Je, viongozi wetu ni 'Smart Upstairs' kiasi gani?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,782
Its so sad. So pathetic. Kwamba Africa sisi bado sana katika Africa yetu tumeamua kuipa SIASA thamani kubwa kuliko taaluma hivyo basi SIASA ina nguvu kubwa sana KULIKO taaluma na ndio inayotuamulia mustakabali WETU. Politic

Kipindi cha miaka mitano ya uongozi wa kisiasa ndio kinafikia tamati hivi karibuni. Je, tuna nini cha kujivunia kama taifa? In terms of uwezo na UTHUBUTU wa kutenganisha SIASA na TAALUMA?

Sioni matumaini bali naona kujikomba, naona kujipendekeza, naona kujitoa ufahamu, naona kujikataa utu binafsi, nauona woga na hofu, naona kinyaa na aibu ya watu wazima na elimu zao na familia zao na utu wao wakiwa wala matapiko na walamba viatu vya wakubwa kisa tu wapate teuzi za nafasi za kisiasa.

Its so pathetic. Kwamba hata forums nyingi kwa sasa hazina mijadala mingine zaidi ya hizi chaguzi za kisiasa
  • Kugombea
  • Kutia nia
  • Kuomba ridhaa
  • Kushikana uchawi
  • Rushwa na milungula
Tunaziishi nyakati ngumu. Siasa za Tanzania zimepoteza matumaini ya wengi. Zimefisha ndoto za vijana wengi. Viongozi wetu wa sasa uono wao ni kimo cha mbilikimo lakini tunaogopa kulisema hili waziwazi kwa kuhofia maisha yetu.. Hofu iko kila mahali. Vijana mamluki waliomwagwa kila mahali kwa ahadi kemkem ni kitisho kwa maisha ya wengi. Tuliowategemea kuwa viongozi wetu wa kisiasa ni WAPUUZI kuliko upuuzi wenyewe.

Jr
 
SWALI: Nchi Masikini sana na Ipi?

JIBU: Ni ile inayopuuza na kudharau Wataalamu na utaalamu wao na kuwathamini Wanasiasa na siasa zao.

Siasa ni Maneno/mbwembwe kuhusu maendeleo ila Taaluma ni Maendeleo halisi.

Imagine hata wasomi wakubwa wameona kukimbilia kwenye siasa ni muhimu zaidi kuliko kustick kwenye taaluma zao ili kusaidia watu.

Watizame Prof. Ibrahim Lipumba, Prof. Jumanne Maghembe, Palamagamba Kabudi, Dr. Godwin Mollel n.k

Hawapo tena kwenye vituo vya kazi, wapo siasani wakijisifu na kujipendekeza ili wapate au wabaki kwenye vyeo.

Inna lillah....!
 
Tatizo la watu wasio na uwezo wa kuongoza, kujiaminisha kuwa wana uwezo, bila ya kujitafakari wanagombea, wapiga kura ni masikini wenye uelewa mdogo, wanasiasa hawa uchwara, hutumia umasikini na ujinga (mtaji wa ccm) wa wapiga kura kujiweka madarakani.
Kutojiamini kwa wanasiasa uchwara waliopewa madaraka, hupelekea kutumia vitisho, kulinda uwezekano wa kuumbuliwa, kulazimisha maamuzi yasiofuata ukweli wa sayansi na sheria hata katiba, na kuhonga kwa hali ya juu wasaidizi na watumishi wa umma ili kulinda maslahi yao binafsi na chama chao.
 
Ndugu Mshana Jr vipi na Wewe pia tukikuuliza kwa hiki ulichokiandika ( ulichokileta ) kwamba upo Smart Upstairs Kwako tutakuwa tunakukosea?
 
Siwezi kujihoji na kujipa credit kwenye andiko langu mwenyewe.... Wewe ndio wa kuona uhalisia wa nilichoandika... Hasa kama tu utakuwa na uono wa kuweza kuona

Jr
 
Yule Jaffo bila hata ya aibu anamnyanyapaa Meneja wa Tarura mbele ya vyombo vya habari! kisa tu hajawakusanya watu wa kuja kumsifia Bwana wake!!!

Kwa hali hii bora hata ya kujiajiri aisee.
Kuna siku taaluma itachukua nafasi yake muhimu na kupata heshima inayostahili.. Wataalam na wanataaluma thamani yao itaonekana na wanasiasa watachutama wakose pa kujificha

Jr
 
.
IMG_20200531_072737_186.jpg
 
Well said, una hoja nzur
Its so sad. So pathetic. Kwamba Africa sisi bado sana katika Africa yetu tumeamua kuipa SIASA thamani kubwa kuliko taaluma hivyo basi SIASA ina nguvu kubwa sana KULIKO taaluma na ndio inayotuamulia mustakabali WETU. Politic

Kipindi cha miaka mitano ya uongozi wa kisiasa ndio kinafikia tamati hivi karibuni. Je, tuna nini cha kujivunia kama taifa? In terms of uwezo na UTHUBUTU wa kutenganisha SIASA na TAALUMA?

Sioni matumaini bali naona kujikomba, naona kujipendekeza, naona kujitoa ufahamu, naona kujikataa utu binafsi, nauona woga na hofu, naona kinyaa na aibu ya watu wazima na elimu zao na familia zao na utu wao wakiwa wala matapiko na walamba viatu vya wakubwa kisa tu wapate teuzi za nafasi za kisiasa.

Its so pathetic. Kwamba hata forums nyingi kwa sasa hazina mijadala mingine zaidi ya hizi chaguzi za kisiasa
  • Kugombea
  • Kutia nia
  • Kuomba ridhaa
  • Kushikana uchawi
  • Rushwa na milungula
Tunaziishi nyakati ngumu. Siasa za Tanzania zimepoteza matumaini ya wengi. Zimefisha ndoto za vijana wengi. Viongozi wetu wa sasa uono wao ni kimo cha mbilikimo lakini tunaogopa kulisema hili waziwazi kwa kuhofia maisha yetu.. Hofu iko kila mahali. Vijana mamluki waliomwagwa kila mahali kwa ahadi kemkem ni kitisho kwa maisha ya wengi. Tuliowategemea kuwa viongozi wetu wa kisiasa ni WAPUUZI kuliko upuuzi wenyewe.

Jr
 
Siasa inaumza kwakwel, yaan nmechukia had nmekosa cha kuandka

Back
Top Bottom