Je, Utajuaje kuwa huyo ndiye mkeo? Mjue mkeo

ROBERT HERIEL

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
2,757
2,000
JE, UTAMJUAJE HUYO NDIYE MKEO?
MJUE MKEO.

Kwa Mkono wa, Robert Heriel

Sasa nimejihangaisha na mambo haya, wala hakuna lolote nitakalo lipata, lakini nafsi yangu itafurahi ikiwa tuu nitaimaliza kazi hii. Haya sasa, mnisikie;

Uzuri wa dunia umejificha, nayo nuru imo gizani hata waitafutao hawaoini. Macho yao wameyafumba hata wasione. Lakini wao husea tunaona, kwa vile walilala na malaya wa njia kuu, huyo aliyepofusha macho yao, kwa sauti yake laini, na penzi la ulaghai.

Niite Taikon wa Fasihi, Mfungwa wa penzi la kahaba.

Jumbe hii isomwe na vijana werevu na wenye hekima, wasome aya kwa aya nao waelewe, lakini vijana wapumbavu wasielewe kitu, bali wabaki katika njia panda za akili zao.

Huwezi kumjua mke wako kama hujifahamu,
Huwezi kumtafuta mkeo kama hujajitafuta,

Kabla hujaanza kutafuta mke wa kumuoa basi anza kujitafuta kwanza, kabla hujaanza kumchunguza mke wa kumuoa basi anza kujichunguza kwanza.

Kabla hujataka kumuelewa mke wa kumuoa nakusihi taka kujieewa wewe mwenyewe.

Mke ni kama kivuli chako, yaani ni taswira yako wewe mwenyewe. Yaani Mke ni wewe mwenyewe.
Hii ni kusema, mtu hawezi kutafuta kivuli chake mwenyewe, labda awe mwendawazimu.

Mke ni mfano wako, nimeshasema ni kivuli chako.

Kivuli ni wewe, ila wewe sio kivuli. Mke ni wewe, ila wewe sio mke. Mke ni mfano wako wewe. Hivyo unapoanza kutafuta mke anza kujitafuta mwenyewe.

Mwanamke hachunguziki kwa sababu kumchunguza mwanamke uliyemuoa ni kujichunguza wewe mwenyewe.
Hakuna mtu awezaye kujichunguza, hii ni kusema hakuna mwanaumme awezaye kumchunguza mke wake, kwani jinsi mume alivyo ndivyo mke alivyo.

Hakuna mwanaume timamu awezaye kuoa wake zaidi ya mmoja. Ni wanaume dhaifu peke yao ndio huweza kuoa wake wawili au zaidi. Ninaposema dhaifu namaanisha wanaume wenye kasoro au madhaifu ya kihisia, kimwili na kiakili ndio huweza kuoa wake wawili.
Mke ni mmoja kama alivyo mume mmoja.

Ninafahamu kasoro nyingi za maumbile, kama kuzidi viungo, nimeshawahi kuona watu wenye mikono minne, pia nimeshawi kuona watu wenye vidole sita au saba kabisa. Hakuna aliyewahi kujivunia jambo mambo hayo, kwani huo tunaita ulemavu.

Hii ni kusema hata wenye tamaa ya kuoa wake zaidi ya mmoja ni kundi la walemavu bila kujali nafasi ya watu hao, iwe kwa cheo, umri, hadhi na hata nafasi yake kijamii na kidini.

Mlemavu ni mlemavu, sio jina zuri lakini hatuna budi kulitaja ikiwa tunataka kujifunza.

UTAJAUJE HUYO NI MKEO?

Je, utajua kwa sababu anasura nzuri?
Je, utajua kwa sababu ana matako makubwa yanayokuvutia?
Je, utajua kwa sababu ana sauti nzuri ya kukuamsha hisia?
Je, Utajua kwa sababu anamali?
Je, utajua kwa sababu anatabia njema?
Je, utajua kwa sababu ni mchapakazi?

Je utajuaje kuwa uliyemuona ndiye mkeo au uliyenaye ndiye mkeo?

Imeandikwa, Mke mwema hutoka kwa Bwana, pia imeandikwa, je mke mwema ni nani awezaye kumjua?

Anyway, Wahenga wanasema Mke mwema anatoka kwa Bwana, kumaanisha mke wako ambaye ni mwema yuko kwa Bwana naam Ndiye Mungu aliyekuumba.

Sasa lazima tuelewane hapa, Mke mwema haombwi, kama vile wewe ulivyokuja duniani bila kujiomba mwenyewe uje, ndivyo mkeo wako alivyokuja na yupo.

Kuna mambo ya kuyahangaikia ili uyapate lakini sio mke mwema. Mke mwema ni kama zawadi kutoka kwa Bwana, haihitaji usote, ufunge na kuomba, au ukeshe kwa kulia. Mke wako yupo hapo hapo sema wewe hujamtambua.

Mke mwema huja pale mwanaume anapokuwa amechoka, hana msaada, hana msaidizi, hana kampani, anakiu, pale ambapo utakapojihisi u pekeako, yaani dunia imekutenga, hakuna anayekutaka tena, hakuna anayeona thamani yako, ukifikia hatua hiyo basi tambua upo katika mazingira ya kupata mke mwema.

Lakini ukijiona hauhitaji msaidizi, bado unakampani, bado watu hawajakutenga, bado unathamani na watu wana kuthamini, bsi tambua bado hauna haja ya kuwa na mke mwema.

Mtu hutaka mke pale anapojiona yupo mpweke, anahitaji kampani, anahitaji msaidizi wake, anahitaji kivuli chake.

Sasa ushakuwa unauhitaji w mke, utajuaje huyo ndiye mke wangu?

Kumbuka, Mungu hajawahi kumuambia mtu yeyote huyu ni mke wako. Hata Adamu licha ya kuwa alikuwa pekeake, lakini Mungu alipomletea Hawa hakumtambulisha kuwa huyu ndiye mke wako.
Kumaanisha, kwenye hii dunia hakuna mwenye jukumu la kukuambia kuwa huyo ni mke wako, jukumu hilo ni lako wewe mwenyewe.

Adamu alipomuona tuu Hawa, akajua ni nyama katika nyama zake, mifupa katika mifupa yake, Huyo ndiye mke wake naam Hawa.

Adamu hakutarajia kuwa ataletewa Mke, wala hakuwahi kufikiri kuwa siku moja atakuwa na kitu kinaitwa mke.
Yaani hakufanya imagination, kwamba mke wangu atakuwa hivi au vile, mnene au mwembamba, mrefu au mfupi, mweupe au mweusi. Hakuwa kufikiri hayo. Ila yeye alikuwa tuu mpweke, asijue upweke ule ulisababishwa na ninn.

Vijana wa sasa wengi tunafanya imagination ya wake zetu, tunawaumba wake zetu kwenye bongo zetu. Utasikia kijana akitaja sifa za mke atakayemuoa;
1. Awe mzuri kama Malaika wa mbingu ya saba
2. Umbo namba nane, nyumba ni choo
3. Sauti ya kumtoa nyoka pangoni
4. Akiwaa na rangi ya Mtume hewala
5. Asiwe kifupi nyundo awe saizi ya kati, tobaa!

Hivyo kijana apitapo mtaani, macho yake yote huyakita kwa aina hizo za wanawake. Kimwanamke chembaba kikijileta anakuwa kama hakioni. Hahaha! Hapo ndipo tunapokosea.

Unapofanya imagination ya mke utakayemuoa tayari unajiingiza kwenye mtego wa kutokupata mke wako halisi.

Ukweli usio na shaka ni kuwa waliopo kwenye ndoa, wengi 90% wanakiri kuwa hawakuwahi kufikiri kwamba angeoana na mwanaume au mwanamke kama aliyenaye. Unakuta mtu alitamani aoe mke mweupe, lakini utashangaa kaoa maji ya kunde au mweusi.

Utajuaje kwamba huyo ni mkeo?

Ili ujue huyo ni mkeo, kwanza acha kufanya imagination, futa imagination zako zote kwanza, kisha endelea na maisha yako. Utakutana na kujua huyo ndiye mkeo au laa.

Kwanza utajua mnafanana mambo mengi sana zaidi ya asilimi 80%
Mbili jina utakalo mpa atalikubali, kumaanisha wewe ndiye mmiliki wake.
Tatu, Makosa atakayo yafanya yatatokana na tabia zako
Nne, Mambo anayoyapenda yatatokana na tabia zako za ndani zilizojificha.
Tano, Atakuwa msaada wako mkubwa kuliko mtu yeyote hapa duniani.

Kuna msemo watu wanasema hakuna kama Mama, msemo huu ni matokeo ya wanaume waliokosa wake wema.
Ukiona nawe au mimi tunaamini hakuna kama Mama basi tambua hatujapata wake wema, yaani mke wako, nyama katika nyama zako, mifupa katika mifupa yako.

Mithali 31: 1- 3
Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana thamani yake yapita thamani ya marijani. Moyo wa mumewe humwamini, Wala hatakosa kupata mapato. Humtendea mema wala si mabaya, Siku zote za maisha yake. Hutafuta sufu na kitani; Hufanya kazi yake kwa moyo wote. Afanana na merikebu za biashara; Huleta chakula chake kutoka mbali. Tena huamka, kabla usiku haujaisha; Huwapa watu wa nyumbani mwake chakula; Na wajakazi wake sehemu zao"

Utajua huyo ni mke wako ikiwa atakuwa msaidizi wako na wala sio mwangamizi wako.
Mke wako atakusaidia kufikia ndoto zako, atakusaidia kupata mali, atakusaidia kujenga heshima yako ndani ya jamii, atakulinda na kukuficha panapotakiwa.

Mke ni msaidizi wako, anakusaidia kufanikisha mambo yako, na sio yake.
Haupo kwa ajili yake ila yeye ndiye yupo kwa ajili yako.

Ukiona mwanamke badala ya kukusaidia kukufanikisha yeye ndiye anakusaidia kuwa masikini, kwa kukupiga vizinga visivyo na mbele wala nyuma, jua huyo sio mkeo.
Ikiwa anakusaidia kufilisi biashara yako, badala ya kuikuza, yeye kazi kudai pesa tuu na kuziharibu kwa mambo ya starehe, jua huyo sio mkeo.

Ukiona Mwanamke uliyenaye anataka wewe ndiye umsaidie badala ya yeye akusaidie, Jua huyo sio mkeo.

Ukiona upo na mwanamke ambaye pesa yake ni yake, na yako ni yenu, basi jua yakuwa huyo sio Mke wako, kama unaweza fukuza, kama hujiamini muache.

Ukiona mwanamke anakulaumu zaidi badala ya kukupa moyo, jua anakulinganisha na mume wake ambaye sio wewe ambaye umemuoa. Huyo sio mke wako.

Ukiona mwanamke, anapenda kutaja kwao licha ya kuwa umemuoa, asijue kuwa hana kwao isipokuwa hapo kwako, basi jua huyo sio Mkeo.

Ukiona mwanamke ambaye yupo tayari kukupoteza kwa urahisi na kumuachia mwanamke mwengine, basi jua huyo sio mkeo.
Mke aliyetoka kwa Mungu kamwe hawezi ruhusu mwanamke mwingine amtoe ndani ya Nyumba.

Mke wako utamjua tuu, ikiwa atakuwa ni msaada mkubwa kwako kuliko mtu yeyote yule chini ya jua. Hapo utasema, huyu ni mifupa katika mifupa yangu, nyama katika nyama zangu.

Lakini kama mwanamke uliyenaye(sithubutu kumuita mkeo) kuna mtu anamzidi kwa kukupa msaada basi jua kuwa amekosa sifa za kuwa mke wako.

Mke wako ni wewe mwenyewe, vile ulivyo ndivyo alivyo, unayoyapenda ndiyo ayapendayo.
Unachokifanya chochote kile lazima naye akipende, lazima ajivunie wewe. Lazima ajitahidi kwa hali na mali kufanikisha kusudi lako la kuwapo duniani.

Hawana wanawake wa siku hizi wanaokuambia bila kumhudumia ati huwapendi, sio kweli, hakuna mke hapo.

Badala ya kuoa msaidizi wa maisha yako(mkeo) unaoa muangamizi wa maisha yako.
Mwanaume ameumbwa kutafuta kwa jasho, amenyeke kwenye utafutaji lakini sio atolewe jasho na wanawake majizi na mavivu.

Mkeo kamwe hawezi kuwa mvivu, lazima awe na sifa za usaidizi kikamilifu.

Ukioa mke mwema jamii yote itakuambia kuwa umeoa mke mwema, kwani wataona matunda ya mke wako.

Ushaambiwa kila kwenye mwanaume mwenye mafanikio basi jua yupo mwanamke imara nyuma yake.

Lakini kila kwenye mwanaume aliyeanguka jua pia yupo mwanamke nyuma yake.

Jamii yenye wanawake wavivu, huwa masikini sana,
matoto huwa mavivu, nyumba chafu, watoto lazima walale njaa.
Jamii yenye wanawake tegemezi lazima iwe masikini.

Mwanamke asipokuwa msaada kwako, basi huyo ni anguko lako.
Msaada sio kupewa tendo la ndoa pekee yake, bali kuwa mke halisi sio hawa wake matapeli.

Usiniulize kwa nini utakufa mapema, ikiwa hautaoa mke wako.

Niishie hapa kwa leo, mwenye swali aweza kuuliza.

Ulikuwa nami;
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa, Dar es salaam
 
MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
17,410
2,000
Duniani hakuna kitu kiitwacho "Soul Mate" , wanadamu huchagua wenyewe.
Pili, hata huo mfano wa Adam kuletewa Hawa nadhani nao hujauangalia vizuri.

Biblia ya Kihebrania inasema Mungu alimuumba Hawa akampitisha mbele ya Adamu,
Katika lugha ya Kiingereza neno hilo linatafsiriwa hivi "Paraded her", haijasema kwamba Adamu alichaguliwa mke.
Adamu mwenyewe baada ya kuona Hawa ni bonge la toto akajiongeza na kuanza kusema wewe ni mfupa wangu.

Kwenye kitabu cha Samweli, baada ya Daudi kumuua Uria aliambiwa na Mungu kwamba, nilikupa mali, ufalme hadi wake za Bwana wako Sauli, na ungetaka na wengine ningekuongezea. Sasa wewe mzee wa fasihi unapotuambia kwamba kuoa mke zaidi ya mmoja ni udhaifu unamaanisha nini ???
 
Jibu ni moja, Daudi na genge lake alikuwa mdhaifu, mlemavu hasa wa kihisia,

Yeye alishindwa kuzuia tamaa yake ya ngono, Daudi na wenzake wote bila kujali nafasi zao walikuwa na ulemavu wa kihisia.

Pia sijasema kuwa Adamu alichaguliwa Mke, ila kwa muktadha kila mtu anaweza kusema hivyo kwa sababu hakuletewa wanawake wengi achague,

Kama ilivyo Mama ni mmoja Baba ni mmoja, Mungu ni mmoja, basi kaa utambue hata mke uliyeumbiwa naye ni Mmoja. Hiyo ukubali ukatae.

Mungu ni Mmoja lakini ipo miungu ingine watu wamejifanyia
Mama ni mmoja ila watu huweza kujifanyia mama wengi
Baba ni mmoja ila watu huweza kujifanyia wababa wengi
Mke ni mmoja ila watu huweza kujifanyia wake wengi,

Suala la Soul mate umezungumza vyema,
 
Sosoma Jr

JF-Expert Member
Aug 7, 2020
250
250
Daah haya ngoja tuwaone wahenga!! Siti yangu ya mbele natazama kila jambo kwa jicho la tatu!!
Tukaze mwendo safari ni ndefu kwanza tumeianza hakuna mzoefu wote tuu wanafunzi!!!!?
 
Proved

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
11,280
2,000
Dah!...somo gumu sana kwa kweli, mabachelor tuna mtihani sana...

Sasa utasubiri mpaka lini uje ukutane na huyo 'mke mwema' bila wewe mwenyewe kujiongeza?, Je atakuja peke yake?

Kumbuka muda unaenda huwezi kukaa unasubiri tu.
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
6,560
2,000
Simply tabia za mume ndio anatakiwa awe nazo mke au mtofautiane kidogo sana ili muweze kuishi pamoja kwa amani, hii itasababisha iwe rahisi kuvumiliana pale ambapo patatokea misunderstanding kati yenu, kwasababu kosa la mmoja litakuwa ndani ya uwezo wa mwingine kulivumilia.

Lakini, kinyume na hapo hakuna mume wala mke kwasababu kosa la mmoja wapo litakuwa gumu sana kusamehewa na kusahaulika na mwingine kama nature ya kosa hilo haiendani kabisa na tabia za aliekosewa, hili litasababisha doa kwenye uhusiano, na baada ya doa kinachofuata ni kutoaminiana, na malalamiko kila wakati, ladha ya nyumba inapotea, mwishowe kuachana.

Au kwa wale wanaojilazimisha kuvumilia, huendelea kuvumilia hali hii ambapo mwishowe huathirika kisaikolojia na wengi wao huishia kufanya baya lolote ikiwemo kujiua wao binafsi, au kuwadhuru watoto, au kumdhuru mwenzi wake, hapa ndipo tunasikia matukio kama mama kawapa sumu watoto kumbe chanzo cha hayo ni tabia za baba na mama akajilazimisha kuvumilia.
 
Naantombe Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
4,421
2,000
Taikon wa fasihi.. humu kuna watu wana karama kubwa sana ya uandishi.. wewe ni mmoja wapo..

Mwingine ni jamaa anaitwa kalamu
 
ROBERT HERIEL

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
2,757
2,000
Simply tabia za mume ndio anatakiwa awe nazo mke au mtofautiane kidogo sana ili muweze kuishi pamoja kwa amani, hii itasababisha iwe rahisi kuvumiliana pale ambapo patatokea misunderstanding kati yenu, kwasababu kosa la mmoja litakuwa ndani ya uwezo wa mwingine kulivumilia.

Lakini kinyume na hapo hakuna mume wala mke kwasababu kosa la mmoja wapo litakuwa gumu sana kusamehewa na kusahaulika na mwingine kama nature ya kosa hilo haiendani kabisa na tabia za aliekosewa, hili litasababisha doa kwenye uhusiano, na baada ya doa kinachofuata kutoaminiana, na malalamiko kila wakati, ladha ya nyumba inapotea, mwishowe kuachana.

Mkuu shikamoo, wewe umenielewa,

Yaani kama Mume ni mlevi lazima apate mke atakayemsaidia kuwa chapombe kabisa :D :D :D
 
ROBERT HERIEL

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
2,757
2,000
Dah!...somo gumu sana kwa kweli, mabachelor tuna mtihani sana...

Sasa utasubiri mpaka lini uje ukutane na huyo 'mke mwema' bila wewe mwenyewe kujiongeza?, Je atakuja peke yake?

Kumbuka muda unaenda huwezi kukaa unasubiri tu.

Siku ukiwa na uhitaji na mke utampata,
sio tamaa ya papuchi lakini;););)
 
King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
41,894
2,000
Ni kweli Mkuu ,Mke ndio wewe mwenyewe maana Mungu alisema nitakupa wa kufanana naye yaani PIPA NA MFUNIKO.
 
Kijana wa jana

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
11,014
2,000
Duniani hakuna kitu kiitwacho "Soul Mate" , wanadamu huchagua wenyewe.
Pili, hata huo mfano wa Adam kuletewa Hawa nadhani nao hujauangalia vizuri.

Biblia ya Kihebrania inasema Mungu alimuumba Hawa akampitisha mbele ya Adamu,
Katika lugha ya Kiingereza neno hilo linatafsiriwa hivi "Paraded her", haijasema kwamba Adamu alichaguliwa mke.
Adamu mwenyewe baada ya kuona Hawa ni bonge la toto akajiongeza na kuanza kusema wewe ni mfupa wangu.

Kwenye kitabu cha Samweli, baada ya Daudi kumuua Uria aliambiwa na Mungu kwamba, nilikupa mali, ufalme hadi wake za Bwana wako Sauli, na ungetaka na wengine ningekuongezea. Sasa wewe mzee wa fasihi unapotuambia kwamba kuoa mke zaidi ya mmoja ni udhaifu unamaanisha nini ???
Umemaliza kila kitu mkuu
 
Mungu akikuletea wanawake maana yake atakupa na namna ya kuwa handle, ndio maana akasema mwanamke ishi nae kwa akili, na namna moja ya kum-handle mwanamke lazima mfanane tabia, kinyume na hapo ni kujiumiza tu kisaikolojia.

Kinyume na hapo naamini hata pendezo la Mungu kwa mwanaume ni kuwa na mke mmoja, ndio maana biblia inasema mwanamke ataachana na babaye na mamaye nae ataambatana na mumewe nao watakuwa mwili mmoja.

Haijasema wanawake wataachana na baba zao na mama zao nao wataambatana na mume wao nao watakuwa mwili mmoja, hili linathibitisha kumiliki wake wengi kunahitaji maarifa zaidi na lazima yatoke kwa Mungu, refer mfalme Suleiman.

Sasa wewe leo toka nenda bar chukua barmaid, then pitia Kwa macheni chukua mtoto, rudi kwa jirani yako chukua binti yake muimba kwaya, wachanganye wote hao halafu uone kama hiyo nyumba yako itakalika.
 
Je kama mtu akiwa na mke na bado akawa na michepuko, utasema hiyo michepuko ni wanawake wa kufanana nae?
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
6,560
2,000
Je kama mtu akiwa na mke na bado akawa na michepuko, utasema hiyo michepuko ni wanawake wa kufanana nae?
Hapa tunazungumzia mke wa kufanana nawe au wake kama ilivyoainishwa kwa wale waliopewa na Mungu kwenye biblia, no mchepuko at all hao sio wake au mke.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom