Je, ushawahi kukutana na kibwengo au jini barabarani/ popote; ulifanyaje?

MR.NOMA

JF-Expert Member
Feb 1, 2014
338
502
Salam Wakuu

Wakati nipo kidato cha pili,siku 1 nikiwa napita mahala kuna mto mdogo/ korongo lenye maji usiku wa saa 3 niliona kitu Kama mtu mfupi Sana kipo mbele yangu kikiwa kimevaa nguo nyeupe.

Sikupoteza muda kukitazama niligeuza na kutoka speed mia na kitu, Mara nikadondoka,ile kucheki nyuma nikaona Kama kanakuja,niliinuka japo nilichubuka mikononi na magoti lakini nilitoka speed ya hatari sana mpaka home.

Sina uhakika mpaka leo Kama kweli kilikuwa ni kibwengo au laah! Kwasababu Mara nyingi tumekuwa tukisikia habari za watu kukutana na viumbe hawa, nini uzoefu wako katika hawa viumbe?

Je, ushawahi kutana nao? Wapi na muda gani? Ulifanyaje? Kwanini uliamini ulichokutana nacho ni kibwengo/ jini?
 
Ise pole ndg,ipo hivi hata kama mazingira uyafahamu vzuri usiku,hubadilika,nakumbuka siku moja nilikuwa maeneo fulani nilichelewa mida ya saa nne usiku,hivyo nilikutana na kitu kimevaa,nguo nyeusi kinanifuata,nikisimama na chenyewe kina simama,ase nilikimbia huku nikipiga yowe,watu walitoka na hawakuona kitu,tola siku hiyoo uoga ukaisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka nilikuwa nasoma shule moja ipo NZEGA inaitwa UCHAMA SECONDARY AU St Justine .

Siku hiyo nikaamua nikadoji mida ya saa 3 asubuhi nikaenda kulala bwenini na ni yale mabweni yapo kama kanisa marefuu vimepangwa vitanda tu alafu mlango huwa mmoja
Basi nikalala kitandani peke yangu bweni zima bwana wee ghafla kakatokea kamtu kafupi saizi ya ndoo la lita 20 kinene kina ulimi mrefu unabiruza chini alafu umegawanyika mara mbilii hayo machoo yake sasa makubwa hatar yani anafanana kama bundi alafu manyoyaa mwili mzima.

Mama weeee kikawa kinakuja kitandani
Nilipokuwa nimelala hapo nimeshatetemeka nusu ya kufaa nikawa nachungulia kwa mbali nikasema leo nakufa leo nanyonywa damu puani.
Nishawahi kusikia kuna vijitu vinanyonya sijui ubongo basi siku hiyo nikajua nakwisha.

Baada ya muda kile kibwengo kikaja mpaka kitandan kinataka kunyanyua ulimi kinashindwa maraa nikasikia mgunoo mhggggggggruruuuuu macho kikatoa mm hapo natetemeka nifanyeje sasa nahisi raha za dunia ndo naacha.

Ghafla kikayeyuka fyaaaaaa
Wewe sijui nilipata wapi nguvu nikatoka bwenini ndukriii sjavaa viatu na getini kulikuwaga na kigeti mshenzi sikumbuki nilipitaje palee bilaa kukisogeza maana huwa mpaka ukisogeze nafasi ni nyembamba sana
Uyo mpaka darasan alafu kulikuwa na mwalimu wa Physics anaitwa Initial velocity daah nikawaambia niacheni kwanza nitahadithia.

Toka siku hiyo sijawahi kudoji mpaka namaliza Secondary

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna Mda Huwa Macho yanadanganya au Yanaunda Taswira isiyo sahihi sehemu yenye Giza..! Ukitaka kuthibitisha hili, Fanya hivi... amka usiku ukiwa usingizini Toka ghafla Nje ya nyumba, ukiwa unaangaza umbali fulani unaweza ukaona labda mtu kasimama, au ukahisi kitu kama mnyama ila kiuhalisia ni kitu tu labda ni mzigo wa takataka...!!
 
Utangulizi "JINI ni nini..."

Jini ni jina la Kiswahili lililotokana na jina la Kiarabu "Jin". Majini ni viumbe wanaosadikika kuishi katika mazingira ya kila aina; pia baadhi ya watu wanaamini majini ni viumbe wenye uwezo mkubwa wa kufanya vitu tofautitofauti, pia wenye uwezo wa kujibadilisha kuwa katika hali
waipendayo.

Kwa asilimia kubwa wenye imani ya uwepo wa majini wanasema ni viumbe wasioweza kuonekana, hivyo ni vigumu kupata uthibitisho wa moja kwa moja kuhusiana na viumbe hao. Imani hiyo huko Arabia ilitangulia mwanzo wa Uislamu ikaingia dini hiyo na kwa njia hiyo kuenea katika nchi mbalimbali.

Kadiri yake majini waliumbwa na Mungu kwa kutumia moto na wakiwa wa jinsia mbili.

Uislamu huamini kuna majini wazuri na majini wabaya kwa maana ya madhara yao katika maisha ya mwanadamu na Waislamu wengine hufuga majini hao katika nyumba zao au miili yao na kuwafanya viumbe hao kama wasaidizi au walinzi wa maisha yao kwa wale ambao huamini ni majini wazuri.

Lakini wengine hutumia majini waitwao wabaya kuharibu na kutesa maisha ya watu wengine kwa kuwatuma kuwaingia miilini na kuleta magonjwa, kuharibu kazi au biashara ya mtu na hata familia.

Ukristo haupatani na imani hiyo, lakini kuna madhehebu ya Kikristo ambayo huamini uwepo wa majini kwa kuwasawazisha na mashetani, sema wenye kufuata mila za Kiarabu. Hivyo kwao
hakuna jini mzuri bali wote ni wabaya na wao na
mashetani ni sawa, hivyo ni adui wa Mkristo
yeyote yule kama alivyo Shetani.

Wakristo wa madhehebu hayo wamekuwa wakifanya maombi kwa watu ambao wanateswa na majini ili kuwafungua kutoka katika nguvu zao za uovu, sawa na mapepo ambao Bwana Yesu (mwanzilishi wa Ukristo) aliwatoa miilini mwa watu na kuwapa wanafunzi wake (wafuasi wake ambao ni Wakristo leo) mamlaka na uwezo wa kuwatoa pia.
 
Wakati nipo sekondari miaka ya 2006 palitokea bwana mdogo mmoja anayelala chumba kinachotazamana na chetu alitokewa na Popobawa mida ya saa saba usiku. Basi akapiga kelele "Mamaaa popobawa ananiuaa"

Bweni letu halikua na umeme kwa hiyo kulikua na giza totoro, niliruka kutoka juu ya kitanda kisha nkakimbia kwa kasi ya kilomita 540 kwa saa, kumbe mbele nilikua nmekosea mlango hivyo nilivamia ukuta na nundu iliota ndani ya sekunde moja.

Sikuwahi kuwa na hofu kuu maishani kama hofu nilioipata siku ile na siku kama 4 zilizofata

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu ndo uhalisia wenyewe.
Kuna Mda Huwa Macho yanadanganya au Yanaunda Taswira isiyo sahihi sehemu yenye Giza..! Ukitaka kuthibitisha hili, Fanya hivi... amka usiku ukiwa usingizini Toka ghafla Nje ya nyumba, ukiwa unaangaza umbali fulani unaweza ukaona labda mtu kasimama, au ukahisi kitu kama mnyama ila kiuhalisia ni kitu tu labda ni mzigo wa takataka...!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku moja nikiwa maeneo ya shuleni (kijijini huko,hakuna umeme wala solar) ninawinda dem.Nikafika nyumbani kwa msichana ninae fukuzia..(kota za shule)
Pemben mwa nyumba yao kuna miti ambayo mchana hutumika kwa wanafunzi kupumzika.

Basi bana usiku huo,nikiwa hapo nimekaa nje ya mlango wao,ghafla nikaona mtu anatoka upande mmoja wa mti akaenda kusimama nyuma ya mti mwingine.
Kichwa kikanisisimka,nikawauliza wenzangu kama wamemuona Huyo mtu wakasema hapana,ila twende ukatuonyeshe.
Bwana weeeee'Nilikuwa nimepakia viroba konyagi, kichwani wakanitanguliza mbele
Mhhhhhh hofu na kipombepombe moyo ukawa unanidunda kama unataka kuchomoka,tukaenda mpk karb na huo mti nikawaonyesha kuwa nimemwona hapa,tukazunguka nyuma ya huo mti hatukuona kitu/mtu. Tukarudi.
Sikuamini kabisa na wala macho yangu hayakunidanganya.
Mpka Leo nikikumbuka,sipatagi picha kua kilikuwa ni kiumbe cha namna gani.
Na ali disappear mda gani,sielewagi na sijapata majibu mpka sasa.

Bado Naendelea Kujifunza
 
Muyamaaaaaaa, Kasulu, Kigoma

Natoka zangu kibanda umiza kwao Erasmus Luziro (mtangazaji wa radio kwizera) madukani kucheki mechi ya Uefa fainal ya arsenal na barca baada ya game nikaanza kujivuta kwenda camp (geto) wakati huo niko na washikaji tulipofika kona ya kushika uelekeo wa kuelekea shule ya msingi muyama, wenzangu wote wakanyoosha kuelekea kijijini ikumbukwe kuwa wanafunzi wengi wanaoishi camp walikua wakitazama mpira sehemu moja inaitwa Kalege na pale palikua karibu na shule.

Nikaanza kujivuta mwenyewe wakati huo nakabiliwa na kupita katikati ya misufi iliyoko shule ya msingi, hapo ndo nikaanza kukumbuka stori ya jamaa mmoja pale kijijini aliyekuwa mlemavu wa mguu, na nilishaambiwa sababu ya ulemavu wake ni kukutana na majini pale kwenye ile misufi yakamtenda jeuri lakini pia kulikua na stori ya mlinzi mmoja alikua na kawaida ya kusinzia usiku, siku moja mida ya nyt kali kakosa usingizi akashuhudia mahudhurio ya wazungu darasani, baada ya kusimulia hiyo stori akavuta

Nimevutika nikafika pale nikahisi nywele zinasimama mwili unasisimka afu kulikua na kaubaridi lakini eneo lile lilikua na joto sana, hiyo ilikua mida ya 6+ hivi, lakini nikavuka poa.

Nikaendelea kuvutika, sasa hapo nikawa napawaza sehemu moja inaitwa kavuruga hapo pia kulikua na msufi afu kalikua kama kakijito fulani, nimevutika na kutoka madukani ni mbali, kwa miguu ni wastani wa dk 45 mpaka 1hr hivi kufika sekondari na ndo nilikokua naishi Tifu likaanza baada ya kufika pale.

Nikawa kama nimeambiwa, nkainua macho kutazama juu nikaona matawi yanatikisika sana wakati hakukuwa na upepo, nikajua hapa game imeanza sasa, nikapiga hatua kadhaa nikaona kama kitu cheupe kimekatiza mbele yangu haraka, wakati nawaza nitimue mbio nikakumbuka mama angu mzazi aliwahi niambia ukikutana na kitu cha ajabu usiku usikimbie wala usioneshe hofu maana wakati mwingine waga vinatisha tu ko' ukiweza kuhimili mikiki watahisi hujaona, lakini ukikimbia unaweza jikuta ukipotea. Nikavaa ujasiri, nikavuta hatua kama 6 nikahisi kama hatua za mtu yuko sambamba upande wa kushoto na mimi lakini kikawa simuoni, mara anahamia kulia mara mbele lakini haonekani ila ukisikia hatua zinakuambia kuna mtu.

Tumetembea na jamaa mpaka kwenye kibao cha shule ndo nikahisi hatua zimepotea. Nikavutika zangu hadi geto maana nilikua naishi nyumba za mwisho kabisa kuelekea kasumo, nikafika nikaingia ndani hapo ndo nikagundua majimaji ya chumvi yalipenya kwenye suruali bila ushiriki wa ubongo.

Ntarudi baadae na vingine viwili, ila hiki kisha ndo kilinitisha zaidi, maana kwanza nilikua mgeni huko na stori za kigoma kama mnavyozijua ilikua full vurugu asee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimetembea sana usiku ila sijawahi kukutana na kitu cha kutisha ila kuna siku nilikutana na kitu kirefu huko katika milima ya Odizungwa nikakimbia sana usiku ila mpaka leo sijathibitisha kama ni kitu cha ajabu au fikra zangu tu ndio zilijenga ile taswira usiku hule huenda ulikua mti. Ila natamani sana siku moja nije kuona vitu visivyoonekana mradi tu iwe katika mazingira rafiki sio ya kuogopesha au nipo peke yangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahaaa umenichekesha sana,mimi nilisikia wanaongea kikosini kuwa kuna kashotii yani kimbwego,si unajua majeshini watu huwa wanadoji iwe usiku au mchana,yani huko madoja ndo wapo sasa.

Sasa kuna madoja walidoji usiku mida kama ya saa nane hivi wapo porini wamelala,walikurupushwa na hako ka shotii ,kakawakimbiza hadi kikosini,kuruta mmoja akawa ameumia mguu kwenye kisigino,ikawa pale kikosini inshu imeenea kuwa kuna kibwengo kinawatimua madoja,dah ilikuwa shida mana mimi mwenyewe nilikuwa doja mzuri sana,ila sikuacha kudoji ,si unajua mkesha ulivyo,unatingwa usingiz balaa ,ukijilaza sekunde 30 nyingi wewe unakoloma harafu ni pori.ila baati nzuri mimi sikukurupushwa na shotii
Nakumbuka nilikuwa nasoma shule moja ipo NZEGA inaitwa UCHAMA SECONDARY AU St Justine .

Siku hiyo nikaamua nikadoji mida ya saa 3 asubuhi nikaenda kulala bwenini na ni yale mabweni yapo kama kanisa marefuu vimepangwa vitanda tu alafu mlango huwa mmoja
Basi nikalala kitandani peke yangu bweni zima bwana wee ghafla kakatokea kamtu kafupi saizi ya ndoo la lita 20 kinene kina ulimi mrefu unabiruza chini alafu umegawanyika mara mbilii hayo machoo yake sasa makubwa hatar yani anafanana kama bundi alafu manyoyaa mwili mzima.

Mama weeee kikawa kinakuja kitandani
Nilipokuwa nimelala hapo nimeshatetemeka nusu ya kufaa nikawa nachungulia kwa mbali nikasema leo nakufa leo nanyonywa damu puani.
Nishawahi kusikia kuna vijitu vinanyonya sijui ubongo basi siku hiyo nikajua nakwisha.

Baada ya muda kile kibwengo kikaja mpaka kitandan kinataka kunyanyua ulimi kinashindwa maraa nikasikia mgunoo mhggggggggruruuuuu macho kikatoa mm hapo natetemeka nifanyeje sasa nahisi raha za dunia ndo naacha.

Ghafla kikayeyuka fyaaaaaa
Wewe sijui nilipata wapi nguvu nikatoka bwenini ndukriii sjavaa viatu na getini kulikuwaga na kigeti mshenzi sikumbuki nilipitaje palee bilaa kukisogeza maana huwa mpaka ukisogeze nafasi ni nyembamba sana
Uyo mpaka darasan alafu kulikuwa na mwalimu wa Physics anaitwa Initial velocity daah nikawaambia niacheni kwanza nitahadithia.

Toka siku hiyo sijawahi kudoji mpaka namaliza Secondary

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati nipo sekondari miaka ya 2006 palitokea bwana mdogo mmoja anayelala chumba kinachotazamana na chetu alitokewa na Popobawa mida ya saa saba usiku. Basi akapiga kelele "Mamaaa popobawa ananiuaa"

Bweni letu halikua na umeme kwa hiyo kulikua na giza totoro, niliruka kutoka juu ya kitanda kisha nkakimbia kwa kasi ya kilomita 540 kwa saa, kumbe mbele nilikua nmekosea mlango hivyo nilivamia ukuta na nundu iliota ndani ya sekunde moja.

Sikuwahi kuwa na hofu kuu maishani kama hofu nilioipata siku ile na siku kama 4 zilizofata

Sent using Jamii Forums mobile app
Hizo siku 4 palitokea kitu gani mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom