Je Viongozi wetu ndani ya Upinzani wana tafsiri sahihi ya Upinzani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je Viongozi wetu ndani ya Upinzani wana tafsiri sahihi ya Upinzani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by NewDawnTz, Apr 14, 2011.

 1. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Nimejiuliza sana hili swali kwa kuangalia matamshi ya wanasiasa wanaohama Upinzani na kurudi chama tawala, hasa kauli za Sambwee hivi karibuni....naamini hakuna dhambi kuhama kwenda chama tawala lakini kuna maswali ya kujiuliza

  Sambwee, kama wengine, ameapa kwa nguvu zake zote kuwa atakibomoa CHADEMA mkoa wa Mbeya kwa nguvu zake kama alivyokijenga.....sina uhakika kama watu wa Mbeya ni wajinga kiasi cha kumpa nafasi hiyo maana naamini walimuunga mkono kujenga upinzani imara sio kwa kuwa yeye ni mkali na shujaa bali kwa kuwa walitaka upinzani imara

  Hii inanisukuma kujiuliza maswali ambayo naomba wadau tusaidiane;-


  1. Je unadhani wanasiasa wetu walioko upinzani wanaelewa nini maana na umuhimu wa Upinzani?
  2. Je wanapojenga upinzani wanajenga kwa ajili ya nani? Kwa ajili yao wenyewe na umaarufu au matumbo yao wenyewe au kwa faida ya kuboresha upinzani kwa maana ya hoja mbadala za namna ya kusimamia njia za kiuchumi, huduma za kijamii na hata mfumo bora wa kisiasa na kiutawala?
  3. Wanadhani anaenufaika na wao kujenga upinzani au kuathirika na wao kubomoa upinzani ni viongozi wa vyama wanavyohama au ni wananchi wa kawaida ambao wanahitaji upinzani imara na uliokomaa ili kuwapa wananchi wa kuamua kubadilisha serikali/chama tawala wanapoona hakiwajali tena?
  4. Je wananchi tunahaja ya kuwasikiliza watu wa namna hii na kuwaamini kuwa bado wanatutakia mema?
  Umuhimu wa kujiuliza na kujibu maswali ni kwa kuzingatia umuhimu wa mfumo wa vyama vingi na kuwa na upinzani imara ili kuwapa wananchi option iliyo bora kubadilisha chama tawala wanapoona haki-deliver the best kwa wananchi kwa njia ambayo ni salama zaidi ya Social and Political Change kwa maana ya "Conventional Politics path"..

  Kama hakuna upinzani ulioimarishwa maana yake ni kwamba "conventional politics path" haitaweza kutumiwa na wananchi na matokeo yake, kwa kuwa msukumo wa mabadiliko ya kijamii (social change), ni mkubwa, wananchi watatafuta njia nyingine ya kuleta mabadiliko hayo na uzoefu unaonesha wazi kuwa njia hii inapofail basi wananchi huhamia kwenye approaches nyingine ambazo ni Violence kwa matumizi ya nguvu za kijeshi (mfano American Revolution and/or Chinese Revolution) au hata kuhamia kwenye approaches nyingine ambayo sio matumizi ya kijeshi wala conventional politics lakini ni vurugu tupu ikiwamo
  [FONT=&quot]rallies, vigils, ostracism, strikes, work-to-rule, boycotts, sit-ins, fasts ili kuweza ku-set alternative political structures

  Ni vema wananchi tuwasaidie kutafsiri na wajifahamu na kubadilika....Sambwee and the rest, Tanzania inahitaji upinzani imara kwa faida ya watanzania

  Nawasilisha na karibuni kwa mawazo

  [/FONT]
   
 2. K

  Kana Amuchi Member

  #2
  Apr 14, 2011
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yaacheni magugu na ngano yaote na kukua pamoja. bwana wa mavuno akija ataivuna ngano na kuiweka ghalani na magugu atayafunga pamoja na kuyachoma moto. usishangae, magugu hayo yanajitenga na ngano.
   
 3. R

  Ray 4 Member

  #3
  Apr 14, 2011
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 37
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Kwa kweli inaonesha Wengi hawajui na hiyo inadhihirishwa pale tunaposhuhudia viongozi wa upinzani wanapohamia chama tawala. Mimi nadhani watu vigeugeu kama hawa ni wakupuuzia maana ukiangalia hata wenzetu walioendelea hawahamagi vyama kama hawa wakwetu ambao kila kukicha wanahama. Wenzetu wako busy kujenga upinzani wao hata kama wakiwa kwenye hali ngumu kiasi gani. they just pull new strategies za kuchukua serikali badala ya kuhama chama kama hawa washamba wa hapa bongo.
   
 4. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #4
  Apr 14, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Tatizo hilo alivihusu tu vyama vya upinzani bali wanasiasa kwa ujumla; kwao jambo linalowapeleka kwenye siasa siyo utumishi bali nikuwatumia wananchi kwa maslahi yao wenyewe. Dhana hiyo ndiyo inayoibua hii misamiati ya "wananchi wangu" kama kwamba kwa kumchagua kuwawakilisha bungeni hiyo inakuwa sawa na kuwanunua, tena siyo kwa kipindi hicho tu anapokuwa amechaguliwa bali milele. Na hivyo utawasikia baadhi ya wabunge wakilalamika, eti fulani ananiingilia kwenye jimbo langu! Ninachotaka kusema ni kwamba kutokana nakasumba hiyo iliyojengeka katika imani ya wanasiasa wengi, hasa wa upande wa chama tawala, wananchi wa kawaida wanawachulia kuwa ni dhana tu yakutumikisha jinsi wapendavyo.
   
Loading...