Je, Uwekezaji wa Vietnam Katika Korosho Mkoani Mtwara una tija kwa Taifa letu?

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
34,669
40,917
Inafahamika kwamba Vietnam ndiye mnunuzi mkubwa wa Korosho hapa nchini na muuzaji mkubwa wa zao hilo katika nchi za ulaya na Marekani.

Katika mwaka 2019 alifanya biashara ya korosho yenye kiasi cha thamani ya Bilioni 3 za Kimarekani ( sawa na Shilingi Trilioni sita za Kitanzania)

Katika siku za hivi karibuni , Balozi wa Vietnam hapa nchini alifanya ziara ya kimkakati mkoani mtwara kuangalia fursa za wafanyabiashara toka taifa hilo mkoani humo.

Moja kati ya mambo yaliyoteka hisia za wengi ni dhamira yao ya kujenga kiwanda cha kuongeza thamani ya zao hilo hapa nchini.

Kinachofanyika ni kuongeza thamani ya zao tu na sio kutengeneza final product kama ile inayotengenezwa nchini mwao na kuisamabaza katika nchi za Ulaya na marekani.

Kinachoonekana hapa ni kuwa mnunuzi mkuu, amekuja hapa kulilinda soko lake la korosho kwa kuhakikisha kwamba yeye anamabia mnunuzi mkuu na muuzaji mkuu bila ushindani toka kwa mwingine.

Swali langu ni kuwa kama kweli Vietnam wanataka kuisaidia Tanzania kwanini wasijenge kiwanda kitachotengeneza final product kama za kule kwao Vietnam.

Ni jambo gani linaizuia serikali kujenga kiwanda huko mtwara na kuiuza korosho hiyo katika masoko ya Ulaya na Marekani.

Kuna faida gani ya kukubali uwekezaji wa Vietnam ambaye ananunua ili akauze kwingine kwa faida ya juu.



 
Hiyo ndio win win, unataka wajenge kiwanda cha final products raia wao kule utawapa ajira wewe maana viwanda vitafungwa kule.
 
Jiwe alisema atajenga viwanda hapa hapa Tz, mwisho wa siku akawadhulumu wakulima korosho zao, kiwanda hakikujengwa na korosho ikamshikisha ajabu.
 
Inafahamika kwamba Vietnam ndiye mnunuzi mkubwa wa Korosho hapa nchini na muuzaji mkubwa wa zao hilo katika nchi za ulaya na marekani...
Shukuru walau kwa hii hatua. Mwendazake hakuweza hata kujenga kiwanda kimoja zaidi ya kuwatia hasara wamakonde wakulima wa korosho
 
Jiwe alisema atajenga viwanda hapa hapa Tz, mwisho wa siku akawadhulumu wakulima korosho zao, kiwanda hakikujengwa na korosho ikamshikisha ajabu.
Mwalimu alijenga viwanda vikubwa vya korosho zaidi ya sita kutoka Japan na Italy.

Nakumbuka ajira ilikuwa sio tatizo kwa mikoa ya Lindi,Mtwara,Pwani.Vijana wengi walipata ajira.

Sasa hatuna hata kiwanda kimmoja sana sana tuna viwanda vidogo vidogo .
 
Jiwe alisema atajenga viwanda hapa hapa Tz, mwisho wa siku akawadhulumu wakulima korosho zao, kiwanda hakikujengwa na korosho ikamshikisha ajabu.
Hivi kwanini fedha tunazotumia kununua ndege zisibadilishiwe matumizi na kuwekezwa kwenye sekta ya korosho ili tuweze kuuza final product huko nje?

Zao la korosho lilihujumiwa mara ya kwanza wakati wa operation vijiji vya ujamaa. Lilipokuja kufufuliwa kabla sekta haijakaa vizuri Magufuli akafanya mambo yake.
 
Shukuru walau kwa hii hatua. Mwendazake hakuweza hata kujenga kiwanda kimoja zaidi ya kuwatia hasara wamakonde wakulima wa korosho
Watu wanasahau kua serikali ilishaingia kwenye uwekezaji wa viwanda vikafa. Mwaka 2018 serikali iliingia kichwa kichwa kwenye kufufua kiwanda cha korosho kilichowashinda wawekezaji Lindi kilichotokea Mungu ndo anajua.
 
Back
Top Bottom