Je usalama wa maisha ya wananchi na usalama wa viongozi upi ni wa muhimu

Gembe

JF-Expert Member
Sep 25, 2007
2,502
153
Kutoka Mwananchi la leo.
Hatuwezi kufanya majaribio kwa rais wetu,sisi atuwezi kukubali avuke katika mazingira haya yasiyo salama alisikika mmoja wa wasaidizi wa Rais akisema
Hayo ni maneno yaliyotolewa Wakati Rais aliposhindwa kupanda kivuko cha Pangani kwa kuwa ni kibovu.Ila Rais alifika hapo baadaye na kuwahaidi wananchi hao serikali itaweka kivuko hivi karibuni sababu mzabuni alishapatanikana.

MYTAKE
1.Ina maana kipindi chote wananchi wengi walikuwa wakitumia kivuko hicho kikiwa na hitilafu ya kupoteza mwelekeo kwa muda mrefu,hawa wasaidizi wa Rais walikuwa wapi kusema kwamba Hatuwezi kufanya majaribio kwa wananchi wetu,sisi atuwezi kukubali avuke katika mazingira haya yasiyo salama.?

2.Hapa unapata Picha gani?Je wanapenda siye tuendelee kuishi?

3.Nimegundua Jk anafanya kazi ila anaangushwa na watendaji wake,wamekuwa wakimuhdaa na kumdanganya.Ngudu Rais Je bado unaona ni haki kwa wanachi kuendelea kuteseka kisa wao siyo viongozi

Yes I said,Kumbe viongozi wakubwa ni bora kuliko wanachi,na hii ndiyo sababu hawatusikilizi.wasaidizi wa viongozi wako tayari siye tuzame na tuishe maisha magumu ila siyo wakuu wao.Wamepandisha kodi ili wao wandelee kusihi

Mie nimekubali yaishe
 
Kevo

JF-Expert Member
Jun 12, 2008
1,333
50
Ulinzi wao its obvious ni wa muhimu ila walalahoi hawana umuhimu kabisa.Mimi nashindwa kuwaelewa hawa watu,hivi walishakaa chini even once in their life time waka acknowledge kwamba bila ya hawa watu ninaowadharau nisingekuwepo hapa nilipo?kazi yao ni kujilimbikizia mali and not otherwise.Anyways tusiwalaumu hawa wakwetu hata huko kwenye developed nations ulinzi wao ni muhimu kuliko hata maisha ya walinzi wao.Ndio mambo ya loyalty and allegiance to your master while making your life worthless.
 
WildCard

JF-Expert Member
Apr 22, 2008
7,510
2,400
Helikopta ile ya Kamanda Tossi haipo? Ingemvusha tu halafu ikaendelea na kazi yake ya kutafuta mapipa ya gongo,...
 
Gembe

JF-Expert Member
Sep 25, 2007
2,502
153
Helikopta ile ya Kamanda Tossi haipo? Ingemvusha tu halafu ikaendelea na kazi yake ya kutafuta mapipa ya gongo,...

Hoja siyo Helikopta ya Tossi,ila umuhimuwa Wanachi wa taifa hili.Kipaumbele kipo wapi hasa.manaake hicho kivuko kimpigiwa kele muda mrefu na serikali haijawahi kukifanyia matengenezo .

What is our Priorities kama siyo wananchi,Serikali inasema hakuna pesa ila kila siku inanunu V8.magari yanayotumia mafuta mengi..kwenda Dodoma ni lita 200.serikali yetu ndiyo kila siku hapo dodoma wanakula Sherehe.
 
Haya ya kweli serikali inapaswa ijipange upya iangalie gharama zake zisizo za lazima and what should come first as matters of national interest.Wananchi wanao nyanyaswa na polisi na wenye fedha zao pamoja na hao majambazi ambao hawaishi kuvamia nyumba za watu asubuhi,mchana na usiku serikali inachukua hatua gani?wao ni kupiga kelele bila vitendo.
Kwa kiasi fulani ningempongeza bwana Tossi kwa kazi nzuri anayofanya.Huyu jamaa anajitahidi angalau kuchimbua na kumaliza baadhi ya maovu na Polisi wengine waige mfano kwake na serikali kuu ielewe umuhimu wa Wananchi wake!
 
Mpita Njia

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
6,997
1,156
Ina maana watanzania wanaotumia kivuko hicho kila siku wanahatarisha maisha yao! Wanatumika kama nguruwe wa majaribio (guinea pigs?)
 
Kevo

JF-Expert Member
Jun 12, 2008
1,333
50
Ina maana watanzania wanaotumia kivuko hicho kila siku wanahatarisha maisha yao! Wanatumika kama nguruwe wa majaribio (guinea pigs?)

Hao ndio specimen mkuu.Mpaka siku hicho kivuko kizame ndio kiatonekana kilikuwa hatari.Hawa viongozi ni wanafiki sijapata ona.
 
Gembe

JF-Expert Member
Sep 25, 2007
2,502
153
Hao ndio specimen mkuu.Mpaka siku hicho kivuko kizame ndio kiatonekana kilikuwa hatari.Hawa viongozi ni wanafiki sijapata ona.
Kwanini wanatufanya sie Specimen.
Nani anawpa kiburi cha kutufanya mandondocha?
Nataka kujua hiki kiburi wanakitoa wapi?
Kuna mtu anajua kuhusu hili?
 
Kevo

JF-Expert Member
Jun 12, 2008
1,333
50
Kwanini wanatufanya sie Specimen.
Nani anawpa kiburi cha kutufanya mandondocha?
Nataka kujua hiki kiburi wanakitoa wapi?
Kuna mtu anajua kuhusu hili?

Anayewapa hiki kiburi ni sisi Wananchi na siyo mtu mwingine yeyote yule.Mind you jana naangalia taarifa ya habari Jk anasema kivuko chenyewe spanner mkononi halafu wale Wamama wa Kiswahili wanacheka kile kicheko chao cha kinafiki mpaka mwisho bila wao kutambua ya kwamba Rais hakupanda sababuya usalama wake.
 
Gembe

JF-Expert Member
Sep 25, 2007
2,502
153
Anayewapa hiki kiburi ni sisi Wananchi na siyo mtu mwingine yeyote yule.Mind you jana naangalia taarifa ya habari Jk anasema kivuko chenyewe spanner mkononi halafu wale Wamama wa Kiswahili wanacheka kile kicheko chao cha kinafiki mpaka mwisho bila wao kutambua ya kwamba Rais hakupanda sababuya usalama wake.
Hii ni kwasababu siye ni mandondocha
 
kalld

Member
Jun 14, 2007
87
0
kivuko hakifanyi kazi muda mrefu watu wanatumia ??mashua au boat ndogo ,hiyo hali ilikuwa mwezi mmoja uliopita!kuna watu walikwenda wale waoga wa mashua walirudi hawakuweza kuvuka!
ila sijui nadhani ni muda mrefu kivuko hicho kimeacha kufanya kazi ukizingatia usalama wa sehemu yenyewe wanadai inakina kirefu sana!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom