Je, uwezo ( umahiri ) wa Walinzi ( Bodyguards ) wa Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu huwa ni sawa au hutofautiana kulingana na Vyeo husika?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,363
108,403
Kwa nchi nyingi tu ( siyo Tanzania ) huwa naona kuanzia Marais wao, Makamu wao wa Rais na Mawaziri Wakuu wao huwa wana 'lundo' la Walinzi ( Bodyguards ) wakiwalinda.

Nikiamini kabisa kuwa hapa JamiiForums kuna Wajuvi ( Pundits ) wa 'Sekta' hii au hata 'Wahusika' wenyewe leo wataweza kunisaidia 'Kunielimisha' Mimi 'Ngumbaru' kwa hili Swali langu.

Je, hawa Walinzi ( Bodyguards ) wa Marais, Makamu wa Rais na Mawaziri Wakuu wa nchi nyingi duniani ( siyo Tanzania ) huwa na uwezo sawa wa Kimedani ( Kimbinu ) au hutofautiana ( huzidiana ) kulingana na 'Vyeo' vya Wahusika?

Nasubiri sana Majibu yenu ili nielimike.
 
Jeshini vyeo hutokana na bahati mkuu,,,,,with that said ingawa vyeo vya chini vinatokana na mapendekezo ya waangalizi wa jeshi ila bahati ndio huwa muamuzi

Mfano kuna askari hawana mbavu hata moja ila wanauwezo mkubwa kimwili na kimapigano kuliko askari wenye vyeo
 
Sitaki tuzungumzie ya Tanzania kwani Mimi siyajui na pia hayanihusu vile vile Mkuu.

Ila nauliza tu Uwezo wa hawa Walinzi ( Bodyguards ) huwa ni sawa au hutofautiana?
 
Kila nchi ina taratibu zake za kulinda viongozi wake hasa wale wa ngazi za juu kutokana na mfumo wa kimamlaka wa nchi husika... swala la kiulinzi wa viongozi kuna kuwa na Agency maalumu ambayo mara nyingi zinakuwa ni kati ya police na Jeshi (imekaa kiraia lakini wanamafunzo ya kiukakamavu ) AGENCY japo kwenye ulinzi wa viongozi vyombo vyote vinashiriki kwa maana ya watu wake, vifaa au vyombo vyake

Mafunzo wote wanakwenda mafunzo ya aina moja si kwamba ukiwa mlinzi wa Rais ww ni bora kuliko mlinzi wa makamu wa rais au waziri mkuu pale atafutwi Rambo au Arnold Schwarzenegger kwa maana ulinzi ni (coordination), ushirikiano wa watu wengi na unaongozwa na mfumo maalumu si jitiada za mtu binafsi.
 
Ahsante kwa Ufafanuzi mwana Medani.
 
Jeshini vyeo hutokana na bahati mkuu,,,,,with that said ingawa vyeo vya chini vinatokana na mapendekezo ya waangalizi wa jeshi ila bahati ndio huwa muamuzi

Mfano kuna askari hawana mbavu hata moja ila wanauwezo mkubwa kimwili na kimapigano kuliko askari wenye vyeo
Hujaelewa swali rudia tena
 
Vyeo jeshini hutokana na elimu, aina ya mafunzo aliyojifunza, huwezi kutunukiwa cheo/rank from nowhere ukawa kanali wa jeshi. Ikitokea ukatunukiwa tu labda umefanya tukio la kipekee.
Cheo/rank jeshini husomewa
 
Mtu mwenye cheo cha Kanali hawezi kufanywa bodyguard

Bodyguard ni askari ambao ni hawajasoma, na nao pia wanavyeo vyao huko chini
 
Back
Top Bottom