Je, Upo uhusiano wa anguko la Socialism ama Ukomunist Afrika na umasikini unaokumba nchi nyingi Afrika!?

M

Mnazareth

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2017
Messages
1,118
Points
2,000
M

Mnazareth

JF-Expert Member
Joined Dec 4, 2017
1,118 2,000
Habari Wanajamvi! ! Nina imani tunaendelea vyema katika shughuli za uzalishaji Mali, natamani tutumie nafasi mujaraab tuzipatazo kuzidi kuweka udadisi kuhusu suala zima la "Ukomunist"ama " Ujamaa";Wazungu hapa wangeweza kusema Socialism na Communism Theory na hususani jinsi ulivyoshindwa kufanikiwa Dunia hii yetu wanayoita ya tatu.

Kujadili suala pana hili lazima tuchimbe chimbuko halisi la Ujamaaa kama nadharia ;Hapa ndipo tunapokutana na watu kariba ya Karl Mar na Friedrich Engels hawa walikuwa waanzilishi wa Socialism theory duniani miaka ya 1830s .

Hawa waliamini kuwa duniani kuna matabaka kati ya walio nacho na wasio nacho( Proletariat na bourgeoisie ) waliamini jamii ili iendelee lazima kuwe na usawa kati ya walionacho na wasio nacho..Waliamini kuwa nadharia hii ingeweza kuleta maendeleo katika uchumi kwa hali ya juu.

Soviet union,Cuba,China, East Germany ni kati ya Mataifa yaliyohubiri na kujaribu kuifuata nadharia ya Socialism duniani na kweli kabisa nchi kama USSR mnamo mwaka 1917, Cuba mnamo mwaka 1959,China mnamo mwaka 1949 nchi hzi zote zilipata uhuru wake baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea kwenye nchi zao na kuamua kufuata sera za kikomunist.

Katika nchi za Afrika ambazo nyingi zilipata uhuru wake katika miaka ya 60..Nchi nyingi ziliamua kufuata sera za kijamaa ambazo msingi wake ulijikita katika maisha ya kijima yaliyokuwepo kabla ya uwepo wa ukoloni ambapo watu wake waliishi kijamaa na kusaidiana katika shida na raha...

Viongozi mahiri kama Julius Nyerere,Kwame Nkhrumah,Tom Mboya ni baadhi tu ya Viongozi waliofuata sera za kikomunist ili ziongoze kwenye uchumi na maendeleo kiujumla..Tanzania chini ya mwalimu Nyerere alitambulisha sera yake ya Ujamaa na kujitegemea na kufanikiwa kuweka azimio la Arusha mnamo mwaka 1967..Hapa tunaona jinsi alivyoweza kuifanya Serikali iwe mmiliki mkuu wa uchumi na kusababisha kutokuwepo ushindani katika biashara na kupingana wazi na sera za kibeberu za soko huria.

Pamoja na yote tunaona jinsi gani nchi zilizofuata mlengo wa kijamaa zinavyofeli katika kuendeleza uchumi wake na mifano hai tunaona jinsi Tanzania ilivyoamua kufuata soko huria na kuingia kwenye ubinafsishaji rejea SAP (Structural adjustment policy ya mwanzoni mwa miaka ya 80 ambayo ilitoa fursa ya ushindani wa masoko,biashara,uwekezaji na kuboresha maendeleo ya viwanda!!!

Tunaona tena Socialism inakataa Ghana na mwishowe Kwame Nkhrumah anapinduliwa mnamo mwaka 1966...Napenda sote kwa Pamoja tuangalie ni vipi ama kwanini hizi nadharia zilishindwa kabisa Afrika ilhali wenzetu kutoka Ulaya na Asia kama China walikuwa na mlengo sawa na nchi za kiafriaka walifanikiwa???

Pamoja na kuwa Socialism ilionekana kama imeshakufa lakini nchi nyingi za Ulaya hazikukubali kufa nayo na mifano ya nchi zilizoinuka tena ni USSR,Germany,Cuba na China ,Vietnam na nyinginezo nyingi ambazo zilifanya mapinduzi makubwa ya kiuchumi...

Labda tuangalie China ni vipi iliweza kuinuka tena ilhali kiongozi wao wa Kikomunist bwana "Mao Tse Tung alifariki dunia!??Tukumbuke pia kulikuwa na vita nyingi baridi baina yao!!

Deng Xiaoping kiongozi wa Kikomunist nchini China kati ya mwaka 1978-1989 ndiye anasemekana kama aliyefanya mapinduzi makubwa ya kiuchumi na kuruhusu ushindani wa viwanda...Napata ukakasi je tatizo ni Viongozi!!? ama tatizo ni elimu???

Kipi kilikuwa kigumu kwa Viongozi wetu kujua kuwa binadamu asili yake ni ubinafsi na si Ujamaa!!!Ama tatizo lilikuwa elimu! ?japo pia kuna ukakasi sababu tulikuwa na watu kama Justinian Rweyemamu nchini Tanzanian ambaye yeye na wenzake walikuwa wabobezi wa masuala ya uchumi na walielewa fika madhara ya kukumbatia..

Je ni kweli hzi nadharia ndizo zilizotufikisha hapa na kuonekana dunia ya tatu,nchi maskini na tusioweza kujiendesha wenyewe.!?

Ama Labda ni asili yetu Afrika kuwa maskini ikiwa na Maana huwezi kutenga umasikini na Afrika!!!Sitaki kuamini kuwa rushwa pekee ndiyo chanzo cha maendeleo yetu .

Kama ukoloni uliacha doa kubwa Afrika tulipaswa kujikwamua katika hiyo hali tukumbuke kuwa hata China alishawahi kutawaliwa na Japan kwa miaka mingi! !!

Wapi Tumekosea! ?Tubadilishe tena mfumo au turudi kwenye asili yetu UJIMA!?
 
Loeb S Mpalasinge

Loeb S Mpalasinge

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2013
Messages
1,116
Points
2,000
Loeb S Mpalasinge

Loeb S Mpalasinge

JF-Expert Member
Joined Dec 1, 2013
1,116 2,000
Upo uhusiano mkubwa tu,,wabepari walijitahidi kwa hali na mali wauangushe ujamaa ili wao mfumo wao wa kinyonyaji uchukue nafasi.Kwa hio katika kuupiga vita mfumo wa kijamaa hata nchi changa kama Tz,Ghana nk zilizokuwa zikijiimarisha ktk mfumo huu zilijikuta nazo kwenye Wakati mgumu,,,na kwa sababu mfumo huu ulihitaji viongozi jasiri sana ili kupiga hatua naweza sema huku Africa hawakuwepo..Mao wa China wakati akitawala walikufa watu 30ml kwa ajili ya kuadopt sera na mabadiliko mbalimbali ili kufikia malengo, Joseph Stalin mpaka unaona Urusi Imekuwa industrial cauntry walikufa watu 25ml

Niulize kwa mwalimu Nyerere,,aliogopa nini kuwanyonga watu waliotaka kumpindua karibia mara tatu ili kujenga nidhamu,,,??
Tuchukulie North Korea ni nani atakaethubutu kuplani mapinduzi ama kwa uchache kuhoji supremacy ya Chairman Kim Jong un?
Utaona viongozi wa kijamaa hawakutakiwa kufanana na padri.

Leo north Korea wanaexpot vifaa vya umeme vinavyokubalika hadi Europe
Vyenye nembo ya ce,,na vipo hadi tz

Kama Mwalimu angeamua kwa thati kuusimamia huu mfumo kwa usahihi leo tungekuwa tofauti na nchi zote za Africa.
 
Loeb S Mpalasinge

Loeb S Mpalasinge

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2013
Messages
1,116
Points
2,000
Loeb S Mpalasinge

Loeb S Mpalasinge

JF-Expert Member
Joined Dec 1, 2013
1,116 2,000
China inakuwa kwa kasi sana lakini wameadopt sera chache za kibepari ila bado namna yao ya ujamaa walioanza nao kama msingi hawajaitupa..Mimi huwa najiuliza maswali mengi saa nyingine..Tunauza uranium nyingi tulio nayo kama raw material,,,halafu tunatenga zaidi ya 7trillion kuchimba na kutengeneza power plant huko stiegler gorge,,,hivi nuclear reactor tukiwapa tender wachina moja wataitengeneza kwa tsh ngapi?
Maana uingereza kawapa wachina kazi kama hio?
Na tuna raw material za uranium nyingi sana.

Hivi watu wa ruvuma wangeenda nchi zilizoendelea wakaona kazi ya makaa ya mawe na uranium kwenye kuzalisha umeme na wakajipima jinsi walivyo na haya material mengi na wanaishi gizani si wangehama hii nchi.

Mfumo wa ujamaa tz ulikufa na kuna mtu wa kumlaumu.
 
Je unafikiri kuwa Ujamaa wa Mwalimu nyerere ulikuwa na nafasi ya kuleta mapinduzi ya viwanda Tanzania!?
 
Tulaumu uongozi mbovu!!!hii ni Kwa mujibu wa maelezo yako.
 
dolomon

dolomon

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2018
Messages
382
Points
1,000
dolomon

dolomon

JF-Expert Member
Joined Jun 5, 2018
382 1,000
Upo uhusiano mkubwa tu,,wabepari walijitahidi kwa hali na mali wauangushe ujamaa ili wao mfumo wao wa kinyonyaji uchukue nafasi.Kwa hio katika kuupiga vita mfumo wa kijamaa hata nchi changa kama Tz,Ghana nk zilizokuwa zikijiimarisha ktk mfumo huu zilijikuta nazo kwenye Wakati mgumu,,,na kwa sababu mfumo huu ulihitaji viongozi jasiri sana ili kupiga hatua naweza sema huku Africa hawakuwepo..Mao wa China wakati akitawala walikufa watu 30ml kwa ajili ya kuadopt sera na mabadiliko mbalimbali ili kufikia malengo, Joseph Stalin mpaka unaona Urusi Imekuwa industrial cauntry walikufa watu 25ml

Niulize kwa mwalimu Nyerere,,aliogopa nini kuwanyonga watu waliotaka kumpindua karibia mara tatu ili kujenga nidhamu,,,??
Tuchukulie North Korea ni nani atakaethubutu kuplani mapinduzi ama kwa uchache kuhoji supremacy ya Chairman Kim Jong un?
Utaona viongozi wa kijamaa hawakutakiwa kufanana na padri.

Leo north Korea wanaexpot vifaa vya umeme vinavyokubalika hadi Europe
Vyenye nembo ya ce,,na vipo hadi tz

Kama Mwalimu angeamua kwa thati kuusimamia huu mfumo kwa usahihi leo tungekuwa tofauti na nchi zote za Africa.
Naamini kabisa japo sina reference kuwa Socialism na Communalism ni DINI kama uislam na ukristo.

Nyerere alishindwa kufanya maamuzi ya kutumia nguvu kubwa ya hata kuuwa watu waliotaka kumpindua, nikwa vile alikuwa mkatoliki..ana chembe ya kuamini MUNGU yupo.

Maendeleo yoyote yale yanakafara, tena kafara KUBWA,KUBWA SANA. China na Russia nasikia hakuna ukristo wala uislam, hapo mungu wao ni aliyemadarakani, wakiamua kwenda mbele hakuna kuwaza mara mbilimbili.

Africa tungeendelea kama nchi hii ingeshikwa na viongozi wa kijeshi, sio hawa wa kiraia...tatizo ni uongozi sio mfumo.
 
Loeb S Mpalasinge

Loeb S Mpalasinge

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2013
Messages
1,116
Points
2,000
Loeb S Mpalasinge

Loeb S Mpalasinge

JF-Expert Member
Joined Dec 1, 2013
1,116 2,000
Viwanda vilikuwepo tayari na kukaanzishwa vyuo kwa ajili ya kuzalisha watendaji mf technician na baadhi walimu walikuwa wametokea mataifa ya kijamaa mfano urusi.
Bado mtaala wa elimu Ulikuwa mzuri sana.Kwa hio kama sio waendeshaji wa hivi viwanda kutokuwa na nidhamu hasa kutokana na kutokuwa na punishment kali toka uongozi wa juu, leo vingekuwepo vingi tu.Angalia magofu ya viwanda na magodown nchi nzima hata Huwezi yahesabu.Haya yametokana na sababu nyingi tu lakini leo tungekuwa tofauti na nchi yoyote ya afrika.
Je unafikiri kuwa Ujamaa wa Mwalimu nyerere ulikuwa na nafasi ya kuleta mapinduzi ya viwanda Tanzania!?
 
M

Mnazareth

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2017
Messages
1,118
Points
2,000
M

Mnazareth

JF-Expert Member
Joined Dec 4, 2017
1,118 2,000
Naamini kabisa japo sina reference kuwa Socialism na Communalism ni DINI kama uislam na ukristo.

Nyerere alishindwa kufanya maamuzi ya kutumia nguvu kubwa ya hata kuuwa watu waliotaka kumpindua, nikwa vile alikuwa mkatoliki..ana chembe ya kuamini MUNGU yupo.

Maendeleo yoyote yale yanakafara, tena kafara KUBWA,KUBWA SANA. China na Russia nasikia hakuna ukristo wala uislam, hapo mungu wao ni aliyemadarakani, wakiamua kwenda mbele hakuna kuwaza mara mbilimbili.

Africa tungeendelea kama nchi hii ingeshikwa na viongozi wa kijeshi, sio hawa wa kiraia...tatizo ni uongozi sio mfumo.
Si vibaya kuamini hivyo ila nakuhakikishia Socialism ama ujamaa kama alivyouita Mwalimu Nyerere si dini bali nadharia ambayo ilipata waamini wengi na kuiabudu... kwa uichoandika umeonesha wazi kuwa ili kueneza nadharia hzi lazima nguvu kubwa itumike.

Labda tu niseme Socialism haina uhalisia katika maisha ya binadamu na ndio maana ilitumika nguvu kubwa kuieneza .
 
S

Silicon Valley

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2012
Messages
795
Points
1,000
S

Silicon Valley

JF-Expert Member
Joined Mar 6, 2012
795 1,000
Socialism au ujamaa hauna mafanikio kimaendeleo ya muda mrefu kwa kulinganisha na capitalism au ubepari, la maana hapa Commitment ya capitalists ipo juu kuliko Socialism.

Kwa dunia ya leo kama mtu hajaliona hilo atakuwa aidha anamapungufu kiakili/ki saikolojia, exposure au upungufu wa elimu.

Hata hiyo china wanaisifia wapate nafasi ya kuitembelea tu, kama ni magofu ya viwanda vya umama yamejaa utaogopa, kiuchumi mtu asikudanganye kwamba china n inchi ya ujamaa uongo japo bado yapo masalia machache sana ya mashirika ya umma au viwanda ambavyo wana exploit wafanyakazi wao maskini cheap labour.

China ninayoijua naweza sema (Wananchi maskini katika maisha duni wakimiliki serikali tajiri sana ulimwenguni) wananchi wa china ni koloni la serikali ya china,

Maendeleo na utajiri wa china ni wa serikali/umma sio mwananchi japo huduma umma ziko juu sana kwa maana mabarabara hospitals, airports, Infrastructures zote

Jambo lingine la Muhimu sana kulitambua penye mjadala kama huu ni vema kutambua kuwa kila mfumo wa uchumi lazima una mazuri na mabaya yake ndani ya jamii husika.
Kwa maana hiyo usitegemee jamii inayonufaika na ujamaa (waliosoma shule za bure na family nzima ikaneemeka) hata siku moja hawezi sifia ubepari, au jamii iliyoteseka au kufilisiwa au kunyang'anya mali zao tokana na ujamaa hawawezi sifia ujamaa

Maoni yangu bora capitalist 10x kuliko ujamaa, kila mmoja kula jasho lake halali
 
Loeb S Mpalasinge

Loeb S Mpalasinge

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2013
Messages
1,116
Points
2,000
Loeb S Mpalasinge

Loeb S Mpalasinge

JF-Expert Member
Joined Dec 1, 2013
1,116 2,000
Nitarejea baadhi ya maandiko yako kipengele cha nne na cha tano
Kwamba wananchi wa china ni koloni la nchi yao na pia kwamba serikali ya china inamiliki utajiri wote wa nchi,,hapa umeongelea ujamaa kwa mantiki ya serikali kuu ndio humiliki njia zote za uchumi..Huu ndio ujamaa.ila katika version iliokuwa modified ndio China walio nao sasa.

Naomba Nikuulize swali kwa nini marekani u imeziwekea nchi zote za kijamaa vikwazo vya Kiuchumi? Wanahofia nini?

Je ubora wa ubepari (capitalism) ni upi katika nchi nyingi za Africa zilizouadopt?
Socialism au ujamaa hauna mafanikio kimaendeleo ya muda mrefu kwa kulinganisha na capitalism au ubepari, la maana hapa Commitment ya capitalists ipo juu kuliko Socialism.

Kwa dunia ya leo kama mtu hajaliona hilo atakuwa aidha anamapungufu kiakili/ki saikolojia, exposure au upungufu wa elimu.

Hata hiyo china wanaisifia wapate nafasi ya kuitembelea tu, kama ni magofu ya viwanda vya umama yamejaa utaogopa, kiuchumi mtu asikudanganye kwamba china n inchi ya ujamaa uongo japo bado yapo masalia machache sana ya mashirika ya umma au viwanda ambavyo wana exploit wafanyakazi wao maskini cheap labour.

China ninayoijua naweza sema (Wananchi maskini katika maisha duni wakimiliki serikali tajiri sana ulimwenguni) wananchi wa china ni koloni la serikali ya china,

Maendeleo na utajiri wa china ni wa serikali/umma sio mwananchi japo huduma umma ziko juu sana kwa maana mabarabara hospitals, airports, Infrastructures zote

Jambo lingine la Muhimu sana kulitambua penye mjadala kama huu ni vema kutambua kuwa kila mfumo wa uchumi lazima una mazuri na mabaya yake ndani ya jamii husika.
Kwa maana hiyo usitegemee jamii inayonufaika na ujamaa (waliosoma shule za bure na family nzima ikaneemeka) hata siku moja hawezi sifia ubepari, au jamii iliyoteseka au kufilisiwa au kunyang'anya mali zao tokana na ujamaa hawawezi sifia ujamaa

Maoni yangu bora capitalist 10x kuliko ujamaa, kila mmoja kula jasho lake halali
 
M

Mnazareth

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2017
Messages
1,118
Points
2,000
M

Mnazareth

JF-Expert Member
Joined Dec 4, 2017
1,118 2,000
Socialism au ujamaa hauna mafanikio kimaendeleo ya muda mrefu kwa kulinganisha na capitalism au ubepari, la maana hapa Commitment ya capitalists ipo juu kuliko Socialism.

Kwa dunia ya leo kama mtu hajaliona hilo atakuwa aidha anamapungufu kiakili/ki saikolojia, exposure au upungufu wa elimu.

Hata hiyo china wanaisifia wapate nafasi ya kuitembelea tu, kama ni magofu ya viwanda vya umama yamejaa utaogopa, kiuchumi mtu asikudanganye kwamba china n inchi ya ujamaa uongo japo bado yapo masalia machache sana ya mashirika ya umma au viwanda ambavyo wana exploit wafanyakazi wao maskini cheap labour.

China ninayoijua naweza sema (Wananchi maskini katika maisha duni wakimiliki serikali tajiri sana ulimwenguni) wananchi wa china ni koloni la serikali ya china,

Maendeleo na utajiri wa china ni wa serikali/umma sio mwananchi japo huduma umma ziko juu sana kwa maana mabarabara hospitals, airports, Infrastructures zote

Jambo lingine la Muhimu sana kulitambua penye mjadala kama huu ni vema kutambua kuwa kila mfumo wa uchumi lazima una mazuri na mabaya yake ndani ya jamii husika.
Kwa maana hiyo usitegemee jamii inayonufaika na ujamaa (waliosoma shule za bure na family nzima ikaneemeka) hata siku moja hawezi sifia ubepari, au jamii iliyoteseka au kufilisiwa au kunyang'anya mali zao tokana na ujamaa hawawezi sifia ujamaa

Maoni yangu bora capitalist 10x kuliko ujamaa, kila mmoja kula jasho lake halali
Mkuu umeandika vyema sana...Ni kweli hakuna mfumo wa uchumi ulioonekana bora zaidi ya" Ubepari"
Umewahi kujiuliza kwa nini Capitalism ni mfumo wenye nguvu???

Kwa mujibu wa mwanafalsafa nguli "Plato "anasema asili ya mwanadamu ni ubinafsi yani kujijali kwanza yeye kabla ya wengine! !!na hili ni jambo la kweli na halisia..

Kinyume na Socialism ambayo ilienda Kinyume na asili ya mwanadamu!!

Kuhusu China ni wazi Ukomunist kwao haukuwa mfumo wao kiuchumi bali mtindo wao wa maisha na ndio mana ilikuwa rahisi kwao kuendelea na mfumo wa viwanda.
 
Bulaya001

Bulaya001

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2018
Messages
3,923
Points
2,000
Bulaya001

Bulaya001

JF-Expert Member
Joined Dec 21, 2018
3,923 2,000
Ili Africa iweze kujikwamua ktk hili janga, naona ni bora turudi utumwani tena maana ni heri utawaliwe na mzungu anaekupa elimu bora, maji na tiba safi kuliko hawa wachumia tumbo.
 
Pendael24

Pendael24

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2014
Messages
2,373
Points
2,000
Pendael24

Pendael24

JF-Expert Member
Joined Feb 13, 2014
2,373 2,000
Kusema ukweli katika hali ya kawaida ujamaa nafasi yake ni ndogo sana katika akili na fikra za binadamu
kama walivyotangulia kusema hapo juu kwamba mwanadamu asili yake ni ubinafsi, nami naongezea wivu uchoyo na uvivu.
kwa sababu hio ilikua ni ngumu sana kuendelea na ujamaa vinginevyo ingehitajika garama kubwa sana ya maisha ya watu.
najaribu kufikiria jinsi ulimwengu ulivyoundika kwa kanuni, na kila kilicho ndani yake kiko kikanuni. ukijaribu kukiuka kanuni hizo ulimwengu utakinzana nawe.
kwa maana hio basi mwanadamu nae ni sehemu ya ulimwengu yupo kikanuni, na kanuni mojawapo ni hio kuwa mbinafsi.
wakati huo huo ujamaa una kanuni zake ambazo ni kinyume na ubinafsi.
kwa hio kusingekua na namna yoyote ya kufanikiwa kwa ujamaa nje ya mauaji makubwa ya watu. ndio mtazamo wangu kwa hili.
 
Mkuu Pamoja na kwamba binadamu ana asili lakini binadamu anabadilika kutokana na mazingira na changamoto hata ukimweka mtoto mdogo wa binadamu akae porini na nyani au ngiri atafanana nao kitabia na matendo.Iweje kuadopt mfumo ulioasisiwa na binadamu mwenye akili kama sisi?
Kusema ukweli katika hali ya kawaida ujamaa nafasi yake ni ndogo sana katika akili na fikra za binadamu
kama walivyotangulia kusema hapo juu kwamba mwanadamu asili yake ni ubinafsi, nami naongezea wivu uchoyo na uvivu.
kwa sababu hio ilikua ni ngumu sana kuendelea na ujamaa vinginevyo ingehitajika garama kubwa sana ya maisha ya watu.
najaribu kufikiria jinsi ulimwengu ulivyoundika kwa kanuni, na kila kilicho ndani yake kiko kikanuni. ukijaribu kukiuka kanuni hizo ulimwengu utakinzana nawe.
kwa maana hio basi mwanadamu nae ni sehemu ya ulimwengu yupo kikanuni, na kanuni mojawapo ni hio kuwa mbinafsi.
wakati huo huo ujamaa una kanuni zake ambazo ni kinyume na ubinafsi.
kwa hio kusingekua na namna yoyote ya kufanikiwa kwa ujamaa nje ya mauaji makubwa ya watu. ndio mtazamo wangu kwa hili.
 
Loeb S Mpalasinge

Loeb S Mpalasinge

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2013
Messages
1,116
Points
2,000
Loeb S Mpalasinge

Loeb S Mpalasinge

JF-Expert Member
Joined Dec 1, 2013
1,116 2,000
Kama ukiambiwa Tanzania ilikuwa na viwanda mpaka vya wembe,,tairi za baiskeli Unaweza ukashangaa maana ndio sisi hatuchoki kuongea upumbavu eti mtu mweusi hana akili hawezi kutengeneza hata wembe
kumbe viwanda vilikuwepo na vilikuwa vinazalisha.

Mara mwafrika hana akili hawezi kutengeneza hata toothpick,,hatujui tunacheza ngoma ya nani? Hatujui kwamba hao wenye kuuchukia ujamaa ndio walioua viwanda vyetu na ndio wanaosema sisi hatuna akili wala uwezo wa kujitegemea.

Hili ndio limenifanya niipende north Korea na nchi zote za kijamaa Maana wameamua kujitegemea na kuishi maisha yao.

Na kamwe North Korea asidanganyike akaachana na silaha za nyuklia.Ile ndio msingi mmojawapo wa Juche.
 
rommy shabby

rommy shabby

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2017
Messages
274
Points
250
rommy shabby

rommy shabby

JF-Expert Member
Joined Jun 26, 2017
274 250
Kiongozi mm nakuelewa sn sn sn kwel kabisa walioukataa umoja ndo hao hao wakaja na maneno mengi ya kutudhihaki, hua napenda sn maisha ya wanaharakati kama guevara, chavezi na lumumba hawa watu kweli walikua wanaharakati wa kijamaa damu damu, dunia ipo hapa leo kutokana na sera chafuu za kunuka za ubepari, ubepari mwenywe nacho anazidi kua nacho mbaya zaidi asiyenacho anapokonywa ata hicho kdg
Kama ukiambiwa Tanzania ilikuwa na viwanda mpaka vya wembe,,tairi za baiskeli Unaweza ukashangaa maana ndio sisi hatuchoki kuongea upumbavu eti mtu mweusi hana akili hawezi kutengeneza hata wembe
kumbe viwanda vilikuwepo na vilikuwa vinazalisha.

Mara mwafrika hana akili hawezi kutengeneza hata toothpick,,hatujui tunacheza ngoma ya nani? Hatujui kwamba hao wenye kuuchukia ujamaa ndio walioua viwanda vyetu na ndio wanaosema sisi hatuna akili wala uwezo wa kujitegemea.

Hili ndio limenifanya niipende north Korea na nchi zote za kijamaa Maana wameamua kujitegemea na kuishi maisha yao.

Na kamwe North Korea asidanganyike akaachana na silaha za nyuklia.Ile ndio msingi mmojawapo wa Juche.
 
Forum statistics

Threads 1,304,173
Members 501,290
Posts 31,505,172
Top