Je, ushawahi kupigwa jungu kazini?

nzalendo

JF-Expert Member
May 26, 2009
11,711
11,972
Je, ushawahi kupigwa jungu kazini? Usiombee...

Hili jambo bado nalifanyia utafiti manake mara nyingi husababishwa na husda(wivu mkubwa).

Namna ya kuepuka;

1. Usichangie neno lolote ukutapo mtu anapigwa Jungu, elewa kwamba ukishawapa mgongo nao watakuzungumza.

2. Usimfahamishe yeyote mipango yako kama ujenzi, biashara, mifugo n.k.

3. Epuka sana neno NAJUA hasa kama kuna kitu unaelekezwa.... Hata kama unajua, sikiliza kwanza mpaka mwisho.

4. Don't shake hands with bosses... epuka kuwa karibu na mabosi.

5. Kama kuna dili usiwe mbele sana wala nyuma sana.
 
Kwa watanzania, Kugongwa JUNGU hakuepukiki.

1. Usipochangia neno lolote kwenye mijadala ya kijungu, utagongwa jungu na kuambiwa UNAJIONA.

2. Usipowashirikisha mipango, utagongwa jungu na kuambiwa UNAJIDAI.

3. Ukiwa unasikiliza tu bila kujifanya mjuaji, utagongwa jungu na kuambiwa UNAJIPENDEKEZA.

4. Usipokuwa karibu na ma boss utagongwa jungu na kuambiwa unawaonea WIVU. Nk

Ha ha ha! Majungu ni watanzania, na watanzania ni majungu ... Ni unkwepable. Lolote utakalofanya watakusema tu.

Cha msingi ni kuwapuuza tu;
 
Ndio maana mjini hapa machizi wanaongezeka.......wewe unadhani ni nani atavumilia kuona kuwa mtu fulani anaisababishia familia yake mahangaiko kwa sababu ya husda zake........jua kabisa unapompiga mwenzio majungu ili atimuliwr kazi haumuathiri yeye tu bali pia unaisababishia matatizo familia yake nikiwa na maan wategemezi wake...........

Sio jambo zuri hata kidogo haya yanayofanyika maeneo ya kazi.....

Niliwahi kufanya kazi kwenye kampuni moja...dah yule boss mzungu akawa kila siku anapelekewa majungu kunihusu....mpaka sik moja akaniita ofisini na kuniuliza kuwa kuna nini kinaendelea kati yangu mimi na wafanyakazi wenzangu....?? Nikamwambia hakuna akaniambi mbona wakina fulani ( akawataja na majina kabisa) wananiambia habari mbaya kila siku kukuhusu wewe....??

Hapo ndipo nikawajua kuwa kweli waswahili ni balaa......
 
Nafanya kazi ya ualimu hapa mwanza,kujamaa hapa wa morogoro anaroho mbaya sana,amewahi kunizungumzia staff ni kiwa sipo eti ninajidai kisa sihusiki na mijadala ya majungu,asee nilitaka nimtolee uvivu bahati yake akakimbia,jama ana miaka 43 lakni yuko mwaka wa pili kwenye ajira ya ualimu,sijui alikuwa wapi umri wote huo.
 
Yaani mimi nilishawahi pigwa jungu,mpaka jamaa wakawa wanatamani niwe kwenye jeneza,halafu sasa watu wenyewe ukiwa nao mnafurahi wakiwa hawaelewi kitu wanakuomba uwasaidie,kumbe ndo maadui number moja.nILISEMA WATATANGULIA WAO KUFA.Mungu mkubwa mpaka ninapoandika wawili kati yao walishatangulia mbele ya haki
 
Mungu hawezi kufanya kitu kama hicho. Unamsingizia. Mpende adui yako
 
Nafanya kazi ya ualimu hapa mwanza,kujamaa hapa wa morogoro anaroho mbaya sana,amewahi kunizungumzia staff ni kiwa sipo eti ninajidai kisa sihusiki na mijadala ya majungu,asee nilitaka nimtolee uvivu bahati yake akakimbia,jama ana miaka 43 lakni yuko mwaka wa pili kwenye ajira ya ualimu,sijui alikuwa wapi umri wote huo.

Kwamba ana miaka 43 na kwamba ni mwaka wake wa pili katika ajira..... mpaka ujue yote haya lazima kuna majungu yalifanyika... right?
 
Yaani mimi nilishawahi pigwa jungu,mpaka jamaa wakawa wanatamani niwe kwenye jeneza,halafu sasa watu wenyewe ukiwa nao mnafurahi wakiwa hawaelewi kitu wanakuomba uwasaidie,kumbe ndo maadui number moja.nILISEMA WATATANGULIA WAO KUFA.Mungu mkubwa mpaka ninapoandika wawili kati yao walishatangulia mbele ya haki
Mmmhhhh..... vipi kwani uliugua kwa muda mrefu?
 
Kwamba ana miaka 43 na kwamba ni mwaka wake wa pili katika ajira..... mpaka ujue yote haya lazima kuna majungu yalifanyika... right?
Unajua serikalini mwisho wa kuajiriwa ni miaka mingapi? Huyo jamaa atakuwa mjanja sana kapiga kazi zake kwenye maeneo yanayolipa vizuri, sasa amekuja kumalizia mahali penye pensheni! MAJUNGU HAYAJENGI!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom