Je upo kama mimi? Nina marafiki wachache wa kweli, nawaza sana siku wakiniacha peke yangu

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,032
Yes, najua kaka zako, dada zako, wadogo zako au familia yako ya wewe na mkeo/mumeo pamoja na watoto ni muhimu kuliko marafiki zako lakini haimaanishi mtu usiwe na marafiki, marafiki ni watu muhimu pia(kwa kiasi)

Nakumbuka zamani nilikuwa na marafiki wengi sana, shule ya msingi ndio nilikuwa nao wengi sana na hawa kusema kweli hata kama sio mabesti bado tupo karibu (tumeishi tangu vitoto).

Sekondari nako wakawepo ila hapa nilifocus sana na wasichana maana ndo nilipoanza kuwa kijana. Form 5 naona circle haikukaa vizuri maana muda mwingi ilikuwa ni kitabu.

Chuoni marafiki walikuwepo ila ghafla tumemaliza chuo naona urafiki umebaki sana sana wa kwenye kukumbushiana mambo ya chuo kwenye groups za whatsapp.

Kazini hapa naona wengi washkaji tu, sio watu wa kusema ni mabesti kivile.

Anyway, kwa sasa nina marafiki watatu wale ambao hata nikiwa Mbeya wao wapo Kenya wanaweza kufunga safari kuja kunicheki (mabesti). Hawa wengine naona ni wa kupiga story za simba na yanga tu maisha yaende.

Nawaza sana endapo hawa watu wachache nilionao wakipatwa na mabaya nikibaki peke yangu itakuwaje.
 
  • Mshangao
Reactions: _ID
Rafiki duuhh walinimwaga sina hamu nae, watoto, familia ndiyo best zangu
 
Rafiki duuhh walinimwaga sina hamu nae, watoto, familia ndiyo best zangu
Mkuu marafiku ni muhimu pia ila kwa kiasi chake.

Nimewahi kukamatwa polisi nikaachiwa fasta tu kwasababu ya urafiki,

nimewahi kufulia nikasaidiwa fresh tu bure kwasababu ya urafiki

Nimewahi kulazwa hospitalini mkoa mwengine nikawa sio mpweke asante kwa marafiki

Hata hii ajira niliyonayo nmepata kwa msaada wa marafiki.


ndio familia ni muhimu lakini marafiki sio wa kupuuza
 
Back
Top Bottom