya kwanza ni kwamba Arsenal walikuwa wamekopa kwa kiasi kikubwa kuweza kujenga uwanja wao mpya kando ya Highbury.

Hii ina maana kwamba Arsene Wenger hakuwa na pesa za kununua wachezaji wapya na alilazimika kutunza makinda wake kwa ajili ya kuiruhusu klabu kulipa madeni. Wakati mwingine inadaiwa kwamba alilazimika kuuza mastaa kwa ajili ya kulipa madeni benki.

Mpaka sasa, tangu wahamie Emirates Arsenal sio tu kwamba hawajawahi kuchukua ubingwa wa England, lakini inaonekana hauwasogelei katika miaka ya karibuni. Inachekesha kidogo lakini ndio hali halisi.

Turudi kwa majirani zao wa London Kaskazini, Tottenham. Waliondoka White Hart Lane wakiwa na kikosi imara. Wamejenga uwanja wao mpya ambao bado haujapewa jina. Nadhani wanasubiri mwekezaji mpya ambaye ataupatia jina uwanja huo na kulipa mamilioni.

Tangu watue uwanja wao mpya ambao wameuanza kuutumia katika msimu kamili huu, Spurs wamekuwa nyanya. Wako ovyo. Ni katika uwanja wao huohuo ndio ambao wamepigwa kipigo cha rekodi katika Ligi ya Mabingwa wa Ulaya cha mabao 7-2 na Bayern Munich.

Kwa sasa kinachotabiriwa ni Pochettino kuondoka, lakini pia imeanza kutabiriwa kwamba Harry Kane anaweza kuondoka. Wakati ukidhania kwamba mambo yatakuwa matamu kwa Spurs baada ya kujenga uwanja mpya wa kisasa, ndio kwanza mambo yamekuwa ovyo.
 
Ooooh nimeelewa sasa kwanini Liverpool wanakarabati tu majukwaa hawataki kujenga mpya ilhali uwanja wao ni mbaya.....hahahaha nimekumbuka chelsea wanajiandaa kujenga uwanja mpya so fans wajiandae psychologically
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom