Volatility
JF-Expert Member
- Aug 22, 2018
- 3,906
- 7,456
Kumbuka hata Ubepari haujawahi kufanikiwa popote pale ambapo ulipigwa vita kwa mabavu, naposimamia ni kwamba hizi mifumo zote zinamazuri na mabaya yake, ingekuwa bora kama zingeachwa zishamiri kwa pamoja.Nashindwa kuelewa uliposimamia mkuu...
Ina maana ujamaa ulitakiwa upewe nafasi ukomae bila usumbufu kutoka kwa wale wanaoamini mfumo mwingine wa kibepari!???
Kuonesha ubora wake ujamaa ulitakiwa kuthibitisha uwezo wake na kushinda hila zozote zilizoletwa na ubepari...hivyo kufeli kwake kunaweza kuonesha ni kama mfumo dhaifu usio na tija!!!
Na sitegemei kwamba ingekuja kutokea eti kukawa na mfumo mmoja utakaokuwa umekubalika sababu ya mafanikio yake, kuna nyakati ujamaa unahitajika na kunawakati ubepari unahitajika hata katika maisha yetu ya kila siku.
extremism is evil