DaveSave
JF-Expert Member
- Nov 20, 2010
- 440
- 637
Kuna makundi manne (4) ya watu wanaotengeneza pesa hapa duniani.
1. WAAJIRIWA.
Hawa ni watu ambao kimsingi wanauza muda wao almost wote wa siku nzima kwa mwajiri wao na yeye anawalipa pesa kwa kuwaambia cha kumfanyia. Kwa kuwa kanuni ya mshahara huwa ni kumlipa mtu 10% ya anachozalisha hasa kwa makampuni makubwa basi haitakaa itokee mwajiriwa kulingana kipato na mwajiri wake. Na hivyo wengi wa waajiriwa hufa maskini na watoto wao pia kuanza kutafuta maisha kivyaovyao kwa kusoma na kuja kuajiriwa pia hivyo hivyo..
Usikubali kubaki kwenye ajira unalipwa laki 5 kwa mwezi sawa na Tsh 1,850 yaani chini ya dola moja kwa saa. Ina maana umesoma mpaka chuo kikuu halafu thamani ya lisaa lako moja ni less than $1!!!!? Ndiyo maana watu wengi waliosoma sana huwa hawawezi kuwa matajiri kwa sababu wanauza muda wao kwa "bei chee" halafu siku zinazidi kuyoyoma haoni mafanikio. Huku tena ana mkopo wa gari nk. Makato na marejesho... Kwa nini usife masikini kwa style hiyo.?
2. WALIOJIAJIRI
Hawa hujitambua kidogo na kuamua kufanya kazi binafsi au kufungua biashara ndogo kama duka nk. Lakini kwa kuwa hawana pesa ya kununua muda wa watu wengine na kuwaajiri hawa nao huwa busy kutwa kucha bila mafanikio ya maana. Ana duka miaka 15 sasa halijawahi kupanuka likawa supermarket. Na mara nyingi huyu mtu akifa na biashara yake nayo humfuata. Ndo watu wanasingizia eti alikuwa na biashara za "uchawi". Kumbe shida ni kuwa kila kitu kilikuwa kinamtegemea yeye.
3. WAMILIKI WA BIASHARA KUBWA
Hawa huwa na kipato endelevu (residual income) maana amemunua muda wa watu weeengi kawaajiri halafu kawapa majukumu kwa hiyo awepo asiwepo pesa inaendelea kuingia kwake. Mfano kina Bakhressa, Mengi, Dewji, etc. Majina yao yanajulikana. Ni wachache nchi hii. Ukihesabu vidole vyako vya mikono na miguu majina yataisha kabla hujamaliza kuhesabu.
4. WAWEKEZAJI
Hawa ni watu wenye pesa nyingi zaidi na wana uwezo wa kuiwekeza mahali hata nje ya nchi ikawa inawazalishia pesa zaidi bila wao kuwepo kabisa. Hawa hata majina huwa hawajulikani
Kwa hiyo nadhani tayari wewe unajua kundi lipi upo (ama kama wewe ni mwanafunzi unaweza kuona kundi lipi unaelekea).
SASA SIKIA...
Makundi mawili ya kwanza ni makundi ya watu maskini. Mfano waajiriwa ni watu wanaotumia muda wao na nguvu na maarifa yao yote (waliyoyakusanya kwa miaka mingi ya kusoma kwa shidashida) kumtajirisha mtu kwa malipo kidogo yanayomwezesha huyu muajiriwa kulipa kodi (siyo kujenga), kula, kuvaa, kusafiri kwenda na kurudi kazini nk. Yaani basic needs tu. Maisha ya waajiriwa wengi yanafanana. Mfano ni wachache sana katika ajira ambao wamejenga nyumba zao binafsi kwa hela halali ya ajira.
Kama vile ilivyo vigumu kwa mwanafunzi kwenda chuo kwa gari lake mwenyewe alilonunua kwa pesa yake halali. Wapo wachache sana. Na hivyohivyo waajiriwa kumiliki nyumba. Wengi wamepanga. Jiulize lini utafikia hizi level especially kama utang'ang'ania ajira tu bila kujishughulisha na kitu kingine cha ziada mpaka uzeeni? Ndo unastaafu unapewa kiinua mgongo lakini miaka 7 tu baada ya hapo unakufa kwa pressure. Coz ndo unaanza kuona wengine wa umri sawa na wewe wako mbaaaali kimaisha hapo nguvu za kuhimili mikikimikiki ya biashara huna tena watoto na wajukuu hawana future unaanza kupata stress. Kisa ulikuwa ungependa kiyoyozi cha kazini. Haya, endelea kufurahia kiyoyozi ndugu. Halafu mi huwa nashangaa..yaani unajua kabisa hapo kazini kuanzia kiti, dawati, computer, kalamu, karatasi, kula kitu si cha kwako. You are just hired to use them to produce for someone else. Hebu tufunguane macho leo..
Waliojiajiri nao wako busy. Kama ana duka basi kufata mzigo yeye (hamwamini mtu), kuuza yeye, usafi yeye, kuhesabu stock yeye, ulinzi wa duka yeye ndo analinda maana analala humo humo. Kama jongoo alivyo na miguu mingi lakini spidi "kiduchu" ndivyo na huyu nae. Miguu mingi ya jongoo bila macho is equal to ZERO. Na hivyo hivyo shughuli nyingi bila maarifa is uqual to ZERO. Yaani yuko busy kila saa lakini spidi ya mafanikio ni ndogo kweli kweli. Sasa maendeleo hayaji kwa style hiyo ila kwa kuwa hajui anahisi siku moja na yeye atakuwa kama Bakhressa. Kwani Bakhressa ndo anauza ice cream za Azam? Hujiulizi?
KWA WANAFUNZI..
Bahati mbaya sana kama ni mwanafunzi uko sekondari au chuo hiyo ndo ramani ya future yako. Ukimaliza chuo lazima uingie katika makundi hayo mawili ya kimaskini hasa kundi la kwanza. Na siku hizi ajira wala usitegemee. Utafiti unaonyesha kuwa katika watu 1,200,000 wanaohitimu vyuo mbali mbali kila mwaka ni 200,000 tu wanaobahatika kupata ajira. Hao milioni moja za zaidi wanakaa huku mtaani bila ajira. Fikiria sasa itakuwaje.
HATA HIVYO.. kuna njia ya kukusaidia kuweza kuhama kutoka makundi hayo mawili kwanza na kuingia makundi mawili ya mwisho hapo juu.
Cha msingi ni Wewe kujishusha tu na kukubali kuwa unahitaji kujifunza hivi vitu. Lakini ukifikiri kuwa unajua kila kitu kuna maarifa utayakosa simply kwa kutothamini mawazo ya wengine ambao huenda ni Mungu tu anawaleta ili kukustua kidogo upate ufahamu fulani lakini wewe aaah. Umeziba maskio na pamba umeweka. Uko busy. Uko determined kufa maskini. Hebu jifunze. Itakusaidia. Kama umeajiriwa na unasoma ujumbe huu hebu jiulize ajira yako ikiisha leo ghafla PAAP!! Utaanzia wapi? Kama utaandika CV tena basi kubaliana na hali halisi tu kuwa wewe ni maskini. Huna cha kuuza kupata pesa zaidi ya muda wako.
Kumbuka rasilimali ambayo Mungu aliwagawia wanadamu wote sawa ni MUDA. 24 hours kwa kila binadamu. Matajiri wananunua muda wewe unauuza. Yaani unafanya opposite na wanachofanya matajiri halafu unasema unataka kuwa kama wao. Unanielewa? Kuna mtu maarufu duniani anaitwa William Gates III au kwa jina maarufu Bill Gates, anasema, "KAMA ULIZALIWA MASKINI HILO SIYO KOSA LAKO ILA UKIFA MASKINI HILO NI KOSA LAKO". Jifunze.
Kuna tajiri mwingine anaitwa JACK MA huyu ni mmiliki wa ALIBABA. Yeye anasema hatua kuja duniani kufanya kazi tu mpaka siku ya kuta bali tulikuja kuishi maisha yetu. Anasema kuifanya kazi tu mpaka mwisho wa maisha yako utakuwa hujawahi kuishi maisha yako. Anasema siri ya mafanikio ni kutafuta kazi ambayo utaifanya kwa miaka mitano Kisha iwe imekupa pesa za kuishi maisha yako. Tafuta mpaka upiate. Kama hujaipata tafuta tu. Kama bado hujaipata watafute waliokwishaipata.
Unaona mawazo hayo? Man, I love that. So..
Usikae tu unaenda kazini tu kila siku mwisho itakuwaje?
Na kama wewe ni mwanafunzi hii ni habari njema sana maana ukiamua kujifunza vitu hivi sasa hivi ukavifanyia kazi, then I assure you miaka miwili au mitatu mbeleni wakati wenzako wanasambaza CV kuomba ridhaa ya kuingia kundi la kwanza la umaskini wewe utakuwa unanunua gari lako la pili au hata kiwanja na huenda umeanza kujenga kulingana tu na ndoto zako ni zipi.
Waingereza wanasema LIFE BEGINS AT 40. Yaani maisha huanza ukiwa na miaka 40. Kwa maana kwamba ukiwa na umri huo hutakiwi kuwa unawaza ada za watoto zinatakiwa ziwepo ulishatafutaga siku nyingi ukiwa na miaka 20-39. Wakati ukifika miaka 40 unapaswa uwe na nyumba gari urithi kwa familia yako biashara zilizosimama nk. Siyo ndo unaandika CV kuomba kazi ya tatu ili kuongeza kipato.
Life begins at 40.
How old are you?