Je, Urembo, Usharobaro wa kizembe na kuzurura mitaani vitaisha?

rbsharia

Member
Sep 14, 2011
41
6
"Hii itasaidia kupandisha heshima, utiifu, ukakamavu na ufanisi wa vijana"
Ni kauli ya mheshimiwa mmoja kufuatia Serikali kutangaza tena na kuthibitisha kuwa, kuanzia mwaka huu ni lazima kwa kila kijana atakayemaliza form VI apitie JESHI kisha ndio aende chuoni au aendelee na mambo mengine ya kujijenga na kulijenga Taifa la Tanzania.

Hapo imekaaje? KARIBUNI UWANJA NI WETU SOTE KUJADILI kama kawaida yetu.
 
hii kwa mimi naipa 50 50 yani ni bora, lakini pia ni kama inapotezea tu watu mda wao kuendelea na masomo!
 
kwa mtu yeyote mwenye mtizamo chanya na hili taifa, hlii wsala ni zuri sana kwani kwa sasa taifa linakosa wale vijana wa Mwalimu. Hivyo tuombe sana serikali yetu irudishe hicho kitengo cha kupitia jeshini ili 2siwe na wasomi abrubakacha ambao hawapo tayari kuwajibika maeneo yeyote ya taifa lao, bali tuwe na vijana imara watakaofanya kazi kwa moyo mweupe na kwa maslahi ya watanzania wote.
 
Naunga mkono hoja, Jeshi lingesaidia kupata uvumilivu, ukakamavu and uzalendo kwa vijana wa sasa. Dot com world, tumeona hata nchi zilizoendelea bado wanahimizi national service.
 
ok ok ok hapo sawa, na je hawa ambao hawaendi shule hawawezi kuwa nyoka wa kuwaambukiza sumu hawa wengine wanaoenda shule na kupita jeshini?
 
mi naona ni mpango mzuri LAKINI kila siku serikal yetu utasikia "tuko mbioni", "tuko kwenye mchakato" sidhan kama itawezekana kutekeleza kwa sasa!!
 
Waache wawapeleke bwana waje watusaidie kupambana na ffu wakati wa migomo
 
Back
Top Bottom