Uchaguzi 2020 Je, utampa Magufuli kura yako uchaguzi ujao?

Yani serious watu kabisa mnapanga mstari kupiga kura? Kwa Tume Gani?

Kujiandikisha kwenyewe wala sijajiandikisha. Mshindi anajulikana.
 
Toka Uhuru ndio mnapata hizo huduma karibuni.poleni sana CCM imewatesa sana .kijijini kwetu zipo toka miaka 1970s na kwa 20yrs CCM haipo hapa
Mimi mke wangu chadema damu, anasema safari hii ni T2020 JPM, kijijini kwao kwenda ni mkeka tu na maji na umeme umefika sasa. Humuelezi kitu sasa hivi, hivyo hakijaaribika kitu. Wanapisha barabarani wako anaenda huku wangu anaenda huku.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani Janga la Dunia la CORONA ambalo limewashinda hata Marais wanaosifika Duniani ndiyo leo hii lifanye Rais Dkt. Magufuli hafai? Sasa naanza Kuamini kuwa Great Thinkers wameshapungua nchini Tanzania.

..ni kwasababu mlisema Magufuli ni sawa na Nabii Musa.

..lakini ktk kupambana na corona amekuwa kama Idi Amin ambaye alikimbia vita Kampala akaenda kujificha kijijini kwao Koboko.

..huyu amevuruga uchumi, amebomoa misingi umoja wa waTz, ameleta chuki na uhasama ktk siasa zetu, chini ya uongozi wake ukabila umechomoza waziwazi. heshima ya nchi kimataifa imeporomoka.

..kwa kifupi Magufuli ame-prove kuwa ni failure na hafai kupewa kipindi kingine cha miaka 5.
 
Mimi mke wangu chadema damu, anasema safari hii ni T2020 JPM, kijijini kwao kwenda ni mkeka tu na maji na umeme umefika sasa. Humuelezi kitu sasa hivi, hivyo hakijaaribika kitu. Wanapisha barabarani wako anaenda huku wangu anaenda huku.
Anajua lakini kuwa kakimbia mjini kujificha kijijini mwezi sasa ili asiongoze mapambano ya koona? Eti ujemedari kampa Dada Ummy?
Hakuna cha "Mimi ni jiwe kweli kweli!" na nimeamini hakuna mkate mgumu mbele ya chai. Mwambie mkeo huyo ni mdebwedo tuu
 
Kwa mbali nakumbuka ile siku nduli Idi Amin alipotushambulia na kuteka sehemu ya Jamhuri yetu huku akitishia kuongeza mashambulizi hadi Bandari yetu ya Salama. Jemadari wetu Mkuu wakati huo, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere hakutafuta pa kukimbilia kujificha na kututaka tusali, hapana.

Baada ya kutangaza tu kwamba tuko vitani, aliingia kazini kuwahamasisha wananchi na kuliongoza Jeshi la wananchi, JWTZ, kwa kazi moja tu, kumpiga adui. Na kweli nduli alitandikwa. Alipigwa hadi akaikimbia si tu ardhi yetu na mambo yakaishia hapo, hapana, alizidi kutandikwa hadi akaikimbia na nchi yake Uganda.

Naam, hivyo ndivyo ilivyo, Kamanda na Jemadari Mkuu hakimbii uwanja wa vita akawaacha askari wake mikononi mwa wahuni kama Bashite.

vita vya uganda.jpg

Rais wa awamu ya kwanza wa Tanzania, Mwl. J.K Nyerere na makamanda wa Jeshi.

vita+pic.jpg

Hapa Kamanda wa kweli na Jemadari Mkuu, Mwalimu Nyerere, yupo juu ya tanki la jeshi, kifaru, uwanja wa vita!
Tukumbuke tunapomchagua Rais, tunamchagua Kamanda na Jemadari Mkuu ambaye atakuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya adui anayeonekana na asiyeonekana na si anayejificha mapambano yakipamba moto...ni hayo tu!
 
..ni kwasababu mlisema Magufuli ni sawa na Nabii Musa.

..lakini ktk kupambana na corona amekuwa kama Idi Amin ambaye alikimbia vita Kampala akaenda kujificha kijijini kwao Koboko.

..huyu amevuruga uchumi, amebomoa misingi umoja wa waTz, ameleta chuki na uhasama ktk siasa zetu, chini ya uongozi wake ukabila umechomoza waziwazi. heshima ya nchi kimataifa imeporomoka.

..kwa kifupi Magufuli ame-prove kuwa ni failure na hafai kupewa kipindi kingine cha miaka 5.

Asante kwa Maoni yako ambayo hayaakisi Maoni ya Watanzania wote.
 
John Pombe Joseph Magufuli---YES
Sijawahi kujutia kumpigia kura mwaka 2015.
Ndimi mtumishi mtarajiwa wa serikali kura yangu 2020 ni kwa Magufuli.
 
Habari za mda huu.
Corona ni hatari kufata taratibu zilizoweka na wizara ya afya kujilinda na kuwalinda tuwapendao.

Niende kwenye mada chap chap.
Kumpa kura yangu ni Big No!

Vipi wewe ndugu yangu utampa kura yako??

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijampa kura yangu wakati ule kwa sababu niliona udhaifu wake mapema safari hii hata akigombea udiwani kura yangu hapati kwa sababu amethibitisha bila shaka yoyote kuwa angefaa abaki kuchunga mifugo tu labda ndo ataweza. Miaka mingine mitano itakuwa janga kuliko Covid-19!
 
Back
Top Bottom