Je, Viongozi wa Afrika kuwatumia Wananchi wao Masikini kama turufu yao Kisiasa Wakihutubia ndiyo Siasa bora, Uadilifu na Maendeleo?

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Na Kinachoniuma kama siyo Kunisikitisha hata hao Masikini wenyewe (ama kwa Kujua au Kutokujua) wakiwa wanatajwa katika Mikutano ya Hadhara ya Viongozi wa Kiafrika (Afrika) kuwa ni Masikini na Wasibughudhiwe hufurahia kweli kweli.

Nijuavyo kwa Kiongozi mchapakazi, makini na anayejitambua kamwe hawezi Kuwatumia Masikini wengi kama ndiyo Turufu yake ya Kujijenga zaidi Kwao na Kujiimarisha kiumaarufu wake.

Kiongozi Mzuri wa Afrika ni yule tu anayepambana kila uchao kuwainua Masikini wengi lakini siyo yule anayependa Masikini wazidi Kuongezeka, wabakie pale pale Kimaisha kisha kila baada ya Miaka yake Mitano aendelee Kuwatumia Kisiasa na Kuwadanganya huku Keki ya Taifa ikiishia tu kwa wana Familia wake, Walinzi wake, Waganga wake wa Kienyeji (kama anao) na Mahawara zake mbalimbali.

Nimalize tu kwa kutoa Pongezi kwa Timu za Maandalizi ya Mikutano ya Hadhara ya Viongozi wa Afrika kwa kupatia vyema kabisa Kuwapeleka Wahudhuriaji ambao si tu ni Masikini (kama wanavyokubali Kuitwa hivyo) bali pia ni Wapumbavu Wakomavu ambao muda wote tu Kiongozi akiwa anaongea hata Pumba (Upuuzi) wao Kazi yao ni Kushangilia huku wakisubiria Ubwabwa wa Vikundi na Maji ya Mifuko wanywe kisha warejee Makwao Kuzaliana kama Sungura Pori kusudi wazidi kupanua Wigo wao wa Umasikini, Taabu, Shida na Dhiki.
 
Hawa huwatumia viongozi wa chama chao kuwarubuni watu maskini,wasio na elimu na wachumia tumbo kwenda 'kumjaza upepo ' mfalme kwa kumshangilia hata akisema upuuzi mtupu.

Watawala wetu hakuna kitu wanapenda Kama kushangiliwa hata kama washangiliaji hawajui wanashangilia nini
 
Mtaji wa CCM ni wananchi wajinga, mafisadi na mafukara.
Mafisadi wako salama zaidi ndani ya chama
 
Hakika hili kimekuwa linanifikirisha sana. Watu wanaambiwa nyie ni wanyonge mtu asiwaguse, wanapigia vigelegele na vifijo
Laiti Ugonjwa wa Corona ungekuwa unatuuliza Uondoke na nani Mimi kila mara ningekuambia uondoke na Wapumbavu wote tu ( hasa hasa ) wale wanaokubali Kuitwa Masikini huku Wakishangilia na kutumika ngazi ya Kisiasa kwa Viongozi ( Marais ) wao Wanafiki tupu.
 
Hawa huwatumia viongozi wa chama chao kuwarubuni watu maskini,wasio na elimu na wachumia tumbo kwenda 'kumjaza upepo ' mfalme kwa kumshangilia hata akisema upuuzi mtupu...
Na Kiongozi ukiona Kundi kubwa la Watu wanaokusikiliza (unaowaita Masikini na Wanyonge) linakushangilia kwa kila Pumba unazozitoa mbele yao jua Wewe ni Mpumbavu zaidi yao na wenye Akili Kubwa ndani ya hiyo nchi si tu Wanakudharau bali walishakudharau Kitambo sana.
 
hiki chama ni vema MABEBERU wakatusaidia kuking'oa madarakani... kinatumia njia za mabavu na ulaghai kusalia kwenye dola!.
 
Back
Top Bottom