Je, Upo uhusiano wa anguko la Socialism ama Ukomunist Afrika na umasikini unaokumba nchi nyingi Afrika!?

Ukiangalia hao wote Che Guevara,,lumumba hata Chavez waliuliwa kwa sababu walikuwa wakimzindua mtu aamke ajitegemee.
Kitu ambacho ni kosa kwa establishment ya capitalism.
Kiongozi mm nakuelewa sn sn sn kwel kabisa walioukataa umoja ndo hao hao wakaja na maneno mengi ya kutudhihaki, hua napenda sn maisha ya wanaharakati kama guevara, chavezi na lumumba hawa watu kweli walikua wanaharakati wa kijamaa damu damu, dunia ipo hapa leo kutokana na sera chafuu za kunuka za ubepari, ubepari mwenywe nacho anazidi kua nacho mbaya zaidi asiyenacho anapokonywa ata hicho kdg
 
Mifumo yote iko sawa kama ikiwa exercised kwa muda mrefu. sisi tumeexecrise ujamaa kwa miaka 25 tu tukakata tamaa. sasa tumebaki tunamangamanga tu tukiangalia nyuma tunapatamani tukiangalia mbele tunapatamani.
 
Socialism au ujamaa hauna mafanikio kimaendeleo ya muda mrefu kwa kulinganisha na capitalism au ubepari, la maana hapa Commitment ya capitalists ipo juu kuliko Socialism.

Kwa dunia ya leo kama mtu hajaliona hilo atakuwa aidha anamapungufu kiakili/ki saikolojia, exposure au upungufu wa elimu.

Hata hiyo china wanaisifia wapate nafasi ya kuitembelea tu, kama ni magofu ya viwanda vya umama yamejaa utaogopa, kiuchumi mtu asikudanganye kwamba china n inchi ya ujamaa uongo japo bado yapo masalia machache sana ya mashirika ya umma au viwanda ambavyo wana exploit wafanyakazi wao maskini cheap labour.

China ninayoijua naweza sema (Wananchi maskini katika maisha duni wakimiliki serikali tajiri sana ulimwenguni) wananchi wa china ni koloni la serikali ya china,

Maendeleo na utajiri wa china ni wa serikali/umma sio mwananchi japo huduma umma ziko juu sana kwa maana mabarabara hospitals, airports, Infrastructures zote

Jambo lingine la Muhimu sana kulitambua penye mjadala kama huu ni vema kutambua kuwa kila mfumo wa uchumi lazima una mazuri na mabaya yake ndani ya jamii husika.
Kwa maana hiyo usitegemee jamii inayonufaika na ujamaa (waliosoma shule za bure na family nzima ikaneemeka) hata siku moja hawezi sifia ubepari, au jamii iliyoteseka au kufilisiwa au kunyang'anya mali zao tokana na ujamaa hawawezi sifia ujamaa

Maoni yangu bora capitalist 10x kuliko ujamaa, kila mmoja kula jasho lake halali
China wanamixed economy kiongozi
 
Mkuu Capital Sido ilikuwepo toka enzi za Mwalimu,,technician wazuri walioko leo na Mainginia wazuri ni waliokuwa toka miaka hio,,,watu walipelekwa nje wasome udaktari,,uhasibu na sheria ili waje hapa wafanye mabadiliko,,kulikuwa na viwanda kila mkoa na vyote vilikuwa kwa ajili ya wazawa,,,

Je mfumo wa ujamaa unafifishaje ubunifu na vipaji na kumzuia mtu kutumia Maarifa yake kama kulikuwa tayari na platform ya kumfanya kila mtu mwenye kipaji kikutumia kwa manufaa mapana kabisa??

Ninapoongelea ujamaa ni mfumo wa kujitegemea sisi wenyewe na kuishi maisha yetu pasipo na kutegemea misaada,,,,,,,,,,leo World bank,,imf na taasisi nyingine za kimagharibi ndio watoa mikopo yenye masharti ya mkopwaji kubadili hadi mifumo ya Kiuchumi na taratibu za nchi,,kitu anachoiga mchina.

Ndio maana Irani anakatazwa kuuza mafuta yake mwenyewe,,na watu wanaambiwa wasiyanunue,,lengo ni ili afuate masharti yao,,mfumo wao na wao ndio wawe wanufaikaji wa raslimali zake kwa asilimia kubwa.

Kwa hio utegemezi wa kutisha na sekta binafsi kuharibiwa ni athari za masharti ya hao wasiotaka tusijitegemee kutaka wao wamiliki njia zetu za uchumi.

Ufisadi na kukosa uaminifu ni athari ya kutokuwa na nidhamu ya wenye kusimamia mfumo,,kusipokuwa na adhabu na ufuatiliaji wa matumizi ya pesa za uma.Sio kwamba ujamaa una loopholes za mtu kufanya ufisadi.

Ujamaa haujawahi kushinda kwa kuwa kuna watu wanataka wengine wasiwe huru,,wawe maskini na wanaowategemea wao.Na nikwambie hivi tulivyokubali masharti yao hakuna siku tutaacha kuwa wategemezi.

Sababu ya nchi za magharibi kuendelea ni kwa sababu nchi za kiafrika kushindwa kujitegemea na kujisimamia.

Na kama ilivyo kwamba Mwanafunzi hawezi mzidi mwalimu wake hatuwezi kuwa na mfumo wa kibepari wenye unyonyaji halafu tukaendelea.Uangalie uwekezaji na uufikirie vizuri.Na Kumbuka wanaosema mfumo wa kijamaa ni dhaifu ni wale wanaouchukia hasa wabepari.
Aiseee
 
China wanamixed economy kiongozi
Nakubaliana na wewe ni CHINA ya leo karibia miongo miwili sasa sio ile ya mwanzo.
Na hiyo ni baada ya kuona U communist una fail, the same Russia, Burgaria, Hungary, Vietinam wote wame switch to mixed economy.

Angalia maisha ya jamii/watu mmoja mmoja korea kaskazin, baadhi ya majimbo ya China,
ndio utagundua kabisa ujamaa ni tabu, aina fulani ya ukoloni wa ndani.
 
Mifumo yote iko sawa kama ikiwa exercised kwa muda mrefu. sisi tumeexecrise ujamaa kwa miaka 25 tu tukakata tamaa. sasa tumebaki tunamangamanga tu tukiangalia nyuma tunapatamani tukiangalia mbele tunapatamani.
Nimekuelewa naomba mfano wa nchi 2 tu zilizofaulu ku exercise ujamaa kwa muda mrefu na ziko imara kiuchumi lakini pia WANANCHI wako huru na maisha BORA kwa kuwalinganisha na majirani zake walio kwenye Capitalism ? natanguliza shukran
 
Kusema ukweli katika hali ya kawaida ujamaa nafasi yake ni ndogo sana katika akili na fikra za binadamu
kama walivyotangulia kusema hapo juu kwamba mwanadamu asili yake ni ubinafsi, nami naongezea wivu uchoyo na uvivu.
kwa sababu hio ilikua ni ngumu sana kuendelea na ujamaa vinginevyo ingehitajika garama kubwa sana ya maisha ya watu.
najaribu kufikiria jinsi ulimwengu ulivyoundika kwa kanuni, na kila kilicho ndani yake kiko kikanuni. ukijaribu kukiuka kanuni hizo ulimwengu utakinzana nawe.
kwa maana hio basi mwanadamu nae ni sehemu ya ulimwengu yupo kikanuni, na kanuni mojawapo ni hio kuwa mbinafsi.
wakati huo huo ujamaa una kanuni zake ambazo ni kinyume na ubinafsi.
kwa hio kusingekua na namna yoyote ya kufanikiwa kwa ujamaa nje ya mauaji makubwa ya watu. ndio mtazamo wangu kwa hili.
Fikra ya binadamu ni kitu ambacho kinatengenezeka kufuatana na mazingira au malezi. Wewe ni mbinafsi kutokana na malezi uliyolelewa na si vinginevyo.
 
Kweli kwa sasa ni ngumu maana pressure itakuwa kubwa kutoka nje kushinda hata ndani,,,,na nchi imeingia mikataba mingi sana ambayo ni kama kifungo.

Naongelea ungekuwa msingi tokea enzi ya mwalimu.Halafu misingi ingekuwa imara ndipo tubadilike tena kwa tahadhari.

Kuna mtu mmoja Anaitwa Edward Moringe Sokoine,,,kifo chake kina impact kubwa sana.Yeye Alikuwa anauamini huu mfumo nadhani hata zaidi ya Mwalimu.Laiti angekuwepo nadhani kuna mabadiliko yangekuwepo.
Ni ngumu sana kuujaribu huo msingi sasa, kuna wasomi wengi sasa huwezi control vichaa vyao kirahisi.
 
Ujamaa ni mfumo dhaifu sana, usio na tija na unaofifisha ubunifu na vipaji. Ujamaa hautoi fursa kwa mtu kutumia maarifa yake kikamilifu. Ujamaa ni mfumo usioweza kutofautisha mtu anayejituma dhidi ya mvivu.
Tanzania kufuata mfumo huo kwa miaka zaidi ya 20 ilikuwa ni kupotea tena vibaya. Na ni kweli tulipotea sana. Watu hatimaye wakawa wanafanya kazi ili mradi tu.. maana hata akifanya kidogo, matokeo ni sawa na aliyefanya sana..

Baada ya kujiingiza katika mfumo haram wa kijamaa tena kwa miaka mingi, Tz itaendelea kulipa kwa gharama kubwa sana na kwa miaka mingi ijayo.. athali za ujamaa ambazo ni wazi zinatukula kutokea ndani ni kama hizi:

1. Utegemezi wa kutisha
Amini usiamini, watanzania wengi zaidi ya 90% ni tegemezi kwa ndugu, jamaa au wazazi wao. Maana yake ni kwamba watanzania hawa hawazalishi mali ya maana ya kuweza kuwategemeza wao kikamilifu. Hali ni mbaya sana maana watz mchango wao kwa uchumi wa nchi ni kidogo sana. Kwa hiyo mzigo mkubwa uko juu ya mabega ya watu wachache sana.

2. Ufisadi na kukosa uaminifu
Sifa moja wapo ya ujamaa ni mgawanyo sawa.. baina ya waliofanya kazi sana na waliofanya kidogo. Ilipokuja suala la wafanya kazi wa umma kulipwa kidogo wakati ndio wanajuwa pesa zilipo.. likaibuka wimbi la wizi na rushwa katika sekta za umma zote. Mtakubaliana na mimi kwa kiasi fulani, tatizo moja kubwa hapa nchini ni ufisadi.. mara kagoda, epa, escrow, nk nk. Madudu kama haya yamesababisha mara nyingi sekta ya umma kuzorota, zikigubikwa na madeni makubwa na mashauri mahakamani yasiyoisha.. rejea trc, tanesco, ttcl, stamico etc zinavyopata shida

3. Kuharibiwa kwa sekta binafsi
Wajamaa ni watu wenye wivu na maendeleo ya mtu mmoja mmoja.. wajamaa wanaamini kwenye usawa wa umaskini badala ya usawa katika ukwasi. Wakiona mtu anarlekea kuwa tajiri kutokana na bidii zake binafsi, utasikia fitina zimeanza, mara uhujumu mara magendo.. upuuzi mtupu. Ni wazi sekta ya umma ina mauza uza yake linapokuja suala la uzalishaji mali au utoaji huduma. Hapa nchini sheria nyingi zilizoanzisha sekta ya umma zimejaa ukiritimba wa ajabu.. kiasi cha kuzifanya sekta ya umma kukosa tija. Ombwe hili lingeweza kufidiwa na sekta binafsi iwapo ingepewa kipaumbele. Katika ujamaa wa kiwango duni, sekta binafsi imebaki mateka, kiasi cha kufanya mchango wake kuwa kidogo. Hii ni sekta ambayo watu wengi wangeshiriki kuzalisha mali na kutoa huduma. Sekta hii baada ya kuzubaishwa, haikui, haiajiri, na serikali haipati pesa kutokana na kodi ambayo ingelipwa.
Serikali ya awam ya tano inaendelea kufanya makosa makubwa kuamini tena ujamaa duni, huku ikijua kuwa ujamaa haujawahi kushinda.
Shukran sana kwa ufafanuzi wako, umeonyesha ukubwa wa fikra zako, nawashauri na wenzangu ktk mjadala huu kuuwelewa haya mawazo yako Asante sana,
Tanzania tunahitaji vichwa kama vyako ili tuendelee.
 
Nimekuelewa naomba mfano wa nchi 2 tu zilizofaulu ku exercise ujamaa kwa muda mrefu na ziko imara kiuchumi lakini pia WANANCHI wako huru na maisha BORA kwa kuwalinganisha na majirani zake walio kwenye Capitalism ? natanguliza shukran

Hauwezi kuendesha mfumo wa ujamaa alafu wananchi wako wakawa huru. Lakini sababu kubwa ya mfumo wa kijaa kushindwa kuyasaidia mataifa mengi kuendelea ni kutokana na vita baridi iliyojitokeza, kama makabaila yangekubali kuwa makabaila na yakaendelea kushirikiana na wajamaa tungeweza kupata kipimo kizuri cha ufanisi wa mifumo yote.

Ukumbuke baada ya vita kuu ya pili ya dunia, ni kama vile dunia ilitikiswa na utajiri wote wa dunia ukahamia marekeani, Marekani ikawa na uchumi mkubwa nadhani kuliko maeneo mengine yote duniani kwa ujumla, sasa ikaanzisha mashirika ya kuzuia sera za kijamaa zisishamiri, Marekani na washirika wake wa ulaya wakawa ndio vyanzo vya elimu na maarifa vya dunia nzima, wakaizuia misingi ya kijamaa isimee kuanzia vichwani mpaka kwenye utekelezaji, dola zikaangushwa na watu wengi kuuwawa.

Wachina walielewa mapema, walifunga mipaka yao, sisi tulioendelea kuacha wazi mipaka yetu ya kifikra na kibiashara tukaishia kupambana na IMF na World Bank.

Lakini ukitaka mifano miwili ntakupatia.
1. UCHINA
2. VENEZUELA.
 
Ujamaa ni mfumo dhaifu sana, usio na tija na unaofifisha ubunifu na vipaji. Ujamaa hautoi fursa kwa mtu kutumia maarifa yake kikamilifu. Ujamaa ni mfumo usioweza kutofautisha mtu anayejituma dhidi ya mvivu.
Tanzania kufuata mfumo huo kwa miaka zaidi ya 20 ilikuwa ni kupotea tena vibaya. Na ni kweli tulipotea sana. Watu hatimaye wakawa wanafanya kazi ili mradi tu.. maana hata akifanya kidogo, matokeo ni sawa na aliyefanya sana..

Baada ya kujiingiza katika mfumo haram wa kijamaa tena kwa miaka mingi, Tz itaendelea kulipa kwa gharama kubwa sana na kwa miaka mingi ijayo.. athali za ujamaa ambazo ni wazi zinatukula kutokea ndani ni kama hizi:

1. Utegemezi wa kutisha
Amini usiamini, watanzania wengi zaidi ya 90% ni tegemezi kwa ndugu, jamaa au wazazi wao. Maana yake ni kwamba watanzania hawa hawazalishi mali ya maana ya kuweza kuwategemeza wao kikamilifu. Hali ni mbaya sana maana watz mchango wao kwa uchumi wa nchi ni kidogo sana. Kwa hiyo mzigo mkubwa uko juu ya mabega ya watu wachache sana.

2. Ufisadi na kukosa uaminifu
Sifa moja wapo ya ujamaa ni mgawanyo sawa.. baina ya waliofanya kazi sana na waliofanya kidogo. Ilipokuja suala la wafanya kazi wa umma kulipwa kidogo wakati ndio wanajuwa pesa zilipo.. likaibuka wimbi la wizi na rushwa katika sekta za umma zote. Mtakubaliana na mimi kwa kiasi fulani, tatizo moja kubwa hapa nchini ni ufisadi.. mara kagoda, epa, escrow, nk nk. Madudu kama haya yamesababisha mara nyingi sekta ya umma kuzorota, zikigubikwa na madeni makubwa na mashauri mahakamani yasiyoisha.. rejea trc, tanesco, ttcl, stamico etc zinavyopata shida

3. Kuharibiwa kwa sekta binafsi
Wajamaa ni watu wenye wivu na maendeleo ya mtu mmoja mmoja.. wajamaa wanaamini kwenye usawa wa umaskini badala ya usawa katika ukwasi. Wakiona mtu anarlekea kuwa tajiri kutokana na bidii zake binafsi, utasikia fitina zimeanza, mara uhujumu mara magendo.. upuuzi mtupu. Ni wazi sekta ya umma ina mauza uza yake linapokuja suala la uzalishaji mali au utoaji huduma. Hapa nchini sheria nyingi zilizoanzisha sekta ya umma zimejaa ukiritimba wa ajabu.. kiasi cha kuzifanya sekta ya umma kukosa tija. Ombwe hili lingeweza kufidiwa na sekta binafsi iwapo ingepewa kipaumbele. Katika ujamaa wa kiwango duni, sekta binafsi imebaki mateka, kiasi cha kufanya mchango wake kuwa kidogo. Hii ni sekta ambayo watu wengi wangeshiriki kuzalisha mali na kutoa huduma. Sekta hii baada ya kuzubaishwa, haikui, haiajiri, na serikali haipati pesa kutokana na kodi ambayo ingelipwa.
Serikali ya awam ya tano inaendelea kufanya makosa makubwa kuamini tena ujamaa duni, huku ikijua kuwa ujamaa haujawahi kushinda.
Mkuu umeadika vyema kabisa. .Rejea kisa cha Said Mwawindi na Dr kleruu yote uliyoyaelezea yanapatikana katika kisa hicho kilichotokea huko Ismani Iringa.
 
Nashindwa kuelewa uliposimamia mkuu...

Ina maana ujamaa ulitakiwa upewe nafasi ukomae bila usumbufu kutoka kwa wale wanaoamini mfumo mwingine wa kibepari!???

Kuonesha ubora wake ujamaa ulitakiwa kuthibitisha uwezo wake na kushinda hila zozote zilizoletwa na ubepari...hivyo kufeli kwake kunaweza kuonesha ni kama mfumo dhaifu usio na tija!!!
Hauwezi kuendesha mfumo wa ujamaa alafu wananchi wako wakawa huru. Lakini sababu kubwa ya mfumo wa kijaa kushindwa kuyasaidia mataifa mengi kuendelea ni kutokana na vita baridi iliyojitokeza, kama makabaila yangekubali kuwa makabaila na yakaendelea kushirikiana na wajamaa tungeweza kupata kipimo kizuri cha ufanisi wa mifumo yote.

Ukumbuke baada ya vita kuu ya pili ya dunia, ni kama vile dunia ilitikiswa na utajiri wote wa dunia ukahamia marekeani, Marekani ikawa na uchumi mkubwa nadhani kuliko maeneo mengine yote duniani kwa ujumla, sasa ikaanzisha mashirika ya kuzuia sera za kijamaa zisishamiri, Marekani na washirika wake wa ulaya wakawa ndio vyanzo vya elimu na maarifa vya dunia nzima, wakaizuia misingi ya kijamaa isimee kuanzia vichwani mpaka kwenye utekelezaji, dola zikaangushwa na watu wengi kuuwawa.

Wachina walielewa mapema, walifunga mipaka yao, sisi tulioendelea kuacha wazi mipaka yetu ya kifikra na kibiashara tukaishia kupambana na IMF na World Bank.

Lakini ukitaka mifano miwili ntakupatia.
1. UCHINA
2. VENEZUELA.
 
Si kwamba asili ya mwanadamu ni ubinafsi!??

Je unaweza kuthibitisha kuwa ubinafsi hutokana na malezi tuliyolelewa na Si vinginevyo!!!
Fikra ya binadamu ni kitu ambacho kinatengenezeka kufuatana na mazingira au malezi. Wewe ni mbinafsi kutokana na malezi uliyolelewa na si vinginevyo.
 
Naamini kabisa japo sina reference kuwa Socialism na Communalism ni DINI kama uislam na ukristo.

Nyerere alishindwa kufanya maamuzi ya kutumia nguvu kubwa ya hata kuuwa watu waliotaka kumpindua, nikwa vile alikuwa mkatoliki..ana chembe ya kuamini MUNGU yupo.

Maendeleo yoyote yale yanakafara, tena kafara KUBWA,KUBWA SANA. China na Russia nasikia hakuna ukristo wala uislam, hapo mungu wao ni aliyemadarakani, wakiamua kwenda mbele hakuna kuwaza mara mbilimbili.

Africa tungeendelea kama nchi hii ingeshikwa na viongozi wa kijeshi, sio hawa wa kiraia...tatizo ni uongozi sio mfumo.
Ungepata raha gani kuishi ktk nchi ya kipumbavu ambayo rais ndiye mungu kama China,Russia,n.Korea na takataka nyinginezo,,heri tz maskini kuliko China,Russia na jehanam nyinginezo
 
Back
Top Bottom