Je viongozi wetu wanapata commission kwa kuhakikisha muundo wa muungano haubadiriki? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je viongozi wetu wanapata commission kwa kuhakikisha muundo wa muungano haubadiriki?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ntemi Kazwile, Apr 11, 2011.

 1. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #1
  Apr 11, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mimi naanza kuwafikiria viongozi wetu vibaya, inawezekana wananufaika kwa kupata fedha za comission kwani kama wananchi wa pande zote mbili za muungano wanaona muundu huu wa muungano hautufai lakini viongozi wamekataa kata kata, zaidi ya yote wanataka kupitisha sheria itakachokifanya kitendo cha kuujadili muungano kuwa kosa la jina sawa sawa na wizi, mauaji, uhaini, n.k.

  Haiingii akilini kwa mtu ambaye hana manufaa na kitu fulani kulazimisha kitu hicho kuendelea kuwepo hata kama kitu hicho kinamgharimu kuwa nacho... Ukimuuliza mtu yeyote mwenye uelewa wa Muungano wetu atakwambia kuwa Tanzania Bara inagharamia shughuli zote za kuendesha mambo ya muungano na kwa maana hiyo hakuna manufaa yoyote kwa wananchi wa Tanzania Bara isipokuwa misifa (kuwa nchi iliyodumisha muungano) BASI!

  My theory of things:
  Kama kuna pesa inatumwa na serikali ya mapinduzi kwa ajiri ya kuendeshea serikali basi pesa hiyo huishia kwenye mifuko ya wajanja (wanaotaka muungano huu uendelee kuwepo au kuna pesa huwa zinachotwa kutoka benki kuu ya Tanzani kupelekwa Zanzibar ambazo huishia kwenye mifuko ya wajanja) .... Hawa kwa namna yoyote ile watasisitiza kuwa muungano huu uendelee kuwepo kwani unawanufaisha! .... Vinginevyo watuache tujadili na tukubaliane muundo wa muungano tunaoutaka!
   
Loading...