Je, vitisho vya kuuawa Zitto vilikuwa na uhalisia?

meningitis

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
8,331
2,000
Hapa chini nawaletea kipande cha maelezo ya Zitto katika moja ya threads maarufu zilizowahi kutokea humu jamvini ambapo bavicha walikuwa wakishambuliana.

#Ninasikitika sana kuona wanachama wa CHADEMA wanavyoweza kutumika kwa maslahi ya kundi fulani kuharibu heshima ya viongozi wao mbele ya jamii.

Ninaomba ndugu Ben Saanane aje hapa jukwaani kuthibitisha maelezo haya ya Bwana Mamuya kutoka Arusha. Mimi binafsi nikikutana na Ben Saanane leo naweza kupishana naye maana sijawi kumwona, wala kukutana naye. Ndugu Ben Saanane nimewasiliana naye kwenye simu mara mbili au tatu kuhusu masuala yake ya kitaaluma au pale alipohisi kuonewa ndani ya chama. Sijawahi kukutana naye hata siku moja. Kama nasema uwongo yeye binafsi aje hapa kukanusha.

Mimi pamoja na wenzangu tumejenga chama hiki mpaka hapa tulipofika. Tumeingiza watu kwenye chama hiki ili kwa pamoja tuweze kujenga asasi imara kabisa ya kidemokrasia. Chama hiki kina damu yangu. Chama hiki kina muda wangu. Chama hiki kina jasho langu. Nitakuwa mtu wa mwisho kusaliti chama hiki. Sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa tofauti na CHADEMA. Sitarajii kuwa mwanachama wa chama zaidi ya CHADEMA.

Ninawasihi wana CHADEMA tuache propaganda za kuchafuana. Nguvu kubwa inayotumika kumchafua Zitto ielekezwe kwenye kujenga taasisi imara ya CHADEMA, chama chenye demokrasia, kisicho na upendeleo, chenye uwakilishi wa kitaifa na chenye kuthamini nafasi ya kila mwanachama.

Mamuya, mara kadhaa umetaka kuniona kwa sbaabu nisizozijua na imekuwa ikishindikana. Unapata dhambi kubwa sana kumwaga sumu unayomwaga kwa mtu usiyemjua wala hujawahi kukutana naye.Acha kutumika. Jisimamie. Simamia chama.

Vijana, wote wa vyama vyote, siku zote simamieni misingi (principles) na sio kusimamia watu. Watu sio mawe. Mtaja juta. Misingi inadumu. Watu hawadumu. Acheni kuramba miguu ya watu. Simamieni misingi ya chama. Misingi ya nchi yetu. Misingi ya demokrasia. Kataeni kutumika.

Angalieni, wanaozungumzia sana usaliti waweza kuta ndio wasaliti wakubwa. wanazungumzia usaliti kama 'defensive mechanism'.
Tuacheni ujinga huu. Tufanye kazi. Kazi tu ndio kipimo cha ukamanda na sio kurambaramba visigino vya watu.

Mwisho, nasikia sikia sana habari za kuchinjana. Kuuana nk. Nasikia habari hizi kwa watu wale wale wa kikundi kile kile. Moja, natoka Kigoma. Nimeaga kwetu. Nitakufa kwa amri ya Mungu. Siogopi kufa. Iwapo kifo changu kitatokana na mkono wa mtu, sidhani kama kwa mtu huyo kama hata panya atabaki nyumbani kwao. Underline this.#

Truncated

Pili, revolutioneries don't talk about deaths. Only cowards do.
 

Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
17,747
2,000
Mimi pamoja na wenzangu tumejenga chama hiki mpaka hapa tulipofika. Tumeingiza watu kwenye chama hiki ili kwa pamoja tuweze kujenga asasi imara kabisa ya kidemokrasia. Chama hiki kina damu yangu. Chama hiki kina muda wangu. Chama hiki kina jasho langu. Nitakuwa mtu wa mwisho kusaliti chama hiki. Sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa tofauti na CHADEMA. Sitarajii kuwa mwanachama wa chama zaidi ya CHADEMA
🤣🤣
 

Naipendatz

JF-Expert Member
Jul 27, 2011
2,882
2,000
Mbowe ni jambazi na dikteta akiyejificha kwenye kichaka cha upinzani! Ni Mbowe huyu huyu aliwakataza viongozi na wanachama wa CDM wasiende kumzika mama yake Zitto ambaye pia alikuwa mjumbe wa kamati kuu wa chama, halafu leo eti wanalalamika Magu kuwazuia wanaCCM kwenda kumuona Lissu Nairobi, wanafiki wakubwa
 

artch2311

JF-Expert Member
Jan 5, 2016
1,115
2,000
Uzi huu utapata wachangiji wachache sana yaan. Nami niongezee kauli moja ya Zitto wakati akiwa kwenye kilele cha mtafaruku na Chadema, aliwahi nukuliwa akisema CHACHA WANGWE DIED BUT I WON'T
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom