Je, vijana wa CHADEMA wamechoka au kuna mgomo baridi?

Mtulia anakubalika Kinondoni hiyo ni fact...sasa ili atekeleze sera zake smoothly akaamua kujiunga kwenye chama dola...na hii ni kwa sababu chadema ya sasa haitaki wabunge wake washiriki maendeleo.
Kwani mtulia alikuwa chadema?
 
Wakazi wa kinondoni wanasema jimbo la kinondoni ni la cuf tu chadema wamekuja kumuhalibia cuf ushindi wake

hata hivyo inasemekana kuna vikao vya siri vimefanyika magomeni katika ofisi mpya ya maalim seif

Katibu mkuu wa cuf maalim seif pamoja na mwenyekiti wa facebook tawi la CUFmtandaoni julias mtatiro walikutana na viongozi wa chadema akiwemo Mbowe

Inasemekana chadema baada ya kuona hali ni tete katika jimbo la kinondoni wanapata upinzani mkali kutoka kambi ya lipumba wameamua kutoa mpunga kinyemela na kuwakabidhi timu seif ili wawaunge mkono kwa kupeperusha bendera za cuf katika mikutano ya chadema na kumnadi ya kwamba huyu ndio mgombea wa ukawa

Baaada ya CUF lipumba kutonywa kuhusu hiyo isue nategemea kuona mnyukano mkali wa kareti na judo katika jimbo la Kinondoni.
 
Katimize majukumu yako wewe! Au kwa vile wewe na bosi wako HM hamjui mnafanya nini hapo basi mnaenda hovyo tuu?
Mnadhani kazi ya hapo ni kudeal na vimini tuu?
Chadema hali Mbaya
na mtapigwa majimbo yote hayo
Utaniambia
 
Chagadema hali Mbaya
na mtapigwa majimbo yote hayo
Utaniambia
Kupigwa labda iwe mapanga na mabomu lakini kura hilo huwa halipo. Kama mnahakika na hilo hayo mabasi ya UDA yanayowaleta mikutanoni watu wa Bagamoyo ya nini? Maana hao hawapigi kura hivyo haiwasaidii labda katika kujenga mazingira ya kuiba tuu
 
Mtulia anakubalika Kinondoni hiyo ni fact...sasa ili atekeleze sera zake smoothly akaamua kujiunga kwenye chama dola...na hii ni kwa sababu chadema ya sasa haitaki wabunge wake washiriki maendeleo.

hahahaha, huijui kinondoni kaa kimya, eti Mtulia anakubalika Kinondoni..
Mtulia aliweza kuwa mbunge kupitia upepo wa ukawa tofauti na hapo hakuna aliyemjua Mtulia Kinondoni, kifupi ni kwa sababu utaratibu ulisema jimbo wapewe CUF. Miaka yake miwili kama Mbunge wa kinondoni ameifanyia nini kinondoni?, maana uzuri tunaweza kumpima kwa kuwa kiongozi kabla kinondoni..
 
Kila wakati na kitabu chake, Chadema ime graduate mambo ya kupost picha za mikutano tumewaachia kina jingalao wajifurahishe this time Chadema inapiga kimya kimya.
Watu wamechoka.
Katika hali hii unaanzaje kupost picha???
tapatalk_1517396901926.jpeg
 
MsemajiUkweli ulicho ongea ni ukweli ulio dhahiri, kuna kila dalili ya kukata tamaa na baadhi yao wameshakubali matokeo kuwa wamedondoka jimbo la Kinondoni. Mkutano wa ufunguzi wa kampeni wikendi iliyopita umetoa taswira kubwa.

Binafsi zaidi ya kuona video ya Lowasa ambayo imetumika kama dhihaka sijaona picha za mkutano wa ufunguzi wa CDM. Kawaida ya CDM picha ya tukio lake kubwa lazima itapewa promo kubwa JF na whatapp zitazunguka sana. Kama hali ita endelea hivi ni ishara ya wazi ya baadhi ya wanazi kukata tamaa na wameshakubali kushindwa.

Mbaya zaidi, CDM wakipoteza haya majimbo itaharibu sana hamasa na saikolojia ya “ makamanda “, bila shaka na migogoro ya ndani itazidi kufukuta sababu lawama zitaongezeka za nini na nani ni tatizo, muda ndio jibu, ila huu unaweza kuwa mwaka mgumu zaidi wa CDM zaidi ya 2017 aliyousema Mbowe.
 
Kwenye maisha hamuwezi wote kuwa level moja lazima liwepo kundi la wahamasishaji na wahamasishwaji na unapofanya fadhila usingoje shukrani..hata vijana wangu wa UVCCM kinondoni nhuwa nawambia hata mpige mayowe vipi mwisho wa siku inabidi mmpiganie wakuja Mtulia hutaki ondoka CCM.
Mkuu;

Hoja yangu ya msingi ni mabadiliko hasi katika rneo la uhamasishaji la CHADEMA.

Kipindi cha nyuma walikuwa active kwenye mitandao ya kijamii lakkni kwa sasa hawaonekani.

Kimetokea nini?
 
Katika chaguzi zote ndogo za ubunge zilizowahi kufanyika hapa Tanzania ambapo CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani kimeshiriki, huu uchaguzi mdogo wa ubunge na udiwani katika majimbo ya Kinondoni na Siha unavunja rekodi kwa kukosa hamasa na msisimuko kutoka kwa vijana wa CHADEMA kwenye mitandao ya kijamii na hasa hapa Jamiiforums.

Vijana wa CHADEMA walikuwa wanaongoza kwa kuleta habari mubashara katika mikutano ya kampeni.

Katika kampeni hizi ambazo zinaendelea kwa sasa, tambo zote za habari mubashara hatuzioni tena.

Vijana wa CHADEMA wamekuwa kama wamekata tamaa au wana mgomo baridi.

Wamekata tamaa kwa sabahu wanajua tambo zao kwenye mitandao ni kupoteza muda.

Wana mgomo baridi kwa sababu juhudi zao za kujitoa muhanga hazitambuliwi kivitendo na wenye CHADEMA.

Hata Makene ambaye alikuwa very active kwenye jukwaa letu la siasa kwa sasa haonekani tena.

Ninaamini neno KARAI alilolisema aliyekuwa Mwenyekiti wa baraza la Vijana Chadema (BAVICHA),Patrobas Katambi hakuliokota bali limetokana na mjadala wa vijana wa BAVICHA wanajitolea kufanya kazi ngumu za kukinadi chama na wagombea lakini baada ya uchaguzi hawathaminiwi tena. Kuna wengine kwa sasa wanasota kwenye magereza bila kupata msaada wa kisheria kutoka CHADEMA.

Makene amewapigania kwa nguvu zote makamanda wengi kama vile Lema, Nassari na Sugu wakati wakiwa masikini lakini kwa leo wamekuwa mamilionea na wawekezaji wakubwa katika hoteli za kitalii, maduka ya kifahari na viwanda wakati yeye akiendelea kusugua kwenye viti vilivyoko kwenye kibanda kinachoitwa Ofisi ya CHADEMA Makao Makuu, Ufipa, Kinondoni.

Nafasi zilipotoka za kugombea Ubunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki hakukumbukwa.

Nafasi nyingine imejitokeza ya kugombea Jimbo la Kinondoni, wenye CHADEMA wameenda kuleta mtu ambaye siyo mpiga kura wa Jimbo hilo ili awe mgombea.

Hata ndugu yangu, Mchambuzi wa Jamiiforums baada ya kuwekwa pembeni mwaka 2015 kumpisha Maulid Mtulia wa CUF ninaamini alidhani bahati imekuja tena kwa mlango wa nyuma bila kujua wenye chama wana mtu wao.

Nimeandika hivi kwa sababu aliyetujuza usiku wa manane kuhusu uamuzi wa CHADEMA kuingia tena kwenye uchaguzi mdogo kwa furaha kubwa alikuwa ni yeye kupitia hii thread,
LINK>>>CHADEMA kutia mguu Kinondoni na Siha

Kwa sasa amebaki karai Yericko na propaganda za kitoto. Ninampongeza kwa kazi ngumu yenye mazingira ya "kubadilisha gia" bila taarifa.

Kwa wale wanaifahamu CHADEMA ya wakati wa Dkt. Slaa watakubaliana na mimi kuwa kuna kitu hakiko sawa ndani ya CHADEMA hasa kwenye eneo la uhamasishaji.
Ma CCM yana mawazo ya kijinga kama kama jingalao
 
Kwenye maisha hamuwezi wote kuwa level moja lazima liwepo kundi la wahamasishaji na wahamasishwaji na unapofanya fadhila usingoje shukrani..hata vijana wangu wa UVCCM kinondoni nhuwa nawambia hata mpige mayowe vipi mwisho wa siku inabidi mmpiganie wakuja Mtulia hutaki ondoka CCM.
Baba jesca anawaita ng'ombe waliokatika mikia, mtulia amekatika mkia na bado ameteuliwa kuwa mgombea, yaani yuleyule aliyegombea 2015 amekuja kivingine, sasa sijui ana jipya lipi, maana nilimsikia neno moja, AMECHUMPA, sasa amechumpa ametua kwa mikono au makalio, ngoja tusubiri matokeo
 
19 Reactions
Reply
Back
Top Bottom