Naja naja
JF-Expert Member
- Sep 13, 2016
- 747
- 1,452
Inafahamika kwa ngazi za chini za elimu mathalani elimu ya sekondari mwanafunzi akiona ana mapungufu sehemu anaomba kukariri darasa na anakubaliwa bila tatizo lolote,je jambo hili kwa ngazi ya chuo linawezekana au mpaka mwalimu aamue kukukaririsha darasa kilazima na si wewe mwanafunzi kwa mapenzi yako?
Case yangu nilisoma kwa tabu na baada ya mzazi kufariki nikaishia njiani kielimu kutokana na kukosa mtu wa kunisomesha na sikuona sababu ya kuandika barua ya kusitisha masomo kwa muda maana nilishafanya mwanzoni kisha nika resume bila mafanikio yoyote sasa.
Kwa sasa wametokea baadhi ya ndugu wanataka kuunganisha nguvu kunisomesha na nikimaliza kusoma kuna kazi nzuri ninaweza nikapata hivyo nimeona nikaombe nikariri darasa moja nyuma ili niwe competent enough nisiweze kuharibu kazi ya watu maana hilo darasa japo nimeshalisoma semester zote mbili ila nataka nilirudie maana kipindi kile cha shida nilipunyua punyua kutokana na ugumu wa maisha uliopitiliza.
Nifuate taratibu zipi au nikaongee na dean na mkuu wa chuo kumueleza lengo langu?