Idugunde
JF-Expert Member
- May 21, 2020
- 6,273
- 6,637
Miaka karibu yote tangu kuanza kwa vyama vingi Chadema na vyama vingine vya upinzani wamekuwa wakishiriki uchaguzi na wamekuwa wakipata ushindi kwa ngazi mbali mbali kama vile ubunge na udiwani.
Lakini sio siri walikuwa wanakichachafya CCM kwenye kampeni hasa kwa kutumia madhaifu ya kutopambana ufisadi na ubadhirifu.
Natolea mfano tu Uchaguzi wa 2010 Chadema pamoja na kutokuwa na washirika wa Ukawa waliitikisa CCM hasa ikuchukuliwa maanani ajenda ya ufisadi iliwabeba sana. Walipata madiwani wengi na karibu miji mikubwa kama Mwanza, Mbeya na Arusha walivuna madiwani wengi na wabunge. Je, baada ya uchaguzi wa 2010 hawakubaini kuwa tume sio huru?
Kwa mujibu wa katiba ya JMT ibara ya 74(7) tume ya uchaguzi ni chombo huru ambacho kinatakiwa kifanye kazi kwa mujibu wa katiba na sheria.
Baada ya uchaguzi wa 2015 na JPM kuwa Rais mambo yamebadilika. Natoa mfano tu, ufisadi na ubadhirifu umedhibitiwa. Na kwa sababu hii serikali imetekeleza miradi mingi yenye tija kwa taifa kwa muda mfupi. Sioni umuhimu wa kuitaja kila mwanachama wa Chadema na mpinzani anaifahamu.
Kwa mantiki hiyo wapinzani wamekosa ajenda ya kuikosoa serikali ni hii dhahiri hawawezi kushinda urais na hata ubunge na udiwani ni kwa nadra sana.
Sasa wao wanadai eti tume ya uchaguzi sio huru. Kwa nini madai haya hawayakuyaleta toka hata 2010? Au ni kwa sababu CCM chini ya JPM imewakaba kila kona na hawapumui, kwa utendaji kazi mzuri na unaokubalika.