Je, Uwezo Wetu wa Kufikiri Umepungua? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, Uwezo Wetu wa Kufikiri Umepungua?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Sep 4, 2012.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Sep 4, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,

  Yanayotokea nchini mwetu yanatutaka sio tu tufikiri, bali, tufikiri kwa bidii. Lakini swali ni hili; Je, uwezo wetu wa kufikiri umepungua?

  Yumkini si kwa aliyekuwa na ujasiri wa kuipiga picha hiyo hapo juu. Alifikiri sana pia. Na si kwa aliyekaa chumba cha habari na kuumiza kichwa, kisha akaamua picha hiyo ipambe sura ya mbele ya gazeti la Mwananchi la juzi. Hapa Iringa gazeti hilo liligombaniwa kama njugu, na bila shaka sehemu nyingine za nchi.

  Naam, siku hizi utasikia ikisemwa; " Tumefika pabaya!" Mwingine atasema; " Tunakokwenda ni kubaya!". Lakini, ni Watanzania wangapi wenye kuuliza maswali haya; " Tumefikaje hapa?" Na " Je, tunaendaje?" Maswali hayo yanamtaka mwanadamu afikiri kwa bidii.

  Wakati mwingine nafikiri, kuwa Watanzania tumechoka kufikiri. Hata kwenye maswali magumu yenye kutuhusu tunataka wengine wafikiri kwa niaba yetu. Unaweza kukutana na Mtanzania mwenzako ukamwuliza; " E bwana ee, unafikiri nini juu ya jambo hili?". Jibu lake; " Kwani wewe unaonaje?"- Ni moja ya maswali yenye kuashiria anaykujibu swali lako amechoka kufikiri.

  Na wakati mwingine tatizo si kutofautiana kifikra, bali kutofautiana namna au jinsi ya kufikiri. Swali moja, lakini unaweza kuona namna tunavyotofautiana katika kuchagua njia ya kulisogelea ( approach) swali husika.

  Na kuna wenye kukimbilia kutafuta njia za mkato. Ndio, majawabu ya mkato. Na baadaye itakuwaje? Inshallah na BwanaYesu Asifiwe!

  Maggid Mjengwa,
  Iringa
   
 2. Rufiji

  Rufiji JF-Expert Member

  #2
  Sep 4, 2012
  Joined: Jun 18, 2006
  Messages: 1,710
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  Maggid,

  Kwanza nikupe pole wewe na wanahabari wote huko Iringa kwa msiba mkubwa uliowapata. Mimi ningependa Bwana Maggid utuelezee kuhusu marehemu Mwangosi kwa kifupi. Kwani nina uhakika ulishawahi kupata nafasi ya kuongea naye au kufanya naye kazi. Pia ningependa utuelezee je unaona ni nani wa kulaumiwa katika kifo hiki? Na jee nini ungependa kifanyike ili janga kama hili lisijirudie tena.

  Natanguliza shukrani.
   
 3. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #3
  Sep 4, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Tumechanganywa Sana na POLITICS za NCHI hii; Wakati Rais Mwinyi alipokuwa anakwenda kusali Kwenye MSIKITI wa kwa

  MTORO (MSIKITI wenye SIASA KALI) Watu walilalama, la ZANZIBAR likapitishwa - UHURU wa DINI na UHURU wa Wafanyakazi

  wa Serikalini hapo hapo UHURU wa Wafanyakazi na CHOMBO kimoja Kilochokuwa kinatuunganisha bila kutubagua JKT likavunjwa

  kwa Manufaa ya kusaidia kwa WINGI wana CCM... Mfano Mtoto wa Mwinyi hakwenda JKT na atakuwa Rais kwa Msaada...

  * Hapo Viwanda Vya Serikali Vikaanza kuunzwa; UONGOZI wa MWINYI UKAPITA

  UONGOZI wa MKAPA yeye ndie aliyesaini MIKATABA UCHWARA na wawekezaji wa MADINI bila hata kuwatoza KODI;

  alihakikisha Hayo Madini Wawekezaji

  Wameyapata kwa CHEE; Wananchi hapo Walikuwa kwenye Ujamaa bado wanachanganywa na CHAMA cha JEMBE na NYUNDO

  wanachokiamini MAISHA yao YOTE

  Kila Kiongozi anaonekana kuwa na MAJUMBA na watoto wao kushiba... RUSHWA ikazidi kukuwa pamoja na MKAPA kujifanya

  MPIGANIA HAKI... UTAWALA wa MKAPA UKAPITA...

