Je, vitunguu swaumu vinapandisha presha?

Akili Kichwani

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
1,508
216
jamani naomba anayejua haya mambo tusaidiane.

nimesikia watu wakishawishi ulaji wa vitunguu swaumu wakidai ni tiba ya magonjwa mengi na ni kinga pia, sasa mimi nilijaribu kutafuna vipunje viwili kavukavu siku moja, nikaanza kusikia mapigo ya moyo yanaenda kasi na ilidumu kama masaa mawili vi, toka siku iyo sijatafuna tena,. sasa kabla sijatafuna tena naombeni ushauri wenu, hivi vitu ni salama kweli kama wanvyoshauri, au ni watu wenye matatizo ya aina gani wanshauriwa kutumia????????

nitashukuru kwa ushauri wenye msaada kwa wengi..............
 
Nimewahi kuvitumia kama tiba ya malaria kwa kuvinywa kwa pamoja na maji ya ndimu. Ilinisaidia.
 
Pole sana ndugu yangu,

Vitunguu swaumu ukila vibichi huwa vinalainisha damu, na damu ikiwa laini mapigo ya moyo huongezeka kwa sababu moyo unakuwa hausukumi kitu kizito hivyo basi kasi ya moyo hukua.

Vitunguu swaumu ni vyema ukatumia punje moja kwa wiki ili moyo upate weekend. Ila haishauriwi kutumia mara kwa mara kwa sababu pindi utakapopata jeraha ni dhahiri utapoteza damu nyingi sana.
 
Pole sana ndugu yangu,

Vitunguu swaumu ukila vibichi huwa vinalainisha damu, na damu ikiwa laini mapigo ya moyo huongezeka kwa sababu moyo unakuwa hausukumi kitu kizito hivyo basi kasi ya moyo hukua.

Vitunguu swaumu ni vyema ukatumia punje moja kwa wiki ili moyo upate weekend. Ila haishauriwi kutumia mara kwa mara kwa sababu pindi utakapopata jeraha ni dhahiri utapoteza damu nyingi sana.

loh, ndio kwanza naysikia haya...........

asante sana mkuu.....
 
Vitunguu swaumu pia vinahusishwa na kurekebisha kiwango cha sukari mwilini kwa kuongeza uptake ya sukari kutumika na misuli, huongeza neutralization ya sumu kwenye ini ikiwa itatumika kwa kiwango moderate. penile dysfunction pia inarekebishwa na vitunguu swaumu. Tatizo ni harufu kali kwa wale utakaokuwa karibu nao kuongea, labda na wao watafune iwe ngoma drawn. Kama harufu ya karanga mkaango ukitafuna usipende kumnong'oneza mwenzio utamkera, mpe atafune naye ili kubalance harufu zenu.
 
Garlic just regulate blood pressure(high or low) through dealing with cholesterol and triglycerides.

Garlic (Allium sativum L) is a common garden plant with an edible bulblike root. it is used for cooking and medicinal purposes.

When fresh garlic is crushed or chopped, enzymes within the clove are released and a sulphur compound called allicin is created. Sulphur-containing compounds are often effective antibiotics. Penicillin is one such example.

Of the sulphur compounds found in garlic, allicin is the most abundant as well as widely studied and appears to be associated with many of the plant's medicinal benefits. But several other sulphur compounds appear to have medicinal benefits. These compounds, found in different forms of garlic, include ajoene and S-allyl cysteine

Advantages
1.To prevent and fight infections
2.To strengthen the immune system
3.To lower cholesterol and triglycerides
4.To slow the production of HIV

Side Effects:
1.Large doses of garlic (the equivalent of 10 or more cloves a day) may interact with
protease inhibitors
2.It is best to avoid combining garlic with drugs that have an anti-coagulant effect such
as acetylsalicylic acid (Aspirin) and warfarin
3.Large doses can cause stomach upset or irritate the intestine

For more nondos visit the links
http://www.garlicfoods.com/lutz1.html
http://www.solgar.com/nutrition_library/healthy_living/garlic.html
http://www.catie.ca/
http://www.thebody.com/health -garlic

All of us we are strongly adviced to take garlic in a form suitable to individual ,my self i take in cooked rice with carrot.
 
hizi tiba za asili ni nzuri sana na zinasaidia ..vitunguu swaumu kweli ni dawa ya magonjwa mengi
wajuvi wa haya wataendelea kutuhabarisha
 
Thanks for your adivices in this... hivi na kwa wa mama wajawazito husaidia nini? Nakumbuka classmate wangu mmoja pale CBE alikuwa akivitafuna hivi sana wakati wa ujauzito wake. Mwenye kujua hili atusaidie.
 
kwa kweli ni dawa lakini ni vikali inahitaji moyo ukiwa unatumia kama tiba tiba yake inaanzia week mbili na kuendelea , hata ukiwa na kihohozi cha kawaida ni tiba magonjwa ya ngozi ni tiba ingawa kama unaugonjwa wa ngozi mfano mashilingi inabidi upake wiki mbili (kila siku unapaka baada ya kd 30, unatoa) lakini ukiwa unapaka mpka kikuunguze kwanza ndio upone ila kovu lake linaisha upesi. so kwa wale wenye magonjwa ya ngozi sugu yasiyosikia dawa ya hosipitali wanaweza kujaribu. ni moyo wako tu.
 
kwa kweli ni dawa lakini ni vikali inahitaji moyo ukiwa unatumia kama tiba tiba yake inaanzia week mbili na kuendelea , hata ukiwa na kihohozi cha kawaida ni tiba magonjwa ya ngozi ni tiba ingawa kama unaugonjwa wa ngozi mfano mashilingi inabidi upake wiki mbili (kila siku unapaka baada ya kd 30, unatoa) lakini ukiwa unapaka mpka kikuunguze kwanza ndio upone ila kovu lake linaisha upesi. so kwa wale wenye magonjwa ya ngozi sugu yasiyosikia dawa ya hosipitali wanaweza kujaribu. ni moyo wako tu.


Pia ni kinga nzuri ya kipindupindu, endapo unakwenda sehemu ina mlipuko kula punje 2-3 yuo are done
 
Kumbeeeeeeeè?. Kadri siku ninavyozidi kuketi kwenye jamvi hili la jF napata mapya nilikuwa nikitambua kijunguu saumu kama kiungo cha mboga ila leo nimetambua ya kuwa kinaweza kutumika kama dawa. Jf inaniongezea maarifa kila ninapo igusa.
 
jamani naomba anayejua haya mambo tusaidiane.

nimesikia watu wakishawishi ulaji wa vitunguu swaumu wakidai ni tiba ya magonjwa mengi na ni kinga pia, sasa mimi nilijaribu kutafuna vipunje viwili kavukavu siku moja, nikaanza kusikia mapigo ya moyo yanaenda kasi na ilidumu kama masaa mawili vi, toka siku iyo sijatafuna tena,. sasa kabla sijatafuna tena naombeni ushauri wenu, hivi vitu ni salama kweli kama wanvyoshauri, au ni watu wenye matatizo ya aina gani wanshauriwa kutumia????????

nitashukuru kwa ushauri wenye msaada kwa wengi..............

inategemea ulikuwa umeweka nini tumboni kabla. Mbona mi nina ulcers lakini navitwanga sana?
 
Faida za Kiafya za Kitunguu Swaumu (Garlic) Featured


1 garlic .jpg
Kitunguu swaumu ni jamii ya vitunguu ambayo kwa kitaalamu huitwa Allium sativum. Jamii hii ilianza kutumika katika mabara mbalimbali duniani hususani Asia, Afrika na Ulaya takribani miaka 6000 iliyopita. Matumizi makuu nyakati hizo yakiwa viungo katika mboga na tiba.


Kitunguu swaumu kimetajwa kwenye vitabu mbalimbali vya dini vikielezea faida zake katika kutibu maradhi mbalimbali yasababishwayo na bakteria, matatizo katika mapafu, matatizo katika mfumo wa umen'genyaji chakula, na matatizo ya kuishiwa nguvu.


Historia inaonesha kuwa, vitunguu swaumu vilianza kutumika China mwaka 510 K.K na pia vilitumiwa na wanajeshi wa Ugiriki na Roma. Aidha wasafiri wa vyombo vya baharini na vijijini pamoja na wakulima barani Afrika walivitumia sana.


Mwaka 1858, mtafiti na mwanasayansi wa nyakati hizo, Louis Pasteur aligundua uwezo wa kitunguu swaumu katika kuua vimelea mbalimbali vinavyosababisha magonjwa, na hivyo vikaanza kutumika kama dawa ya kusafishia vidonda na kuzuia kidonda ndugu hasa zama za vita ya kwanza na pili ya dunia. Isitoshe, mpaka sasa zipo dawa kadhaa zilizotengenewa kwa kutumia jamii hii ya vitunguu swaumu ikiwemo dawa ya kusafisha mdomo (mouth wash) ingawa watumaiji wake wengi huilalamikia dawa hiyo kwa sababu ya harufu mbaya ya dawa hiyo inayowasababishia kunuka kwa mdomo.


Faida za vitunguu swaumu


Katika tafiti mbalimbali vitunguu swaumu vimeonekana kuwa na uwezo wa kutibu maambukizi ya bakteria, fangasi na virusi vya aina mbalimbali. Aidha husaidia kuzuia magonjwa ya moyo ikiwemo kuondoa lijamu katika mishipa ya damu na hivyo kusaidia katika kurekebisha shinikizo la damu. Faida nyingine za vitunguu swaumu ni pamoja na
  • Kutibu saratani ikiwemo saratani ya tumbo na utumbo mkubwa. Tafiti zinaonesha idadi ndogo ya wagonjwa wa saratani katika nchi ambazo wakazi wake wana utamaduni wa kutumia vitunguu swaumu kwa wingi.
  • Vitunguu swaumu husaidia kudhibiti kiwango cha sukari katika damu. Hata hivyo inashauriwa kwamba wagonjwa wa kisukari wanaotumia sindano za insulin wasitumie kitunguu swaumu kwa wingi mpaka watakaposhauriwa na daktari.
  • Huzuia kusanyiko la chembe sahani zinazosaidia kuganda kwa damu (platelet aggregation)
  • Husaidia ufyozwaji wa thiamin, hivyo kusaidia kuepusha mwili na ugonjwa wa beriberi
  • Ina kiasi kikubwa cha vitamini C ambayo husaidia kuzuia ugonjwa wa kiseyeye
  • Hutumika kutibu magonjwa nyemelezi kama toxoplasmosis, hasa kwa watu wenye upungufu wa kinga mwilini.
Ushahidi wa Kitafiti

Katika utafiti uliofanyika nchini Czech ilionekana kuwa matumizi ya vitunguu swaumu yalisaidia sana katika kupunguza kusanyiko la lijamu (cholesterol) pamoja na mafuta yasiyofaa mwilini (low density lipoproteins) katika mishipa ya damu. Aidha, mwaka 2007 BBC iliripoti matumizi ya vitunguu swaumu katika kusaidia kumkinga mtumiaji dhidi ya aina fulani ya mafua iliyosababishwa na virusi. Mwaka 2010, ulifanyika utafiti mwingine ambao ulijumuisha wagonjwa 50 wenye shinikizo la damu sugu ambalo lilikuwa ni vigumu kudhibitiwa hata kwa matibabu yaliyozoeleka ya dawa na njia nyingine. Kama njia ya kuchunguza ufanisi wa vitunguu swaumu katika kutibu shinikizo la damu, baadhi ya wagonjwa hao walipewa vitunguu swaumu wakati wengine walipewa dawa isiyohusika na matibabu ya shinikizo la damu (au placebo). Ilionekana kuwa wale waliopewa vitunguu swaumu kama dawa ya shinikizo la damu walionesha maendeleo mazuri kwa vitunguu swaumu kuweza kushusha vizuri kiwango cha shinikizo la damu, hususani systolic pressure, tofauti na wale waliopewa placebo.


Nini siri ya kitunguu swaumu?


2 garlic.jpg
Sifa kuu zinazokifanya kitunguu swaumu kuwa na uwezo na faida zilizoainishwa hapo juu ni kule kuwa kwake na viasili kadhaa (ingredients) ambavyo vinafanya kazi tofauti tofauti. Uwezo wake wa kiutendaji unatokana na mambo yafuatayo;
  • Vina uwezo wa kusababisha kutanuka kwa mishipa ya damu (vasodilation) kwa kubadilisha polysulfides zilizopo ndani yake kuwa hydrogen sulfides kwenye seli nyekundu za damu.
  • Husaidia uthibiti wa kiwango cha sukari mwilini kwa kushusha kiwango cha kemikali ya homocystine na kupunguza madhara ya kisukari.
  • Iwapo vitapondwa pondwa vizuri, vitunguu swaumu hutoa kemikali iitwayo Allicin ambayo ni dawa dhidi ya bateria, na phytoncide ambayo huua fangasi wa aina mbalimbali.
  • Harufu mbaya ya kitunguuu swaumu hutokana na gesi aina ya hydrogen sulfide ambayo inayotolewa baada ya kuvila.
Nini Madhara ya vitunguu swaumu?


Ukiacha faida zake, vitunguu swaumu pia vina hasara na madhara mbalimbali kwa mtumiaji. Madhara hayo ni pamoja na;
  • Harufu mbaya mdomoni ambayo hutokana na kemikali ya AMS (allyl methyl sulfide). Harufu mbaya hii, hata hivyo, yaweza kupunguzwa kwa kunywa maziwa au kunywa maji mengi.
  • Kwa baadhi ya watumiaji, vinaweza kuwaletea mzio au mcharuko mwili (allergies au inflammatory reactions)
  • Kichefuchefu, Kutapika na kuharisha.
  • Huweza kusababisha hatari ya kuvuja damu, kwa sababu huzuia kazi ya seli sahani (platelets) zenye kusaidia kuganda kwa damu kushindwa kufanya kazi yake vizuri, na hususani kwa mama wajawazito, baada ya upasuaji au mara baada ya kujifungua.
  • Huingiliana katika utendaji kazi wake na dawa kadhaa kama vile warfarin, antiplatelets, saquinavir, dawa za shinikizo la damu kwa ujumla hasa calcium channel blockers, na antibiotiki za jamii ya quinolone kama vile ciproflaxacillin.
  • Aidha, vinaelezwa pia kuwa na madhara kwa wanyama jamii ya paka na mbwa.
 
MATUMIZI KATIKA NCHIMBALIMBALI:
kitunguu ni kiambatanisho muhimu kidishi kimaendeleo katika sehemu nyingi ulimwenguni.
Zamani Egpta iliheshimiwa kuwa ya hadhi ya kimungu.

MAANDALIZI YA KITUNGUU SAUMU KIMADAWA:

Kitunguu saumu na asali. Jaza chupa ya glasi na vitunguu saumu vilivyomenywa na
kukatwa katwa polepole mwaga katika asali ya kwamba inajaza nyufa katikati ya fundo ya

kitunguu. Weka glasi kwenye sehemu ya joto yenye c 20oc. Katika siku mbili hadi wiki nne,
asali itanyonya juisi ya kitunguu saumu na kitunguu hicho kitachechemea na kutoingiza

mwanga usichuje. Tumia katika muda wa miezi 3.
Kitunguu Saumu dawa ya kikohozi

Ponda kijiko cha chai cha kitunguu saumu katika kipimo hicho hicho cha sukari au asali.
Tumia mara moja k.mf. kwa kikohozi.
Kitunguu saumu mafuta. Weka g 200 za vitunguu vilivyokobolewa saga kitunguu saumu na

kuweka kwenye chombo cha glasi na ongeza mafuta ya kutosha (au vizuri mafuta ya chakula)

funga. Funga jagi kwa kubana vizuri, na weka ikae kwenye sehemu yenye joto kama C 20
kwa siku tatu. Tikisa mara chache kila siku. Halafu weka kwenye sehemu ya baridi, bila

kuchuja. Tumia katika muda wa mwezi mmoja.
Kitunguu saumu „tinkcha". Loweka g 200 za vitunguu vilivyomenywa na kukatwakatwa
katika lita moja ya brandi au alikoholi 40-50%, kwa siku 14 kwenye C 20° katika chupa

yenye kufungwa vizuri bila kupitisha hewa. Tikisa chupa hiyo mara nyingi kwa siku. Chuja
vipande vya kitunguu saumu. Tinkcha inakaa muda wa mwaka.

MAPENDEKEZO YA MATUMIZI
Kula kitunguu saumu kibichi- hii ni bora.
Tumia katika kupika.

Kula vitunguu saumu vingi kuzuia magonjwa. Kitunguu saumu ni safi sana kwa mfano kuna
usemi kwamba, chakula chako kiwe ndiyo dawa yako, na dawa yako chakula chako. Hii ni
kweli tu, hata hivyo, kwa kitunguu saumu kibichi, kama ilivyo vitu vingi vyenye nguvu

vinaangamizwa katika kupikwa. Vitunguu saumu vibichi vinatia nguvu katika mfumo wa
kinga ya maradhi. Matumizi kawaida ya vitunguu saumu yameonyeshwa katika kupunguza
madhara ya magonjwa ya moyo, kiharusi, kansa, msukumo wa damu na homa ya mafua

makali (flu). Tunashauri kwa nguvu ya kuwa wanaoteseka kwa UKIMWI (AIDS) waweke
kitunguu saumu katika chakula chao cha kila siku, kupunguza nguvu ya magonjwa mengine.

Kwa sababu inafanya mara mbili, kwa matumizi ya nje na kwa ndani kama dawa ya kuua
wadudu, vitunguu saumu ni masaada wa kutibu magonjwa yote ya kuambukiza; Toifodi,
minyoo, bilhazia, malaria, damu yenye maambukizo na sumu n.k. Zaidi yake vitunguu saumu

vinaimarisha kumbukumbu, hupunguza shindikizo la damu na Homa, na vinafanya kazi
kupinga ugumu wa kuta za ateri (hardening of arteries). Vitunguu saumu pia vinapinga virusi
na dhidi ya kinyume cha mambo ya fangasi.


Majipu au uvimbe na chunjua.

Saga vitunguu saumu vibichi na funga vilivyopondwa kwenye sehemu ya jipu, uvimbe au
Chunjua mara mbili kwa siku na gandamiza. Anza matibabu haya mapema iwezekanavyo.

2. Amiba.
Katakata vitunguu saumu sawasawa vipande vidogo na chukua kijiko kikubwa 1 pamoja na
Chai mara tatu kwa siku (usitafune, kusaidia kupinga kutoa harufu mdomoni). Endelea na
Matibabu haya kwa siku 5. I (H-M Hirt) aliponywa mwenyewe toka Amiba kuharisha
damu kwa Tiba hii.

3. Malaria.
Katakata vitunguu saumu sawasawa. Meza kijiko kimoja cha vitunguu hivi mara tatu kwa
Siku na kunywa lita 2 za limao glasi ya chai kwa siku. Endelea na tiba hii kwa siku 5.
Angalia pia ukurasa wa 8 kwa ajili ya malaria.

4. Kisukari, shindikizo la damu, kinga ya ugumu wa kuta za arteri (hardening of the
arteries).
Kula vitunguu saumu kwa wingi, vitunguu saumu na vitunguu vinapunguza sukari katika
damu na kusawazisha damu ya cholesteroli, na shindikizo la damu. Badala yake chukua
matone 20 ya vitunguu tinkcha mara 3 kwa siku, basi hii ni pungufu ifuatayo:

5. Kikohozi, homa, sinusitis na kuvimba koo.
a) Kula klovu ya vitunguu saumu mara tatu kwa siku.
b) Chukua kijiko cha chai cha kitunguu saumu asali kila masaa machache.
c) Watoto wanaweza kutumia kijiko cha chai cha kitunguu saumu
mchanganyiko kila baada ya masaa machache.
d) Chukua kijiko cha chai cha kitunguu saumu mafuta mara 6 kwa siku.
6. Kandika.

Chukua kijiko cha chai cha kitunguu saumu au kitunguu saumu yenye asali, kila masaa
machache. Weka mdomoni kwa muda mrefu iwezekanavyo.

7. Fangasi inayoambukiza pamoja na ugonjwa wa ukungu kwenye vidole vya miguu.
Funga sehemu zilizoathirika kwa juisi ya vitunguu saumu vibichi vilivyopondwa au
mafuta.

8. Homa ya matumbo na maambukizo mengine.
Kama itatokea homa ya matumbo, bacillary, kuharisha damu, kifua kikuu, kipindupindu,
trypanosomiasis (ugonjwa wa kusinzia): Siku zote ongeza kitunguu saumu kwa tiba ya
kawaida.

9. Kinga ya mishipa ya damu.
Kitunguu saumu siku zote kinafanya damu kuwa laini na kukinga kutengeneza damu
kuganda ambayo inasababisha shida ya thrombosis. Hii ni muhimu kwa wagonjwa
wanaolala kitandani kwa muda mrefu.
10. Kuota meno utotoni.
Futa ufizi kwa fundo la kitunguu saumu.

MADHARA YAKE:

Kitunguu saumu kinaweza kukera ngozi hasa baada ya kutumia kwa muda mrefu. Epuka
kuhusisha kwenye macho.
 
Kweli JF wasioijua wameingia hasara. Mafunzo ni mengi, sio wote wanatoa bla bla na ushabiki usio tija. Nawahamasisha watu wajiunge na kutoa michango yao, sema usikike.
 
Back
Top Bottom