Je, Utumbuaji/Teuzi/Tenguzi zinazoendelea kote nchini ndani ya Serikali kunatoa picha gani?

Mtamba wa Panya

JF-Expert Member
Aug 6, 2017
695
1,712
Habari,

Naomba tujadili hii mada kwa kuongozwa na akili zetu wenyewe bila kuweka ushabiki wa kisiasa mbele. Je, hili suala la Utumbuaji/Teuzi/Tenguzi serikalini kila leo katika serikali ya awamu ya tano kunaleta picha gani?

Je, waTanzania wengi hata waliosoma (cc PhD zilizotumbuliwa) hawana weledi na hizo nafasi ?

na/au

Je, waTanzania wengi ni wabinafsi/mafisadi wakipewa nyadhifa?

na/au

Je, 'Dereva' ndiye mwenye 'matatizo'?

na/au

Je, watu kutoka Chama tawala (wanaCCM) ni hovyo?? (cc Wapinzani walioteuliwa, je, kuna aliyetumbuliwa??)

na/au

Je, waTanzania tu kiujumla si wachapakazi?

na/au


Je, 'upigaji' ndio utamaduni wetu?

Tatizo ni nini hasa kwa mtazamo wako??


Kumbuka: Kugundua tatizo ni mwanzo wa kupata suluhisho la tatizo hilo.
 
Back
Top Bottom