  UTAWAKA wa JAKAYA KIKWETE Ulipowadia Uliamsha Shamra Shamra na Furaha lakini MATATIZO yakaanza sababu ya

  MGOGORO uliopelekea Waziri Mkuu kuacha Kazi kuilinda Serikali; lakini Uchaguzi wake wa Mwisho Ukazua UDINI, UKABILA,

  UTAJIRI, UBAGUZI... Sasa kila mtu sasa tunaanza kuogopana hata Marafiki Tunaanza kuwa na Uwalakini kwasababu tunaongea

  lakini deep inside our hearts kuna kitu ambacho hatupatani na tunafichana kwahiyo TUNAKUWA KAMA

  PUNGUANI; WATU WASIOFIKIRIA; HAKUNA RAHA TENA; NI MASUALA MAZITO YAMEWEKWA MEZANI MWETU

  HATUJUI JINSI YA KUYATATUA; RAIS WETU HANA HEKIMA YA KUYAZUNGUMZIA; HANA UPEO HUO; HAKUFAA KUWA

  RAIS HATA KIDOGO... URAIS NI KAZI... SIO MCHEZO... SASA ATAMALIZA MDA WAKE

  NA KUTUACHIA MADUDU ALIYOANZISHA, TANGANYIKA ALIYOICHUKUA NA KUITAWALA HAITAKUWA ILE

  ATAKAYOIACHIA 2015.
   
 4. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #4
  Sep 4, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  maggid, pole kama umegundua leo uwezo wetu wa kufikiri umepungua. Pengine tunatumia vema sehemu ya ubongo yenye kufanya analysisi (Neocortex) lakini ile ya kuwezesha watu kuwa viongozi(Limbic sytem) tuliiua siku nyingi sana. Ndio maana tuna wasomi wasiosoma maana wakianza kukuchambulia mambo utashangaa mtu huyu alisomaje somaje mpaka akapata alichopata. Elimu ya kudesa imetengeneza wafanyakazi kama madesa. Hatuwezi tena kujifunza wala kufikiri zaidi ya pale tulipofikia.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #5
  Sep 4, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 24,967
  Likes Received: 37,523
  Trophy Points: 280
  Mkuu tatizo kubwa la sisi watanzania kuanzia waandishi wa habari,wanaharakati wa haki za binadamu n.k,na umma mzima wa watanzani ni kuwa huwa tuna kitu ninachoweza kukiita" reaction ya nguvu ya soda" hata kwa mambo mazito ambayo yanayohitaji tuwe na msimamo wa pamoja.

  Imekuwa ni tabia ya watanzania kuwa ni watu wa bla bla tu bila vitendo na tusioweza kusimamia kile tunachoamini kinafaa kusimamiwa mpaka majibu yapatikane.Kumbuka tukio la Dr. Ulimboka lilivyovuta hisia za watu na kupelekea kutolewa kwa kauli na matamko mbali mbali lakini mpaka leo imebaki historia tu.Hali kadhalika, tukio hili nalo litapita tu na hakuna cha maana kitakachofanyika licha ya kelele zote zinazopigwa kila kona ya nchi yetu.

  Mwisho niseme hata watawala wa nchi hii wameshagundua udhaifu huu na wanautumia ipasavyo.Hivi sasa wanahesabu siku tu zipite na tukio zima lipite pia.Naamini hawana wasiwasi wowote kwani kelele kama hizi wameshazizoea na sasa wanakuwa na wataendelea kuwa sugu zaidi siku hadi siku.
   
 6. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #6
  Sep 5, 2012
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,898
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Majjid ninakuheshimu na ninakuamini sana katika kusimamia ukweli na haipiti siku bila kutembelea kijijini kwako,lakini kwa suala hili nashauri ninyi waandishi mjipange na kufungua akaunti ili tuwachangie na mtafute wakili wa kueleweka ili wauwaji wa mpiganaji mwenzenu Daudi wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria .Hatuwezi kukaa kimya kwa hili..
   
 7. s

  sanga malua JF-Expert Member

  #7
  Sep 5, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 228
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NITAKUWA WA KWANZA KUCHANGIA.sitachangia harusi yoyote mpaka kwanza nitimize ahadi yangu ya kuichangia familia ya marehemu MWANGOSI.
   
 8. m

  maggid Verified User

  #8
  Sep 5, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndahani,
  Asante sana. Mimi nimeuliza swali na kuchochea mjadala. Naamini michango ya fikra tofauti itatusaidia kufikiri zaidi ya tulipofikia.

  Maggid,
  Iringa.
   
 9. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #9
  Sep 5, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  maggid, lakini hata hivyo, haya yanayoendelea sasa yanatulazimisha kufikiria mara mbili mbili. Sijui kama tutaendelea kuacha kufirkiria mambo kwa mapana.
   
Loading...