Je, utofauti wa voltage kati ya nchi moja na nyingine unaweza kuathiri kifaa cha umeme?

RJ45

JF-Expert Member
May 20, 2014
337
113
salaam wakuu

kwa wataalamu wa umeme naomba mnisaidie hili: kama tunavyofahamu umeme wetu wa majumbani kwa hapa tanzania ni kati ya 220v-250v (sina takwimu sahihi mtanisaidia) lakini kuna mashine inayotumia umeme nimeagiza nje na wameelekeza umeme unaotakiwa ni 120v, hata hivyo nimeunganisha kwa umeme wa hapa imekubali kufanya kazi lakini nauliza hii haiwezi kuwa tatizo ikapelekea labda hii mashine kuungua?
 
kwanza una bahati sana lkn bado uko katika hatari ya kuua machine, mbona kuna transformer nyingi tu zenye input ya 220 na output ya 110?
 
kwanza una bahati sana lkn bado uko katika hatari ya kuua machine, mbona kuna transformer nyingi tu zenye input ya 220 na output ya 110?
na je, hyo transiformer ya 110v nkichomeka device ya 120v sio tatizo?
 
Hiyo mashine inatumia powersupry sio transformer ingejuwa transformer sasa hv hapa ungeongea mengne
Fanya mpango upate transforma itakayonyambulisha umeme toka 220 kuja 120 kabla capacitor hazijafumuka hizo ukaua mashine hiyo
Ikiwezekana usitumie mashine mpk upate transformer
Tena nzuri ni za kusuka ni bora na ghalama nafuu zaudi
 
Jua kifaa chako kinatumia power kiasi gani, halafu tafuta hiyo transformer kubwa kidogo zaidi ya hicho kifaa chako.
Jambo la pili mara nyingi 110V, frequency zake ni 60Hz, na za 220V ni 50Hz angalia hilo pia, hususan kama kifaa chako kina motor

asante kwa ushauri mkuu
 
ni photocopy mashine specification zake ni 120V, 60Hz na 7.5A
 
Mkuu hao KVD bei zao hatari faya fanya kama nilivyokushauri km ni mwezangu na mm
Ila km upo vizuri nenda bidhaa zao nzuri hukosi kitu ila bei zao hawajambo
hiyo ya kusuka napata wapi mkuu
 
hiyo ya kusuka napata wapi mkuu
Upo DSM kama upo DAR natengezeshaga kwa jamaa mmoja yupo VINGUNGUTI huwa anasuka mitambo ya viwandani sasa anakaofisi kake VINGUNGUTI jioni nikipita nitachukua namba yake nitakutumia mkuu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom