Je ushirikiano wa wapinzani unatakiwa bungeni tu katika kuunda serikali kivuli? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je ushirikiano wa wapinzani unatakiwa bungeni tu katika kuunda serikali kivuli?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Naloli, Feb 4, 2011.

 1. Naloli

  Naloli JF-Expert Member

  #1
  Feb 4, 2011
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 416
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nimesoma maoni mbalimbali ya wanasiasa hasa wa CDM, CUF na NCCR wakionyesha umuhimu wa kuunda serikali kivuli ya kambi ya upinzani Bungeni iliyoshirikishi kwa vyama vyote vya upinzani. Mimi binafsi HOJA hiyo inanikanganya, maana inahonyesha vyama vyetu vya upinzani vinaona umuhimu wa kushirikiana hupo Bungeni lakini ktk harakati za kuing'oa CCM mabarakani kupitia Chaguzi watu hao hawako pamoja, najiuliza kila wakati je hawa watu watawezaje kuwa wamoja Bungeni wakati wakiwa nje wanaongea lugha tofauti?

  Nakumbuka kuna uchaguzi wa marudio(kama kumbukumbu zangu ziko sawa) ulifanyika Zanzibar baada ya mizengwe ya CCM na Tume yake ya Uchaguzi Zanzibar walipoona CUF wanapata ushindi wakishindo, lakini wakati wa harakati za marudio ya uchaguzi Mwenyekiti wa NCCR mageuzi JAMES MBATIA akawawekea pingamizi wagombea zaidi ya 6 wa CUF na pingamizi likapitishwa, hadi CUF wakabuni kura za maruani ili kuvuruga uchaguzi huo. lakini ulifanyika na CCM wakashinda, Chakujiuliza pingamizi lile lilikuwa na manufaa gani kwa upinzani na NCCR? je Chama cha namna hiyo ni cha kushirikiana nacho? mwaka 2010 MBATIA huyohuyo kashindwa vibaya ktk uchaguzi wa UBUNGE jimbo la KAWE yaani hata mshindi wa pili toka CCM kamuacha mbali mno, mshindi ni MDEE wa CDM, kama kawaida yake kaweka kapinga ushindi huo mahakamani, cha kujiuliza pingamizi hilo ni lamanufaa kwa NCCR au upinzani?

  Mbunge wa TARIME marehemu CHACHA alipofariki viongozi wa upinzani MBATIA toka NCCR na Prof. LIPUMBA toka CUF walitangazia umma kuwa wanaushaidi kuwa CHACHA kauwawa na Uongozi CDM wanausika, Hivi wapinzani wa aina hii ni wakushirikiana nao kweli? na katika uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi hiyo vyama hivyo vikasimamisha wagombea na ktk kampeni ya vyama hivyo kauli hizo zikajirudia, Hadi mpinzani mwingine MTIKILA kupigwa mawe na wanaTARIME.

  Wakati huohuo Mwenyekiti wa TLP ktkt kampeni za urais 2011 alimtosa mgombea urais wa chama chake na kumpigia debe kikwete kuwa ndie rais bora na kutaka wananchi wamchague,huyu kagombea Urais mara mbili kupitia TLP wanachama wote walimuunga mkono, leo wanachama wanampitisha mtu mwingine kugombea anasema hafai anampigia debe mgombea wa CCM je mpinzani au wapinzani wa aina hii ni wa kushirikiana nao?

  Yaani kuna vituko vingi vya vyama hivi vya upinzani? wana jf kweli kuna upinzani wa maana au kugangia tumbo? je ushirikiano wa upinzani unatakiwa Bungeni tu? nje kila mtu kivyake?​
   
Loading...