Je, Vita dhidi ya ubaguzi na tofauti wa usawa baina ya watu yawezekana vilishindwa kabla ya kuanza?

Immortal Joe

New Member
Nov 10, 2021
3
1
Licha ya kuwa na kampeni za muda mrefu zenye lengo la kutuamasisha na kutuaminisha katika jamii yenye usawa ambayo haina ubaguzi lakini bado tunaendelea kushuhudia gap kubwa la utofauti wenye kuheshimisha na kudidimiza mtu dhidi ya mtu fulani au jamii fulani dhidi jamii nyingine. Je kwa hali ilivyo twaweza kupata kibali cha kusema kuwa vita dhidi ya ubaguzi vilishindwa kabla ya kuanza?

Swali hilo linaweza kujibiwa kwa hoja zifuatazo ambazo zitakuwa katika mfumo wa maswali.

Hoja ya kwanza ni kwa nini kuna uwepo wa jinsi mbili mwanaume na mwanamke? Ni wazi licha ya wote kuwa na sifa zinazofanana bado kuna tofauti inayofanya mmoja kuitwa mwanamke na mwingine mwanaume asili imewatofautisha je wewe mwanadamu una mamlaka gani kutaka mwanaume na mwanamke wawe sawa? Hii haimaanishi upande mmoja unapaswa kudharauliwa au kukandamizwa wote tunahitaji kuheshimiana.

Hoja ya pili ni kuwa dunia ina mabara 7 yenye asili ya watu tofauti kuanzia Wazungu, Waasia na Waafrika. je kama kweli dunia ilihitaji usawa kwa nini pasingelikuwa na bara moja lenye asili moja ya watu? Hiyo inaonyesha ubaguzi wa rangi ulikuwepo, upo na utaendelea kuwepo kikubwa ni jamii fulani kujikubali na kufurahia asili yao.

Hoja ya tatu ni utofauti wa uwezo katika kufikiri na vipaji kama kweli uumbaji wa dunia ulidhamiria kuwa na usawa ni kwa nini kuna utofauti mkubwa wa uwezo ya mtu mmoja mmoja?

Hoja tatu hapo juu zinathibitisha kuwa ulimwengu wenyewe ndo muasisi nambari moja wa kutokuwepo na usawa ulimwenguni kwa hiyo kuhamasisha usawa ni kupingana na asili ya dunia ilivyo hatimaye matokeo yake ni kuzidisha matatizo kuliko kupunguza tatizo la usawa.

Mwisho huu ni mtizamo wa mtu binafsi wa Immortal Joe na sio hitimisho.
 
Pamoja na tofauti ama kutokuwepo na usawa we hakikisha ukae sehemu bora sio ya ma victim wa hii hali ya dunia kutokuwa na usawa
 
Back
Top Bottom