Mnazareth
JF-Expert Member
- Dec 4, 2017
- 3,474
- 7,401
Habari Wanajamvi! ! Nina imani tunaendelea vyema katika shughuli za uzalishaji Mali, natamani tutumie nafasi mujaraab tuzipatazo kuzidi kuweka udadisi kuhusu suala zima la "Ukomunist"ama " Ujamaa";Wazungu hapa wangeweza kusema Socialism na Communism Theory na hususani jinsi ulivyoshindwa kufanikiwa Dunia hii yetu wanayoita ya tatu.
Kujadili suala pana hili lazima tuchimbe chimbuko halisi la Ujamaaa kama nadharia ;Hapa ndipo tunapokutana na watu kariba ya Karl Mar na Friedrich Engels hawa walikuwa waanzilishi wa Socialism theory duniani miaka ya 1830s .
Hawa waliamini kuwa duniani kuna matabaka kati ya walio nacho na wasio nacho( Proletariat na bourgeoisie ) waliamini jamii ili iendelee lazima kuwe na usawa kati ya walionacho na wasio nacho..Waliamini kuwa nadharia hii ingeweza kuleta maendeleo katika uchumi kwa hali ya juu.
Soviet union,Cuba,China, East Germany ni kati ya Mataifa yaliyohubiri na kujaribu kuifuata nadharia ya Socialism duniani na kweli kabisa nchi kama USSR mnamo mwaka 1917, Cuba mnamo mwaka 1959,China mnamo mwaka 1949 nchi hzi zote zilipata uhuru wake baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea kwenye nchi zao na kuamua kufuata sera za kikomunist.
Katika nchi za Afrika ambazo nyingi zilipata uhuru wake katika miaka ya 60..Nchi nyingi ziliamua kufuata sera za kijamaa ambazo msingi wake ulijikita katika maisha ya kijima yaliyokuwepo kabla ya uwepo wa ukoloni ambapo watu wake waliishi kijamaa na kusaidiana katika shida na raha...
Viongozi mahiri kama Julius Nyerere,Kwame Nkhrumah,Tom Mboya ni baadhi tu ya Viongozi waliofuata sera za kikomunist ili ziongoze kwenye uchumi na maendeleo kiujumla..Tanzania chini ya mwalimu Nyerere alitambulisha sera yake ya Ujamaa na kujitegemea na kufanikiwa kuweka azimio la Arusha mnamo mwaka 1967..Hapa tunaona jinsi alivyoweza kuifanya Serikali iwe mmiliki mkuu wa uchumi na kusababisha kutokuwepo ushindani katika biashara na kupingana wazi na sera za kibeberu za soko huria.
Pamoja na yote tunaona jinsi gani nchi zilizofuata mlengo wa kijamaa zinavyofeli katika kuendeleza uchumi wake na mifano hai tunaona jinsi Tanzania ilivyoamua kufuata soko huria na kuingia kwenye ubinafsishaji rejea SAP (Structural adjustment policy ya mwanzoni mwa miaka ya 80 ambayo ilitoa fursa ya ushindani wa masoko,biashara,uwekezaji na kuboresha maendeleo ya viwanda!!!
Tunaona tena Socialism inakataa Ghana na mwishowe Kwame Nkhrumah anapinduliwa mnamo mwaka 1966...Napenda sote kwa Pamoja tuangalie ni vipi ama kwanini hizi nadharia zilishindwa kabisa Afrika ilhali wenzetu kutoka Ulaya na Asia kama China walikuwa na mlengo sawa na nchi za kiafriaka walifanikiwa???
Pamoja na kuwa Socialism ilionekana kama imeshakufa lakini nchi nyingi za Ulaya hazikukubali kufa nayo na mifano ya nchi zilizoinuka tena ni USSR,Germany,Cuba na China ,Vietnam na nyinginezo nyingi ambazo zilifanya mapinduzi makubwa ya kiuchumi...
Labda tuangalie China ni vipi iliweza kuinuka tena ilhali kiongozi wao wa Kikomunist bwana "Mao Tse Tung alifariki dunia!??Tukumbuke pia kulikuwa na vita nyingi baridi baina yao!!
Deng Xiaoping kiongozi wa Kikomunist nchini China kati ya mwaka 1978-1989 ndiye anasemekana kama aliyefanya mapinduzi makubwa ya kiuchumi na kuruhusu ushindani wa viwanda...Napata ukakasi je tatizo ni Viongozi!!? ama tatizo ni elimu???
Kipi kilikuwa kigumu kwa Viongozi wetu kujua kuwa binadamu asili yake ni ubinafsi na si Ujamaa!!!Ama tatizo lilikuwa elimu! ?japo pia kuna ukakasi sababu tulikuwa na watu kama Justinian Rweyemamu nchini Tanzanian ambaye yeye na wenzake walikuwa wabobezi wa masuala ya uchumi na walielewa fika madhara ya kukumbatia..
Je ni kweli hzi nadharia ndizo zilizotufikisha hapa na kuonekana dunia ya tatu,nchi maskini na tusioweza kujiendesha wenyewe.!?
Ama Labda ni asili yetu Afrika kuwa maskini ikiwa na Maana huwezi kutenga umasikini na Afrika!!!Sitaki kuamini kuwa rushwa pekee ndiyo chanzo cha maendeleo yetu .
Kama ukoloni uliacha doa kubwa Afrika tulipaswa kujikwamua katika hiyo hali tukumbuke kuwa hata China alishawahi kutawaliwa na Japan kwa miaka mingi! !!
Wapi Tumekosea! ?Tubadilishe tena mfumo au turudi kwenye asili yetu UJIMA!?